Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Huu ni upumbavu mwingine wa Tanzania diaspora, wapopo hawajuani ila wakishajua ni mpopo mwenzao they always help ndio maana remittance ya wapopo ni mara 100 ya kwetu,Kenya au Zimbabwe ni almost 1%ya GDP ya nchi nzima, unaongea upumbavu huu na ukifa unataka uzikwe na watanzania wote waliopo hapo wakati unaishi selfish life.
hao wapopo ni binadam? Au akili yangu ndio ipo mbali
 
Sawa nitamwambia maana jamaa amedai yuko sehemu inaitwa Deira
Mkuu kama yupo Deira akiishiwa pesa,mwambie awe anaenda Dubai Marina jioni, karibu na Dubai municipality kuna cruise ships zinapaki,vyakula ni bure na hata kubeba ni ruksa, watanzania wenzangu acheni roho za kishetani,yaani mtu anaenda kutafuta watu wanatukana, akikaa hapa akasema hakuna fursa, wanatukana yaani basi tu.
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wa kuishi Dubai kwa miaka michache kuna mambo naweza kukushauri umshauri huyu rafiki yako:

Kwanza kwa mtu mweusi kazi ambayo uhakika wa kupata kwa mda mfupi sana ni SECURITY NA CLEANING. Kuna kampuni nyingi sana ambazo zinatafuta watu kila siku mwambie atafute kampuni ndogo ndogo asitafute kampuni kubwa kama Transguard.

Mshahara huwa si chini ya 1M ya Kitanzania. Unapewa chumba cha kulala, usafiri kila unapoenda kazini, bima ya afya, na ticket kila baada ya miaka 2/3.

Akifanya kazi miaka 2au 3 atakuwa ameshazoea mji anaweza kuamua kuchua “bed space” kisha akafanya mishe yake mwenyewe ili atoboe haraka.

NB. -Akitegemea msaada wa wabongo kazi anayo.
- Kama inawezekana nicheki PM ili tuone namna ya kumsaidia japo wabongo ukiwasaidia mara nyingi wanaharibu na kukubaribia jina
Huu ndio msaada,lakini unakuta mwanamme mzima anamkashifu mwanaume mwenzie kisa ameenda kupambana kutafuta maisha,mambo yakaenda nje ya matarajio, watanzania sisi wajinga sana.
 
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi

Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu.

Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua

Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo

Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha

Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu

Natanguliza Shukrani[emoji1545]


View attachment 2275923View attachment 2275925View attachment 2275926
yuko dubai sehemu gani? na ana driving licen
 
Deira azame kwenye maduka ya wachina,walebanon,wairan... atapata kazi yeyote hapo,Deira ni mjini hapo kuna heka heka nyingi sana,awasaidie hata wanigeria kubeba mizigo yao apate chochote huku akiuzowea mji,

Unatakaje mtu asaidiwe na hujaweka hata jina lake au jinsi ya kumpata? Watu watampataje?

Deira kuna Mahoteli kibao azame ndani akafanye hata usafi ili kusukuma siku,mwambie jamaa yako asirudi kindezi akomae,mwanzo hua ni mgumu,asisikilize kelele za waliozowea kushinda vijiwe vya kahawa na kulaumu Serikali tu,

Akiona Dubai mambo magumu apande basi Mpaka Abudhabi kule kuna kazi za siku hatokosa,ni 1hour kwa basi Dubai mpaka Abudhabi,

Msisitize jamaa akomae hata kama atakua analala nje siku za mwanzoni.
Pia angejaribu sehemu za pembeni mwa mji, kama Jabel Al, Al Quiz, Rashidia na Al Qusas kuna ware house nyingi sana, lakini pia akiiona mambo hayaendi mwambie aende UNION BUS STOP ni hapo hapo Deira, pembeni kidogo mwa BAN YAS SQUARE, kama bado yuko vizuri, apande Bus ajaribu pia SHARJAH (Industrial area) au AJMAN FREE ZONE.
 
Watanzania sio watu trust me.
Ni washenzi wa mwisho hasa kwenye hizi diaspora zetu,angalia hapa mtanzania mwenzetu he take a huge risk kwenda Dubai kutafuta riziki, but imekua ngumu kwake na kabla ya sisi kumpa moyo aendelee kupigana ili lengo lake lifikiwe ndio kwanza tunamkatisha tamaa kwa kauli zetu za kiroho mbaya, ajira humu kila siku kuna mada mara ohoo ualimu, afya,polisi ,uhamiaji, magereza na zote hizi bila connection ni zero,sasa mwenzetu kaamua kujilibua Dubai sisi huku tunamkatisha tamaa, please mkuu kama unasoma uzi huu ,usikate tamaa pigana huko mpaka kieleweke maana riziki ni popote ni ni just 2min,right place ,right time ...good luck
 
