Niliwahi kuidukua simu ya ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua, Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia!

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,850
Uzi huu nimeuandaa baada ya kusoma post flani inatrend jukwaani muda huu kuna dada yetu anahisi mme wake anatumia ushirikina kujua mawasiliano yake ya watu anaoongea nao, Huenda ni kweli lakini kisa hiki kimenikumbusha mbali sana kwamba labda mme wake katumia mbinu niliyowahi kuitumia zamani kwa ex wangu kwa kumnunulia simu mpya ambayo niliidukua kisha kumzawadia. Enzi hizo ilikuwa rahisi sana kudukua simu ila kwa siku hizi sijajua, sijafatilia na wala sina hamu.

Ilikuwa ni miaka ya 2015 hivi, nilikuwa na girlfriend wangu ambae niliingia tamaa ya kutaka kumpeleleza zaidi, alikuwa ni kisu haswa.

mimi ni fundi seremala lakini mambo ya teknolojia napendaga sana kuyafatilia tangu zamani hivyo nilishawishika kumdukua simu yake.

Nilijaribu kudukua smartphone yake lakini ilikuwa na ulinzi imara kuzidi uwezo nilionao so ikabidi nizame mfukoni nikaenda kumnunulia simu used kali kimtindo ambayo nilishaifanyia uchunguzi naweza kuidukua.

Niliidukua kirahisi wala haikunipa shida, step ya kwanza ilibidi nipate access ya mafaili yote ya simu hata yale ya ulinzi ambayo hayaonekani, hapa nilifanya zoezi linaitwa "rooting" ili kudhoofisha ulinzi wa simu ifanye nachotaka. Baada ya hapo nikaweka sasa mtambo wangu ambao ni app, enzi hizo ulikuwa unaitwa android lost nikaongezea na vikorombwezo vya ziada.

Huo mtambo ni kwamba ukiuweka kwenye simu, unaweza kutumia laptop ama simu nyingine kuona meseji zote za simu uliyoidukua, call logs zote hata zikifutwa, unaweza kufungulia maiki mda wowote kunasa sauti, simu inaweza kupiga picha mda wowote uone mazingira, kucheki chats za whatsapp, n.k.

Nilijiona mjanja sana ila kilichotokea ni maumivu tu.

Kwa vile dem alikuwa ni pisi kali, zile meseji za hi sweety, hi mrembo, n.k. zilikuwa hazikauki hata iwe ni mtu waliezoeana kawaida tu, hizi mesej zilikuwa zinanifanya nijawe na wivu na hasira sana.

Wapo jamaa walikuwa ni ving'ang'anizi balaa, wanapiga saundi hadi nakosa amani, si mnajua tena huu ulimwengu wenye simu, hata asipotoa wataipata kwa marafiki. Nikwambie tu ya kwamba mwanamke kutongozwa ni jambo la kawaida sana.

Wivu wangu ulizaa hasira za kutaka kumlinda zaidi, hii ilisababisha kila muda niwe nafatilia sehemu anazokwenda kimya kimya akitoka nje ya chuo, mtambo ulikuwa na uwezo kuonyesha alipo na ruti zake na mda aliokaa hio sehemu, hata hivyo alikuwa ni mtu wa kukaa sana chuoni ila akitoka kwenda sehemu ambayo si gheto kwangu niliingia wivu wa kwenda kupachunguza.

Kelele na ugomvi vilianza pindi nilipooana kuna chats za ex wake ama kuna sehemu kaenda ambayo nina mashaka nayo, sikumwambia nimedukua simu yake ila nilikuwa namwambia kuna watu wameniambia, Nilikuwa na wivu uliopitiliza.

Siku niliyochapiwa !!

