Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Boss Man

JF-Expert Member
Feb 10, 2022
458
991
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi

Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu.

Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua

Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo

Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha

Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu

Natanguliza Shukrani

Screenshot_20220628-215857.jpg
Screenshot_20220628-215941.jpg
Screenshot_20220628-215958.jpg
 
Ivi una endaje sehem tena nchi za watu ukiwa na plan A tu...yaan wabongo hapo ndo tunapo feliii...!!
Ngoja ni kupee idea ya kumsaidia huyo jamaa wakoo ikitik urudi hapa uje kunipa mrejesho maana mimi ni jobless.

Nampa pongezi za kufika huko dubai inaoneka jamaa kajitoa ..Ilaa anatakiwa afutee kabsa swala la kuajiriwa na atafute mpunga(hela) kidogo.

Dubai kama dubai mimi na chojua ni soko kubwa sana la vifaa vya electronic used kwa nchi zetu.

Sasa kwa sababu yuko eneo husika asikae kindeziii asome ramani zote mzigo unapo patikana na ikibidi achague yeye mwenye ile vile vifaa grade A yani vile vitu piruu.

Akisha vipata asome ramani ya kuvituma na jinsi ya kuvitoa bandarani kwa bei isaiyoo umiza lakin arudi Bongo kujakupambana sasa.

Angekua anaijua Zanzibar ninge mwambia aende kutafuta frem kule kwa MCHINA alafu afungue goli kulee alafu utakuja niambia.
 
Aliendaje kienyeji hivyo? No recconaisance?

Alitegemea kushukia wapi? Kwa nani...
Swala la kufikia kwake halikuwa tatizo, Kuna Mahali yupo anaishi fresh ila ndio hivyo anatumia tu Hela za Bongo alizoenda nazo kujikimu
 
Ivi una endaje sehem tena nchi za watu ukiwa na plan A tu...yaan wabongo hapo ndo tunapo feliii...!!
Ngoja ni kupee idea ya kumsaidia huyo jamaa wakoo ikitik urudi hapa uje kunipa mrejesho maana mimi ni jobless...
Hizi mentality za kizamani,wanigeria walizamia ulaya hawajui watafikia wapi,akilini kucheza mpira..na wakatusua
 
Nimekumbuka wimbo wa bongo.

Dar e salaam wake prof jay Kuna mstari anasema "safari bado ngumu jamani tusiende kwa nguvu za ndumu, Jonas kiwira wasalamie Washington"

MY TAKE
Jamaa akaze unapofika mjini kama huna connection au hata kama unayo mji unatabia yakukupokea yani Kuna time utapitia magumu hayo mpqka unawaza dah! nirudi home au nimelogwa ila ukikomaa badae mambo yanatulia na unakuwa na uelewa so akaze mwambie sisi tunasubilia mwili wake pale kwa JK akomae

Mungu ajawahi mtupa mja wake anayekaza na kiza kikizidi basi mwanga unakaribia.
 
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, Nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi

Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu

Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua

Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo

Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha

Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu

Natanguliza ShukraniView attachment 2275923View attachment 2275925View attachment 2275926
Kazi bongo zimeisha,, hao waarabu siwaelewi kabisa .. siwezi kwenda nchi yoyote kwa ujira wowote hata kama kuosha gari moja nilipwe dola 20..sikuzaliwa kwa ajili hio thamani yangu ni kubwa sana ..bora nibaki bongo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom