Jebel
JF-Expert Member
- Jul 10, 2021
- 383
- 2,605
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi
Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu.
Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua
Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo
Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha
Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu
Natanguliza Shukrani[emoji1545]
View attachment 2275923View attachment 2275925View attachment 2275926
Kwa uzoefu wangu mdogo wa kuishi Dubai kwa miaka michache kuna mambo naweza kukushauri umshauri huyu rafiki yako:
Kwanza kwa mtu mweusi kazi ambayo uhakika wa kupata kwa mda mfupi sana ni SECURITY NA CLEANING. Kuna kampuni nyingi sana ambazo zinatafuta watu kila siku mwambie atafute kampuni ndogo ndogo asitafute kampuni kubwa kama Transguard.
Mshahara huwa si chini ya 1M ya Kitanzania. Unapewa chumba cha kulala, usafiri kila unapoenda kazini, bima ya afya, na ticket kila baada ya miaka 2/3.
Akifanya kazi miaka 2au 3 atakuwa ameshazoea mji anaweza kuamua kuchua “bed space” kisha akafanya mishe yake mwenyewe ili atoboe haraka.
NB. -Akitegemea msaada wa wabongo kazi anayo.
- Kama inawezekana nicheki PM ili tuone namna ya kumsaidia japo wabongo ukiwasaidia mara nyingi wanaharibu na kukubaribia jina