VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya lililofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?
Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?