Mtandao wa Airtel unasumbua mno maeneo ya mikoa ya Pwani

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,989
Habari zenu wana jamvi,

Katika siku za karibuni mtandao wa simu wa Airtel Tanzania unasumbua sana maeneo ya Dar es Salaam, Mkuranga, Kibiti, Rufiji hata Kilwa. Hili tatizo limewahi kujitokeza siku za nyuma lakini wenye mtandao wao wakakaa kimya kama vile hakijatokea kitu.

Nitaeleza siku ya jana tarehe 2 May, 2021. Usumbufu uliokuwa unapatikana kwa watumiaji wengi wa Airtel ni kama ifuatavyo:

1. Unapiga namba (ya Airtel) kwa nyakati tofauti unaambiwa haipatikani na wakati namba kwa hiyo iko hewani muda wote na haiko busy.
2. Unapiga namba simu inasearch tu haisemi kama inapatikana au haiko hewani na inakatika bila majibu.
3. Internet yasumbua sana.

Hivi wanajua usumbufu na hasara wanazosababishia wateja wao? Chukulia mtu ni mfanyabiashara umepigiwa simu akupe order hupatikani, fasta anapiga kwa mwingie na mtu huyo tayari amepoteza mauzo.

Airtel wana upuuzi sana, wanaweza hata kukupa GB 3 kwa elfu 2 lakini mtandao ukatafute mwenyewe. Mwisho kifurushi kinapitwa na muda ndio imeisha hiyo. Kama wameshindwa kutoa huduma bora, waache. Soko hilo huru tutahamia kwingine. Kinachokera zaidi ni tabia yao ya kukaa kimya bila kutoa taarifa kwamba kuna shida ya kimtandao. Haikakaa poa kibiashara.

Nina imani wahusika wanapita hapa. Wachukue hii in a positive way lest they loose me for the fisrt time.

Kudos.
 
Wapuuzi, jana nikawa napata mbili tatu moja moto moja baridi na kitimoto ili nije kulipa kwa Airtel Money. Aiseee, mtandao ukazingua. Nisingekuwa na njia mbadala ningeonekana muhuni. Wanazingua hasa, internet nilishawahama niko Halotel.
 
Hafu hiyo mitaa ya Kibiti Kifumangao huko Airtel ina watumiaji wengi sana. Wakianza huo huuni watu watawahama.

Labda sababu ni hizi mvua za hapa na pale mawimbi hayakai vizuri.
 
Wanazingua sana, text unaweza kutuma asubuhi ikafika jioni au isifike kabisa. Unaweza kutumiwa text ikabaki kwenye minara yao tu, baadae zinakuja lawama. Watu wanalalamika napiga simu yako inaita tu, wengine naambiwa haipatikani wakati simu umewasha na inasoma network.

Nimeona shida kubwa ni hizi line za 4G haswa ukiwasha 4G kwenye simu ndiyo majanga yanazidi. Kikubwa weka 3G kwanza na mzigo ukisumbua weka Edge tu na internet sahau.

Na vifurushi hawajarudisha vya zamani, tuna kila sababu ya kuhama. Turudi TTCL tu.,1000 siku 5(dk ,sms, internet), kwa mwezi matumizi hayazidi 10,000/=.
 
Mbona mitandao mingine maisha yanaendelea kama kawaida.
 
Wanatusumbua sana. Wapuuzi mno.
 
Yaani kwenye data utawafurahia, una bando lako kila ukitaka kutumia mtandao unazunguka tuu. ukiwapigia wanakuuliza unatumia simu ya aina gani.

Nilishatupa line yao tena chooni baada ya kuikatakata.
 
Niko pwani likizo ya mwezi 1 natumia vzuri bila ttzo llte mkuu pole kwa changamoto hiyo, nikutakie Ramadan Kareem
 
Yaani Kama huku kwenye mradi wa bwawa la umeme Rufiji ndio majanga zaidi aisee, Yaani kukaa siku tatu bila mnara kusoma ni kawaida Sana kila wiki
 
Yaani kwenye data utawafurahia, una bando lako kila ukitaka kutumia mtandao unazunguka tuu. ukiwapigia wanakuuliza unatumia simu ya aina gani.

Nilishatupa line yao tena chooni baada ya kuikatakata.
Hahahaah mkuu una hasira sana.
 
Habari zenu wana jamvi,

Katika siku za karibuni mtandao wa simu wa Airtel Tanzania unasumbua sana maeneo ya Dar es Salaam, Mkuranga, Kibiti, Rufiji hata Kilwa. Hili tatizo limewahi kujitokeza siku za nyuma lakini wenye mtandao wao wakakaa kimya kama vile hakijatokea kitu.

Nitaeleza siku ya jana tarehe 2 May, 2021. Usumbufu uliokuwa unapatikana kwa watumiaji wengi wa Airtel ni kama ifuatavyo:

1. Unapiga namba (ya Airtel) kwa nyakati tofauti unaambiwa haipatikani na wakati namba kwa hiyo iko hewani muda wote na haiko busy.
2. Unapiga namba simu inasearch tu haisemi kama inapatikana au haiko hewani na inakatika bila majibu.
3. Internet yasumbua sana.

Hivi wanajua usumbufu na hasara wanazosababishia wateja wao? Chukulia mtu ni mfanyabiashara umepigiwa simu akupe order hupatikani, fasta anapiga kwa mwingie na mtu huyo tayari amepoteza mauzo.

Airtel wana upuuzi sana, wanaweza hata kukupa GB 3 kwa elfu 2 lakini mtandao ukatafute mwenyewe. Mwisho kifurushi kinapitwa na muda ndio imeisha hiyo. Kama wameshindwa kutoa huduma bora, waache. Soko hilo huru tutahamia kwingine. Kinachokera zaidi ni tabia yao ya kukaa kimya bila kutoa taarifa kwamba kuna shida ya kimtandao. Haikakaa poa kibiashara.

Nina imani wahusika wanapita hapa. Wachukue hii in a positive way lest they loose me for the fisrt time.

Kudos.
Huku Zanzibar ndo kabisa, ukiwapigia simu wanakuuliza unatumia simu ya aina gani? Nikamwambia huyo dada natumia ili hali situmii Tecno na jibu lake lilikuwa ndo maana kwa sababu simu za Tecno zinasumbua sana, nakumwuliza tena tangu lini? Baadae nikaona huyu naye ni mpira ramuli tu nikaachana naye.
Kifupi airtel kwa Zanzibar na mikoa ya Pwani ni shida, nenda hata hapo kibaha shida
 
Back
Top Bottom