Ni siku ambayo walimaliza mitihani yao ya muhula, kuna jamaa nahisi ni class mate wake walienda nae geto kwake, siku hio hata simu yake ilikuwa haipatikani, sasa kesho yake asubuhi ndio kawasha simu, kwenye mtambo naona jamaa anamtumia mesej, vp umerudi salama chuoni, leo uje tena, n.k. jamaa akahamia kuanza kuzungumzia yaliyotokea jana yake, akaanza kuzungumzia mnyanduano wa jana yake, anaomba irudiwe sometimes kwa kiingereza mfano "babe am horny i need a few more pumps to fix the situation", wajaribu style mpya, ex nae anamtania alipiga kimoja basi nae jamaa anajitetea mitihani ilimchosha ana nguvu mpya kumpiga vitatu, n.k. iliniuma sana jamani, kidume hadi machozi yalikuwa yananilenga lenga. Mda wote huo moja kwa moja mawazo yananijia kwamba jamaa kanizidi ufundi na huenda ana mkuyenge mkubwa kunizidi, aish! Dah! Sio poa jamani nyie sikieni tu yani niliumia sana yani.

Huwezi amini nilijifanya sijui chochote, nikampigia simu ex aje, ex alivyo mshenzi ndio kwanza aliniletea zawadi ya t-shirt na akawa anazuga jana simu yake ilikuwa na matatizo flani. (nimeyasahau ).

Nikamkalisha kitako na kumwambia jana umenichiti na nikamwambia nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa hapo chuoni kwao kanipa A - Z wa usaliti ulionifanyia, nilimtajia hadi jina la huyo jamaa waliekuwa nae jana, alipiga magoti na kulia sana na kuomba msamaha akaanza visingizio sijui shetani kampitia machozi kama yote analia, nadhani wengi mnajua kipaji walichonacho wanawake kwenye kulia, Kwa upande wangu nilikuwa nimeumia sana kwamba kuna jamaa kamcharaza mkwaju, Very painful na hasira kwa juu.

Nilimtolea uvivu kuna vinguo nguo na kibegi alikuwa nacho hapo gheto vya siku akija kwangu nikavifungasha ovyo ovyo nikamrushia hicho kibegi aondoke mara moja, alikuwa mbishi nami hasira zimenipanda nilimtandika vibao vya nguvu sana kama vitatu hivi timua nje kabisa nikafunga mlango, uzuri hio siku nilikuwa peke yangu hakuna wapangaji wengine.

Nilikuwa nafatilia mesej zake kwa wiki hivi huku nikiwa na maumivu, alikuwa anapiga sana simu ikabidi namba yake niliblok asinipigie, hivyo alikuwa anatumia simu za rafiki zake ila nikigundua sauti yake nakata, kwenye mtambo naona alikuwa anapitia kipindi kigumu alikuwa anachat na marafiki zake juu ya break up, kuomba ushauri, wanamliwaza, n k. kiukweli niliona kajutia nami nilihisi pengine kweli kashetani kalimpitia ila maumivu niliyokuwa nayapata kila nikiwaza alivyonisaliti ni kama kisu kikali kimegonga mfupa, yule jamaa aliemtafuna jana nilikuwa naona kafura analalamika dem hajibu text wala kupokea simu bila kujua msala uliotokea huku, mda ulienda niliacha hata kumfatilia nikafuta huo mtambo maana ulikuwa unanifanya nimuwaze badala ya ku move on.

that was the end.
 
Uzi huu nimeuandaa baada ya kusoma post flani inatrend jukwaani muda huu kuna dada yetu anahisi mme wake anatumia ushirikina kujua mawasiliano yake ya watu anaoongea nao, Huenda ni kweli lakini kisa hiki kimenikumbusha mbali sana kwamba labda mm wake katumia mbinu niliyowahi kuitumia zamani kwa ex wangu kwa kuidukua simu yake nijue kila mahali alipo, mawasiliano yake, n.k.

Ilikuwa ni miaka ya 2015 hivi, nilikuwa na girlfriend wangu ambae niliingia tamaa ya kutaka kumpeleleza zaidi, alikuwa i kisu haswa na nikawa na insecurity ya kutaka kumfatilia zaidi.

Nikiri tu mimi ni fundi seremala lakini mambo ya tknolojia napendaga sana kuyafatilia.

