Mtangazaji 'Diva The Bawse' aaga rasmi Wasafi Media

Mtangazaji 'Diva The Bawse' aaga rasmi Wasafi Media

At her age 37 yrs hana Nyumba ,hana ndoa hana mtoto anabidi kujitafakari Sana akumbuke Malinzi sio Baba yake hivyo anaweza asimpe urithi.
Umeongea Kwa hasira Sana mkuu.

Huyu bado binti mbichi kabisa
 
-Hivi unakosaje diploma jamani? Sheria ya media services imetungwa 2017 walikuwa na miaka nane, wangekuwa wajanja wangejiunga na Open university mapema.

mkuu hao hawahitaji Diploma kufanya kazi, waki focus kwenye social media ataendelea na kazi, Bongo tuna sheria zilizoshapitwa na wakati. chakushangaza zaidi ndio kwanza zinatungwa.
 
Mtangazaji maarufu na kipenzi cha mashabiki, Diva Gissele Malinzi almaarufu Diva The Bawse, ametangaza rasmi kuachana na kituo cha Wasafi Media, akieleza kuwa amefikia hatua ya kuanza ukurasa mpya katika maisha yake ya kazi.

Kupitia ujumbe uliojaa hisia, shukrani na upendo mkubwa kwa familia ya Lavidavi na timu nzima ya Wasafi, Diva amesema amewasilisha barua yake ya kuondoka mapema leo asubuhi, ameeleza kuwa kipindi cha Lavidavi kilikuwa moja ya sura nzuri zaidi katika taaluma yake, na kwamba kila usiku, kila sauti ya msikilizaji na kila ujumbe vilikuwa sehemu ya moyo wake.

"Tumejenga nyumba ya hadithi halisi za mapenzi, uponyaji, vicheko, ujasiri na mazungumzo ya kweli. Mmenilea, mmenisukuma, na mmenifanya kuwa bora zaidi," ameandika Diva.

Akiwaaga kwa heshima timu nzima ya Wasafi, kuanzia kwa watayarishaji, timu ya kidijitali, wahandisi wa sauti hadi uongozi, Diva amesema anaanza msimu mpya wa maisha, lakini akasisitiza kuwa huu si mwisho wa safari, bali ni pumziko la heshima.

"Popote nitakapokwenda, roho ya Lavidavi itaendelea kuishi. Endeleeni kupenda, kupona, na kuamini katika mapenzi."

Kwa miaka kadhaa, Diva The Bawse amekuwa sauti ya kipekee usiku katika redio ya Wasafi, akitoa nafasi kwa simulizi za mapenzi, mafanikio na changamoto za maisha, huku akibaki kuwa miongoni mwa watangazaji wenye ushawishi mkubwa Tanzania.

Shidaya huyu dada wa kihaya ni afya ya akili...iko siku ataingia studio na miwani ya welding
 
It's like a jungle in this habitat" sio wote wanaweza na shida ni kupata following...; ila kama huyu tayari ana wasikilizaji ni rahisi kuingia na kwenye podcast; yaani podcast kwa sasa ni muhimu sana na kitu cha lazima kwa mtoa habari yoyote (in short sio huku tu teknolojia imefanya industry zote kuwa ngumu, kuna a lot of competition) inabidi ku capitalize kwenye following yako
Podcast ni mahali pa kupiga soga, kutoa elimu na mara nyingi kujadili jambo moja kwa kirefu. Radio na TV bado vipo sana, tatizo ni mazingira ya habari ya bongo ni duni sana na content ni haba kwa sababu vyombo vya habari viko kama PR firm zaidi.
 
Media Houses are a dying breed (evolving) it's time for podcast.., kwahio kama una following na content anzisha podcast yako ila usiache kwenye media houses huko unakuwa unakwenda part time hata usipolipwa inakuwa ni kama promo tu... na kuongeza connection...
You're too naive,
Legacy media zipo sana, podcast sio sehemu ya kupata breaking news na uchambuzi wa habari.
 
Watangazaji lazima wawe na diploma lakini watu tunaowapa dhamana na watunga sheria za nchi wanatakiwa wajue kusoma na kuandika tu. Tanzania nchi yangu.
 
Asee nimeicheki hiyo interview YouTube seriously itakuwa ina mchango mkubwa kwa huu mshangazi kuondoka wasafi nimesoma comment mwanzo mpaka mwisho watu wote wanampopoa Diva,
Bushoke was calm and relaxed hata kama ndo Mimi nipo kwenye level ya management huu mshangazi usingebaki hapo
Havihusiani bhana
 
Back
Top Bottom