Mtambo Mpya wa Ufuatiliaji Mawasiliano nchini (TTMS): Kwanini sasa? Nini kipya?

Ex Spy

Senior Member
Jan 15, 2007
184
1,000
Wakuu,

Nianze kwa kuwasalimia baada ya kimya cha muda mrefu na kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya 2019.

Twende kwenye hoja yangu:

Serikali ya Awamu ya 5 inaenda kuzindua "Mtambo Mpya" wa 'udhibiti' wa Mawasiliano maarufu kama "Telecommunications Traffic Monitoring System (TTMS)".

Kwa wengine watapongeza na wengine wataponda, mimi nina maswali kadhaa najiuliza na kukosa majibu.

Si kweli kuwa TCRA haikuwa na mtambo wa aina hii; upo na ulilalamikiwa kutumiwa visivyo kuingilia mawasiliano ya wananchi kinyume na sheria (Sheria Mama, yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005)

katiba-2005-UhuruMaoni.jpg


Tanzania-Constitution-Freedoms2005.png


Aidha, ziliandikwa stories kibao miaka michache tu iliyopita kusifia mfumo huo 'mpya wa zamani'; unaweza kusoma:

Tanzania Deploys the First Mobile Money Monitoring Solution for Regulatory Authorities in the World - NextBillion
&
Inauguration of the Telecommunications Traffic Monitoring System in Tanzania

Huku tukiambiwa mfumo huu (mpya wa zamani) ni wa kipekee duniani na utaokoa mabilioni, wizi, utapeli n.k

Unaweza kusoma pia:

https://www.ippmedia.com/sw/habari/wizi-wa-kampuni-za-simu-kwa-wateja-mwisho
au
SERIKALI IMEKUSANYA BILIONI 63 KUPITIA MTAMBO WA KUHAKIKI NA KUSIMAMIA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI. ~ CCM Blog
au
Uzindua wa mitambo maalum ya usimamizi wa Mawasiliano & wa Kudhibiti Matukio ya Uhalifu wa mtandao - JamiiForums


Maswali yangu:

1) Je, mtambo huu tunaoambiwa unazinduliwa, una jipya gani?

2) Mtambo huu, umetugharimu kiasi gani? Pesa zimetoka wapi? Ni kodi zetu?

3) Ni jambo jema kuwa 'wa kwanza', lakini hatugeuzwi chambo?

4) Mtambo uliokuwepo ulikuwa na kasoro? Ni zipi? Gharama zilizotumika kwa mtambo 'tunaoachana nao' zilikuwaje?

5) Aliyetuuzia/tupatia mtambo wa awali - kulikuwa na mkataba naye? Unasemaje? Nini kimepelekea maamuzi ya 'kuupiga chini' mtambo wake? Mawasiliano yetu yalikuwa salama?

MASHAKA YANGU:

Tunapoelekea Uchaguzi Mkuu 2020, mtambo huu unaweza kutumiwa kufanya illegal communication surveillance na wanasiasa wakatumia visivyo taarifa watakazozipata tokana na wao kusikiliza simu za watu au kusoma taarifa binafsi za watu.
 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,699
2,000
Kufatilia mawasiliano inamaanisha watasikiliza mazungumzo na kusoma sms zetu? Au huko kufatilia kukoje?
 

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
5,570
2,000
Kulikuwa na haja gani ya kununua mtambo mpya kama wa zamani unafanya kazi sawa na huu mpya?

Huyu jiwe anataka awe mfalme katika nchi ya kidemokrasia kwamba lolote atakalotaka litekelezwe na lifanyiwe kazi.

Tutaanza kusikia tena flani katoweka hajarudi nyumbani tangia alipotoka nyumbani kwake mara flani ametekwa na hajapatikana tena.

They are about to deploy new and sophisticated method if eliminating those who will be talking against him.
 

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,441
2,000
Kesho utasikia huu mtambo unatibu hadi panga boi zetu
Na pia utawasaidia warusha mwewe wetu waonane angani na kufanya overtaking maana tunazo mingi na zote zinapaa
Wote:makofi mengi
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
75,986
2,000

sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
3,280
2,000
Mbona vitu vya namna hiyo viko vingi tuu, kuanzia rada, mkonga wa internet( mara unapita ardhini na baharini) , umeme wa gesi nk, niambie ufanisi wake kwa sasa ukilinganisha na ilivokuwa ikitangazwa hapo awali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom