Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Uzuri wa Dubai huwezi kufa njaa,
Kuna supermarket za kwa ajili ya watu wasio na hela.

USHAUR wangu:
Aendelee kupambana uko uko,
Asikae sehemu Moja mjini anashangaa shangaa tu.

Aende hata masaar au hata maeneo ya KAY,
Kule Kuna project nyingi Sana za ujenz zinaendelea, Hawez kukosa hata kibarua cha kubeba zege.
Sawa nitamwambia maana jamaa amedai yuko sehemu inaitwa Deira
 
Mwambie ajiongeze kama yatima asitegemee kubebwa, japo huko napo wabaguzi wa dini, akiweza abadili dini kwa mda
 
Kazi zipo tele, maadamu pa kuanzia, aende kwenye mahotel, migahawa, magodown, maduka, masupermarket, magarage, mashuleni, vyuoni, viwandani,msikitini, nk akaombe Kazi ya usafi hata kwa kujitolea.
Atafaulu maana popote penye watu wabaya na wema wapo sema tu ajapata chance ya kukutana nao.
 
fumba macho alaf ufikirie na utoe jibu,fikiria ni jumapili tulivu umekaa home unacheza na watoto,mara anakufuata H.GIRL na kukwambia"baba kuna mgeni" unamwambia "mwambie aingie ndani"ile anaingia ana mizigo kama yote,sio ndugu yako,ila ni mwanakijiji mwezako huko bush kaja kutafuta kazi na ameona aje kuishi kwako tena bila taarifa.ukishapata jibu ndo unaweza kuwalaumu hao wa tanzania wa dubai,.......kumbuka huyo jamaa hana udugu wa damu na hao watanzania na alivoenda hakuwasiliana nao kabla,,,,tuache uswahili ndo una2ponza bhana...samahani kama nimekukwaza


,
Mfano wako mbona hauconnect!!! coz jamaa sio kwamba kaenda kuishi kwa hao wabongo, Bali ameenda akiwa kajipanga Mahali pa kuishi, Sasa kama amepambana kwa bidii zake kutafuta kazi na ikashindikana ni vibaya kutaka msaada/miongozo kutoka kwa Watanzania wenzake ambao wamemtangulia yeye kwenda huko?
 
Kilichomtuma aende na hajui anaenda kufanya nini ni nini?

Mshauri arudi apambane tu huku

Hii ndio shida ya kufake maisha

Tujitahidi kujikubali kuishi kwa uwezo wa maisha Mungu aliyoturuzuku kwa muda huo
Huku tukipambana kutafuta ya mbele yenye uhalisia
Usimlaumu nchi yetu ni ngumu sana, kijana ameenda kupambania kombe lake hayo ni matokeo tu inabidi akubaliane nayo na apambane aweze kutimiza lengo lake
 
Tatizo ni kuwa wabongo ukimpa connection lazima alete tabia za ajabu/u-snitch.

Kuna dogo mmoja tulimsaidia ila alichokuja kufanya... Sasa hivi Hata kuchangamana na wabongo wenzio unaona nuksi tu.

Bado ana nafasi apambane
Wabongo watu wa kuharibu sana yani😂 mwanzo anakuwa kama mtu ila ukimpa line anakudidimiza wewe uliemtoa.😂😂😂
 
Umeweza ishi bongo pasipo na mfumo unashindwa vipi ishi nchi zenye mifumo ya maisha tayari
Je kama mifumo yao inabagua? Coz jamaa amedai ngozi nyeusi haiaminiki kabsa Yani Hadi uingie katika system connection ya maana inahitajika, Wahindi na Wafilipino mifumo ndio imewakubali....Sasa sijui ni mifumo kuwakubali au ni ujanja wao tu pamoja na kubebana wao kwa wao
 
Wabongo watu wa kuharibu sana yani[emoji23] mwanzo anakuwa kama mtu ila ukimpa line anakudidimiza wewe uliemtoa.[emoji23][emoji23][emoji23]
Iyo tabia ya mwanadamu au ya mbongo!!? Kama unaamua kumsaidia mtu usiangalie nyuma!

Maana Kuna sehemu watu wamefika inawezekana pia ni mmojawapo,kwa kusaidiwa hapo walipo! Hao wangetaka kuangalia nyuma kwa kusema hayo, ungefika?
 
Je kama mifumo yao inabagua? Coz jamaa amedai ngozi nyeusi haiaminiki kabsa Yani Hadi uingie katika system connection ya maana inahitajika, Wahindi na Wafilipino mifumo ndio imewakubali....Sasa sijui ni mifumo kuwakubali au ni ujanja wao tu pamoja na kubebana wao kwa wao
Shida ndo hio huwezi badili rangi Ingekuwa dini unabadili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom