Mkalukungone mwamba
Member
- Aug 29, 2022
- 24
- 39
Mkuu wa Programu JamiiForums, Ziada Seukindo amesema taasisi za serikali zinaruhusiwa kutumia mtandao wa JamiiForums kwa sababu ni Jukwaa la mtandao kama majukwaa ya mitandao ya kijamii mengine duniani.
“Taasisi za serikali zinapaswa kutambua JamiiForums ni mtandao wa ndani tuuthamini, baadhi hatutambui vitu vinavyoanzishwa na wataalamu wetu wa ndani sijajua kwa nini hatuna imani navyo na wakati huo huo tunakimbilia kutumia mtandao kama ‘TikTok’ wakati ‘TikTok’ yetu ya Tanzania ni Jamii Forum,” amesema Ziada.
Ziada amesema hayo wakati akiwasilisha mada ya mitandao ya Kijamii wakati wa mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) unaofanyika mkoani Mwanza.