Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Habari Wadau.
Imenibidi niseme tena maana najua imeshasemwa sehemu kibao. Kwa serikali yetu hii ilivyo kasi katika kutuletea maendeleo naona suala la mtandao wa internet limekuwa tatizo kubwa hata katika awamu hii.
Mfano unaenda TANESCO kujaza fomu ili uwekewe umeme lakini inamaliza hadi wiki 3 kwa kuambiwa kuwa mtandao shida control number hazitoki. Hii hali pia iko ofisi za NIDA, NSSF na ofisi nyingine nyingine tu.
Tunachotaka kujua ni kweli kwamba mtandao hamna au kinahitajika kitu cha kuchokonoa mtandao? Maana wengine wanaingia wanatoka na huduma wanayoihitaji wanakwambia walibahatisha tandao!!!!!!
Kupitia TBC 1 serikali yetu imekuwa ikelezea kwa jinsi sasa serikali ilivyoboresha mitandao ya serikali kupitia MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO (eGA) ambapo moja ya maelezo ya mamlaka hii ni:-
e-GA inakusudia kutekeleza afua mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi. Utekelezaji huo utafanyika kwa kufanya yafuatayo:
Wadau wanaomsaidia Mh. Raisi nendeni kimya kimya muwapige tukio wahusika wawaoneshe mtandao unakwama wapi. Ninafahamu waathirika hapa ni wengi. Ngoja tuone.

Shughuli Muhimu
Huduma Mtandao
e-GA inakusudia kutekeleza afua mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi. Utekelezaji huo utafanyika kwa kufanya yafuatayo:
- Uongezaji na uboreshaji wa njia za utoaji wa huduma za serikali mtandao
- Utoaji wa huduma za ushauri na msaada wa kiufundi
- Uboreshaji wa uwezo wa rasilimaliwatu katika taasisi,
- Uwezeshaji wa upatikanaji wa miundombinu na mifumo salama na ya kuaminika ya Serikali mtandao
- Uimarishaji na uratibu wa jitihada za usalama wa kimtandao katika taasisi za umma.