Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Ajaribu biashara ya kufuga nguruwe hukohuko
 
Mkuu kama yupo Deira akiishiwa pesa,mwambie awe anaenda Dubai Marina jioni, karibu na Dubai municipalily kuna cruise ships zinapaki,vyakula ni bure na hata kubeba ni ruksa, watanzania wenzangu acheni roho za kishetani,yaani mtu anaenda kutafuta watu wanatukana, akikaa hapa akasema hakuna fursa, wanatukana yaani basi tu.
Wacha nitamwambia akiingia online mkuu, hauna umbali sio
 
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi

Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu.

Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua

Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo

Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha

Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu

Natanguliza Shukrani[emoji1545]


View attachment 2275923View attachment 2275925View attachment 2275926
ktk vitu cwezi kufanya kutoka mahala kabla ya koneksheni.
 
Vijana mna mambo mengi sana,

Sasa huyo mwenzio hata ujuzi wowote hana alafu anatafuta kazi ugenini kweli inaingia akilini.

Hiyo pesa aliyopewa na Bi Mkubwa kwa nini asifanye mtaji hapa Bongo ,sasa ona inateketea alafu hakuna mwanga wowote.

Wakati mwingine ni vizuri kutulia na kufanya mambo kwa uhakika ,siyo kubahatisha ni hatari sana.
 
Awe anaulizia yale makampuni ya uwakala yamuunganishe na kazi na hapo ndipo itakapokuwa rahisi kwake kupata kazi,Dubai,Oman ama nchi zilizoendelea kazi nyingi za kufanya hupitia kwa agents
 
Haya maneno yaongee ukiwa na shida ndio yata make sense
Nauli ya dubai ni sh ngap au alienda bure ?? Sisemei maskini alieko bongo bali maskini alietumiaa pesa kibao nauli dubai kusaka maisha
 
Uzuri wa Dubai huwezi kufa njaa,
Kuna supermarket za kwa ajili ya watu wasio na hela.

USHAUR wangu:
Aendelee kupambana uko uko,
Asikae sehemu Moja mjini anashangaa shangaa tu.

Aende hata masaar au hata maeneo ya KAY,
Kule Kuna project nyingi Sana za ujenz zinaendelea, Hawez kukosa hata kibarua cha kubeba zege.
Nilitaka nimwambie aje hata huku Abudhabi kuna construction sites nyingi sana kila uchwao Majengo mapya yanaporomoshwa atoke huko Dubai mbona atapata kibarua.Mwanaume ni kupambana.
 
SAFI sana na mwambie akomae hapo Dubai mpaka kieleweke na kama amenities mafunzo ya jeshi mwambie ukumbuke zoezi la uvumilivu,la kupiga mesitini usiku kucha,akomae hapo
Mkuu sikufichi nilivyoweka huu Uzi na kusoma komenti 7 za mwanzo nilijuta na kuandika Uzi wenyewe, ila nashukuru Mungu wamekuja watu wenye moyo kama wako na kwa michango hii michache jamaa atapata mwanga na kujua wapi pa kuanzia, Nashukuru sana
 
Yani tunawaona waburundi wanavo force na vi birika vyao vya kahawa na wanakaa hadi 6 kwenye chumba na wananidhamu ya pesa hao hadi wanafanikiwa kujitegemea fresh tu,leo mtu anamshangaa mwewnzie alie enda kutafuta maisha Dubai me namshauri akaze hadi dakika ya mwisho wala asifikirie kurudi bongo mambo yatafunguka tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom