Mtandao gani wa simu hujawahi kuuelewa au huwa unahisi unasumbua sana maeneo mengi?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,994
17,893
Mtandao gani wa simu hujawahi kuuelewa au huwa unahisi unasumbua sana maeneo mengi na hujawahi kuuelewa

Mimi ni hii hapa sijawahi kuwaelewa

1.TTCL=Hawa hawajulikani kama ni kunguru au ni mwewe kiujumla ni watu wa hovyo wapo rafu tu kama geto la mvutabangi hawatabiliki saa yoyote wanaweza kulala yooo unaweza nunua umeme kwa TPesa ukalipia malipo ya umma ushaweka hela za watu msg ikaja kurudi 2025 hapo ushaonekana mwizi, hata mtandao wao haueleweki

2.AIRTEL=Hawa sehemu nyingi huwa hawapo utashangaa magomeni wapo ubungo hawapo mbezi wanakamata kibamba hawakamati, hawa hata kama una safari usiwaaamini kuwatumia utajuta sehemu nyingi ni mizinguo

3.TIGO: Hawa nao sijawahi kuwaelewa kote nilipowahi kupita lazima mtandao uwe na kasoro tu wana tabia ya kubadilika badilika mfano January mtandao unaweza ukawa unakamata vizur eneo moja ghafla feb mtandao ukawa haushiki kbs eneo hilo hilo hadi najiuliza hawa mitambo yao huwa wanakodi na kurudisha au coz hawanaga permanent kbs ya mtandao pia mtandao wao haujawahi kuwa strong lazima uwe slow slow tu.

4.HALOTEL: Hawa ni mabingwa kufake data gb 1 wakikupa ujuwe wamekupa mb 500 yaani ni sawa na mchele nusu uwekwe hamira utoke kilo moja ndo wataalam wa kunyonya mabando na pia hawa wana 4G ya mchongo....3G yao au H+ ina kasi kuliko 4G yao...Hawa sidhani km wana 4g...Mimi nilipo mtandao upo vizur sana lakini huwezi amini huwa naset 3G ndo inakua fasta kuliko 4G yao ya mchongo...fatilieni hii mtagundua kuwa wana 4G ya uwongo

Kwa mtazamo wapo unadhani ni mtandao upi hujawahi kuuelewa?
 
Mimi ni Airtel na Voda ndo sijawahi wakubali ila Voda ndo the best Kwa Kila kitu
 
Voda sijawahi kuuelewa huo mtandao hata bure, japo tigo ina vipengele vyake ila bora mara 100 na ndio nayotumia kwa mawasiliano yote . Kwa kuwa simu ina line mbili, nimemalizia na airtel japo siungi bando wala nini huwa natumia huduma ya pesa tu kuwatumia ndugu mkoani
 
Voda kwa kukata 100 zisizoeleweka hawajambo, sema mtandao wao ni hatari hata porini 4G,

Tigo ni kama haitaki wateja wa kanda ya ziwa maana network hovyo

Halotel unaweza ona mtandao unasoma 4G ila hata meseji za wasap haziingii
 
Halotel nilitumiwa msg saa Tisa jioni ifika Kesho yake saa Moja asubuhi ,ukipiga simu inakata yaani Kwa ufupi halotel ni Bure bireshi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom