Mtangazaji 'Diva The Bawse' aaga rasmi Wasafi Media

Mtangazaji 'Diva The Bawse' aaga rasmi Wasafi Media

Wakuu kweli BUSHOKE sio bwege kama vile alivyoimba. Nitakuwa wamwisho kuamini kuwa ule ujinga aliouonesha huyu mwanamama umepita bila madhara yoyote kwa wasafi na Diva.
Imekuaje hii conversation ya Bushoke na Diva?
 
Itafute tu mtandanoni ujionee maajabu Mkuu.
Asee nimeicheki hiyo interview YouTube seriously itakuwa ina mchango mkubwa kwa huu mshangazi kuondoka wasafi nimesoma comment mwanzo mpaka mwisho watu wote wanampopoa Diva,
Bushoke was calm and relaxed hata kama ndo Mimi nipo kwenye level ya management huu mshangazi usingebaki hapo
 
Na kizazi alifunga sijui kabla hata hajazaa masikini ya Mungu
Dah imam Hussain ibn Ali aliyeuwawa kikatili kuutetea na kuulinda uislamu dhidi ya dhulma ukandamizaji unyanyasaji na uonevu amsamehe.

Screenshot_2025-07-09-18-01-08-90_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg
 
Asee nimeicheki hiyo interview YouTube seriously itakuwa ina mchango mkubwa kwa huu mshangazi kuondoka wasafi nimesoma comment mwanzo mpaka mwisho watu wote wanampopoa Diva,
Bushoke was calm and relaxed hata kama ndo Mimi nipo kwenye level ya management huu mshangazi usingebaki hapo
Alizingua sana
 
Mtangazaji maarufu na kipenzi cha mashabiki, Diva Gissele Malinzi almaarufu Diva The Bawse, ametangaza rasmi kuachana na kituo cha Wasafi Media, akieleza kuwa amefikia hatua ya kuanza ukurasa mpya katika maisha yake ya kazi.

Kupitia ujumbe uliojaa hisia, shukrani na upendo mkubwa kwa familia ya Lavidavi na timu nzima ya Wasafi, Diva amesema amewasilisha barua yake ya kuondoka mapema leo asubuhi, ameeleza kuwa kipindi cha Lavidavi kilikuwa moja ya sura nzuri zaidi katika taaluma yake, na kwamba kila usiku, kila sauti ya msikilizaji na kila ujumbe vilikuwa sehemu ya moyo wake.

"Tumejenga nyumba ya hadithi halisi za mapenzi, uponyaji, vicheko, ujasiri na mazungumzo ya kweli. Mmenilea, mmenisukuma, na mmenifanya kuwa bora zaidi," ameandika Diva.

Akiwaaga kwa heshima timu nzima ya Wasafi, kuanzia kwa watayarishaji, timu ya kidijitali, wahandisi wa sauti hadi uongozi, Diva amesema anaanza msimu mpya wa maisha, lakini akasisitiza kuwa huu si mwisho wa safari, bali ni pumziko la heshima.

"Popote nitakapokwenda, roho ya Lavidavi itaendelea kuishi. Endeleeni kupenda, kupona, na kuamini katika mapenzi."

Kwa miaka kadhaa, Diva The Bawse amekuwa sauti ya kipekee usiku katika redio ya Wasafi, akitoa nafasi kwa simulizi za mapenzi, mafanikio na changamoto za maisha, huku akibaki kuwa miongoni mwa watangazaji wenye ushawishi mkubwa Tanzania.

ITHIBATI ITHIBATI Mamaaaa!!
 
-Hivi unakosaje diploma jamani? Sheria ya media services imetungwa 2017 walikuwa na miaka nane, wangekuwa wajanja wangejiunga na Open university mapema.
 
Ila diva ana sura nyingi km agano la kale..!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom