Mtambo Mpya wa Ufuatiliaji Mawasiliano nchini (TTMS): Kwanini sasa? Nini kipya?

TCRA mnafanya vitu vya kiupuuzi sana,mnaendeshwa na wanasiasa,ni vizuri kiusalama kuweza kujua uhaini wa watu lakini si vyema kuweka Audio clips mlizorecord kuwa public,hizo clips mngemalizana nao kimya kimya na sio kuziweka hadharani.
 
Wakuu,

Nianze kwa kuwasalimia baada ya kimya cha muda mrefu na kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya 2019.

Twende kwenye hoja yangu:

Serikali ya Awamu ya 5 inaenda kuzindua "Mtambo Mpya" wa 'udhibiti' wa Mawasiliano maarufu kama "Telecommunications Traffic Monitoring System (TTMS)".

Kwa wengine watapongeza na wengine wataponda, mimi nina maswali kadhaa najiuliza na kukosa majibu.

Si kweli kuwa TCRA haikuwa na mtambo wa aina hii; upo na ulilalamikiwa kutumiwa visivyo kuingilia mawasiliano ya wananchi kinyume na sheria (Sheria Mama, yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005)

View attachment 997481

View attachment 997483

Aidha, ziliandikwa stories kibao miaka michache tu iliyopita kusifia mfumo huo 'mpya wa zamani'; unaweza kusoma:

Tanzania Deploys the First Mobile Money Monitoring Solution for Regulatory Authorities in the World - NextBillion
&
Inauguration of the Telecommunications Traffic Monitoring System in Tanzania

Huku tukiambiwa mfumo huu (mpya wa zamani) ni wa kipekee duniani na utaokoa mabilioni, wizi, utapeli n.k

Unaweza kusoma pia:

https://www.ippmedia.com/sw/habari/wizi-wa-kampuni-za-simu-kwa-wateja-mwisho
au
SERIKALI IMEKUSANYA BILIONI 63 KUPITIA MTAMBO WA KUHAKIKI NA KUSIMAMIA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI. ~ CCM Blog
au
Uzindua wa mitambo maalum ya usimamizi wa Mawasiliano & wa Kudhibiti Matukio ya Uhalifu wa mtandao - JamiiForums


Maswali yangu:

1) Je, mtambo huu tunaoambiwa unazinduliwa, una jipya gani?

2) Mtambo huu, umetugharimu kiasi gani? Pesa zimetoka wapi? Ni kodi zetu?

3) Ni jambo jema kuwa 'wa kwanza', lakini hatugeuzwi chambo?

4) Mtambo uliokuwepo ulikuwa na kasoro? Ni zipi? Gharama zilizotumika kwa mtambo 'tunaoachana nao' zilikuwaje?

5) Aliyetuuzia/tupatia mtambo wa awali - kulikuwa na mkataba naye? Unasemaje? Nini kimepelekea maamuzi ya 'kuupiga chini' mtambo wake? Mawasiliano yetu yalikuwa salama?

MASHAKA YANGU:

Tunapoelekea Uchaguzi Mkuu 2020, mtambo huu unaweza kutumiwa kufanya illegal communication surveillance na wanasiasa wakatumia visivyo taarifa watakazozipata tokana na wao kusikiliza simu za watu au kusoma taarifa binafsi za watu.
Tutajie na jina la alievunjika miguu. Kumbe wewe c wa mchezo mchezo
 
Ahah Haya Bhna Nabii wa Jf

Tutaanza kusikia tena flani katoweka hajarudi nyumbani tangia alipotoka nyumbani kwake mara flani ametekwa na hajapatikana tena.

They are about to deploy new and sophisticated method if eliminating those who will be talking against him.
 
Back
Top Bottom