Umesema kweli Mkuu, pia angejaribu sehemu za pembeni mwa mji, kama Jabel Al, Al Quiz, Rashidia na Al Qusas kuna ware house nyingi sana, lakini pia akiiona mambo hayaendi mwambie aende UNION BUS STOP ni hapo hapo Deira, pembeni kidogo mwa BAN YAS SQUARE, kama bado yuko vizuri, apande Bus ajaribu pia SHARJAH (Industrial area) au AJMAN FREE ZONE.
Welldone done mkuu, mtafutaji huyu anahitaji mawazo kama haya sio kumkatisha tamaa
 
Inasikitisha sana hii Tanzania diaspora yetu ni majitu yenye roho mbaya ,roho za kishetani, uongo na chuki zenye jeoulsy ndani yake,huwezi kulinganisha na wapopo, wasomali,wakenya, even warundi sasa wanatupita katika kusaidiana, ikienda nje na ukasikia watu wanaongea kiswahili cha kitanzania, kimbia mbali na waogope kama ukimwi!,ukijichanganya tu wanakugeuza dili
Ukifika Dubai wana KIKUNDI chao cha kusaidiana wanakutana UNION pembeni mwa METRO STATION kila jioni ya siku ya IJUMAA fika hapo ukutane nao, ndio utajua mtanzania ni ng'ombe[emoji1][emoji1][emoji16]
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wa kuishi Dubai kwa miaka michache kuna mambo naweza kukushauri umshauri huyu rafiki yako:

Kwanza kwa mtu mweusi kazi ambayo uhakika wa kupata kwa mda mfupi sana ni SECURITY NA CLEANING. Kuna kampuni nyingi sana ambazo zinatafuta watu kila siku mwambie atafute kampuni ndogo ndogo asitafute kampuni kubwa kama Transguard.

Mshahara huwa si chini ya 1M ya Kitanzania. Unapewa chumba cha kulala, usafiri kila unapoenda kazini, bima ya afya, na ticket kila baada ya miaka 2/3.

Akifanya kazi miaka 2au 3 atakuwa ameshazoea mji anaweza kuamua kuchua “bed space” kisha akafanya mishe yake mwenyewe ili atoboe haraka.

NB. -Akitegemea msaada wa wabongo kazi anayo.
- Kama inawezekana nicheki PM ili tuone namna ya kumsaidia japo wabongo ukiwasaidia mara nyingi wanaharibu na kukubaribia jina
Asante sana, Nakuchek mkuu kwa miongozo zaidi
 
Deira azame kwenye maduka ya wachina,walebanon,wairan... atapata kazi yeyote hapo,Deira ni mjini hapo kuna heka heka nyingi sana,awasaidie hata wanigeria kubeba mizigo yao apate chochote huku akiuzowea mji,

Unatakaje mtu asaidiwe na hujaweka hata jina lake au jinsi ya kumpata? Watu watampataje?

Deira kuna Mahoteli kibao azame ndani akafanye hata usafi ili kusukuma siku,mwambie jamaa yako asirudi kindezi akomae,mwanzo hua ni mgumu,asisikilize kelele za waliozowea kushinda vijiwe vya kahawa na kulaumu Serikali tu,

Akiona Dubai mambo magumu apande basi Mpaka Abudhabi kule kuna kazi za siku hatokosa,ni 1hour kwa basi Dubai mpaka Abudhabi,

Msisitize jamaa akomae hata kama atakua analala nje siku za mwanzoni.
Asante sana kiongozi, Wacha jamaa akiingia online nitampa miongozo yote hii kazi ibaki kuwa kwake
 
Ni washenzi wa mwisho hasa kwenye hizi diaspora zetu,angalia hapa mtanzania mwenzetu he take a huge risk kwenda Dubai kutafuta riziki, but imekua ngumu kwake na kabla ya sisi kumpa moyo aendelee kupigana ili lengo lake lifikiwe ndio kwanza tunamkatisha tamaa kwa kauli zetu za kiroho mbaya, ajira humu kila siku kuna mada mara ohoo ualimu, afya,polisi ,uhamiaji, magereza na zote hizi bila connection ni zero,sasa mwenzetu kaamua kujilibua Dubai sisi huku tunamkatisha tamaa, please mkuu kama unasoma uzi huu ,usikate tamaa pigana huko mpaka kieleweke maana riziki ni popote ni ni just 2min,right place ,right time ...good luck
Mkuu sikufichi nilivyoweka huu Uzi na kusoma komenti 7 za mwanzo nilijuta na kuandika Uzi wenyewe, ila nashukuru Mungu wamekuja watu wenye moyo kama wako na kwa michango hii michache jamaa atapata mwanga na kujua wapi pa kuanzia, Nashukuru sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom