MTEGO wa DR.ULIMBOKA uko tayari...

movie mpya imetoka , produced and directed by Kamanda kova, starring ; jambazi la kikenya, screenplay: tanzania police forces, music by Kamanda kova, producer: DPP feleshi, Sponsor: Serikali ya Tanzania.

sinema hii imeletwa ketwu kwa hisani ya Serikali ya Tanzania, Jshi la Polisi na Usalama wa Taifa.
 
LAKINI WAELEWE kuwa WATABANA IPO SIKU WATAACHIA TU..... na TUTAPIGA BAO KAMA TUNAIMBA KWA RAHA ZETU. ndipo WATABAKI na AIBU.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
mimi namshauri atoe tamko akiwa huko huko alipo aite waandishi wa habari duniani kote na kutoa tamko akiwa hospitalini kwa jinsi ninavyo elewa wataalamu wanasema sheria hazivuki bahari nito teyari kukoselewa


We nani kakuambia Ulimboka ana mpango wa kurudi Tanzania kwa sasa kabla usalama wake haujahakikishwa?! Ulimboka ni mkimbizi kwa sasa mpaka hali iatakaporuhusu kurudi nchini...meaning 'mtandao' wa serikali hii utakapotoka madarakani!
 
Hebu tufafanulie kidogo mkuu, hapo Usalama wa Taifa wanahusika vipi?

Mi nina wasiwasi na hilo 'jambazi' ambalo Afande Seleko alituambia linaitwa Joshua Gitu Muhindi. Hapo hapo ndio kunaweza kuwepo link. Tangu lini jambazi akaenda kujitangaza mwenyewe kwenye geti la askari kanisani kwamba alifanya uhalifu?
 
Hilo jambazi lilienda kutubu kwa "gwajima" kanakwamba lilimteka na kumtesa dr. Ulimboka

kusomewa tu shitaka limekana!

kova fomulae
"like poles atracts each other & unlike poles repeal one onother"
 
CCM hawezi kushindana na technology, kama hata hilo suala la kumteka Dr. Ulimboka wameacha every trace, leo wataweza kushindana na technology.

Mimi naomba wamueleze Dr. Ulimboka huko aliko kuhusu huo mpango mchafu dhidi yake na serikali ya Kikwete.

Halafu Dr. Ulimboka akubali kufanyiwa mahojiano akiwa hukohuko aliko na kuyaweka kwenye U-tube kama alivyofanya wakati alipohojiwa Clouds FM baada ya kuokotwa Mabwepande.

Halafu tuona huyo JK na Kova wake wataweka wapi USO wao, maana hizo copy zitafika UN human rights na ICC the Hague.
 
Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya lililofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?

Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?
namshauri Dr.Ulimboka atumie zile mbinu zinazotumiwa na wasanii wa kundi la vinega.sio lazima afikishe habari kwa uma kupitia mainstream media,atumie mitandao kama JF,FB,youtube n.k.Ccm na Mahakama yake hawatakuwa na uwezo wa kuzuia.
 
Mtego dhaifu sana huo kesi iliyoko mahakamani
Ni ya mkenya yeye watekaji wake sio mkenya hivyo
Atawataja watu ambao hawana kesi mahakamani
 
Jana baada ya kumaliza mishemishe za siku nikarudi home; nikawa katika maongezi na wife kuhusu ajali za ZNZ, halafu nikabadili mada nikajisemea sijui Dr. Uli anaendeleaje huko south, wife akanikatisha akasema, "mume wangu usiongelee suala lililopo mahakamani!" nikaondoka kwenda kunywa castle.......
 
Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya lililofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?

Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?

Nalo hilo wazo lakini; try as hard as they may, bottom line ni kwamba ukweli utajulikana tu, Newtons 3rd law of motion inasema hivi "to every action there is an equal and opposite reaction" upo hapo, tafakari na kwa kuwa swala hili liko mahakamani tusilijadili hapa kwenye forum maana kadiri unavyojieleza sana ndivyo vivyo hivyo unavyojiachia kupigwa sucker punch" waache waendelee kuandaa mkikakati ya hujuma lakini kaa tulia ukweli wa sakata la Dr. ullimboka litaanikwa siku si nyingi. tulia, vuta pumzi, tafakari!!.One mistake one goal.

Jiulize: Anti virus software ziko kibao lakini mbona virus zinaendelea kutengenezwa?!
 
Kwakuwa
1. Aliweza kuongea akiwa mahututi hospital
2. Aliongea pia akiwa anakimbizwa ugenini kutibiwa
3.Anajua kingereza fasaha
Hivyo afanye press conference huko huko ughaibuni, asisubiri ukumbi wa maelezo.
 
Huyo "mkenya" alishawahi pigwa picha na kuanikwa magazetini? Kamanda Kova si alete picha?
 
Inaonekana hili suala la kwamba 'jambo lipo mahakamani' kwa hiyo lisijadiliwe limekuwa ni mjadala unaohitaji ufafanuzi. Mh Wenje alisema kuwa kuingilia mwenendo wa mahakama ndiyo hairuhusiwi, lakini kutaja tujio si kosa. Kwa nini wanasheria msitupatie ufafanuzi kamili wa suala hili ili jamaa wasilitumie kama kichaka? Kwa mfano gazeti la Mwanahalisi la jana karibu makala zake zote limeandika suala la Kova na igizo lake la mkenya, je hiyo ina maaana Mwanahalisi limeingilia mahakama? mimi hapa nachanganyikiwa na ninahitaji msaada. Mipaka ikoje?
 
DR.Ulimboka kashatoa taarifa zote za msingi ikiwemo kuwataja wahusika wakuu kama A.MSANGI na ABEID,wanachofanye serikali ni wehu fullstop
 
kisheria ni kwamba huyu dr kwa vile ni main witness anatakiwa ahojiwe na polisi au na tume ambayo imeundwa kuchunguza hii kesi, hata ulaya ni hivyo hivyo kama kesi iko mahakamani mshtakiwa au mshtaki anaruhusiwa kuongea na wapelelezi, tume ya uchunguzi au na lawyers wake...na sio waandishi wa habari kwa sababu inaweza kuharibu uchunguzi so yes kujibu hoja yako hapo serikali imecheza kweli kwa kukimbilia mahakamani kwa sababu walijua hii kesi isipofika mahakamani huyu jamaa akarudi itakua kasheshe...well done TISS
 
Back
Top Bottom