Girlfriend wangu alikuwa ni mwana chuo ana kismartphone chake nilitaka nikidukue lakini kilikuwa na ulinzi imara kuzidi uwezo nilionao japo kuna watabe wanaeza kukifyatua.

Nilizama mfukoni nikaenda kumnunulia simu used kali kimtindo pamoja na risiti yake na mkataba wa pande mbili kwa mwanasheria (nilichajiwa elf 20).

Kwa kuwa nilishafanya research yangu simu hio wala haikunishinda kuidukua, Niling'oa kisiki cha mafaili (rooting) kisha nikaweka mtambo wangu amba enzi hizo ulikuwa unaitwa android lost na vitu vya ziada.

Huo mtambo unaweza kusikia sauti kwa kuifungua maiki mda wowote unaotaka, kujua ruti za mtu kwa kufatilia location, simu inaweza kupiga picha ma wowote bila mwenye simu kujua, mesej zote zinasomeka, call logs zote zinarekodiwa, screen shoots zote unapata, n.k.

Nilijiona mjanja sana ila kilichotokea ni maumivu tu.


Kwa vile dem alikuwa ni pisi kali, zile meseji za hi sweety, hi mrembo, n.k. zilikuwa hazikauki hata iwe ni mtu waliezoeana kawaida, hizi mesej zilikuwa zinawasha moto wa kifuu cha nazi kwenye mfumo wangu wa neva, kila mtu anaetuma meseji hizi nilichukulia dem wangu ananichiti.

Mesej za ma ex wake wengine walikuwa wanakumbushia nyakati walizopitia ikiwemo kwenye minyanduo, vitu vilikuwa vinanipa chuki na hasira sana hivi.

Kelele na ugomvi vilianza kuwa kawaida, sikumwambia nimedukuasimu yake ila nilikuwa namwambia kuna watu wameniambia, Nilikuwa na wivu uliopitiliza.

Siku niliyochapiwa !!

Ni siku ambayo walimaliza mitihani yao ya muhula, kuna jamaa nahisi ni ex wake walienda nae geto kwake, siku hio hata simu yake ilikuwa haipatikani, sasa kesho yake asubuhi ndio nimefungua mtambo naona jamaa natuma mesej, vp umefika salama, leo uje tena, naendela kufatilia ndio jamaa akaanza kuzungumzia mnyanduano wa jana yake na anaomba warudie tena, iliniuma sana !!. Huwezi amini nilijifanya sijui chchote ila yule dem ndio kwanza aliniletea zawadi ya t-shirt na akawa anazuga jana simu yake ilikuwa na matatizo flani. (nimesahau ).

Nikamkalisha kitako na kumwambia jana umenichiti na nikaanza kumchorea picha kuendana na huyo jamaa aliemkamua jana, alipiga magoti na kulia sana na kuomba msamaha sijui shetani kampitia machozi kama yote!! nadhani wengi mnajua kipaji walichonacho wanawake kwenye kulia, Kwa upande wangu nilikuwa nimeumia sana kwamba kuna jamaa kamcharaza mkwaju, Very painful.

Nilimtolea uvivu kuna vinguo nguo na kibegi alikuwa nacho hapo gheto vya siku akija kulala kwangu nikavifungasha ovyo ovyo nikamrushia hicho kibegi aondoke mara moja, alikuwa mbishi nami hasira zimenipanda nilimtandika vibao kama vitatu hivi timua nje kabisa nikafunga mlango, uzuri hio siku nilikuwa peke yangu hakuna wapangaji wengine.

Nilikuwa nafatilia mesej zake kwa wiki kama mbili alikuwa anachat na marafiki zake juu ya break up nami nilihisi pengine kweli kashetani kalimpitia ila ndio hivyo tena, kila nikikumbuka kuna jamaa kafukua hasira zinanijia fasta nashindwa kabisa kusamehe.
Inachekesh🤣🤣🤣
 
Kuweka kidukuzi kufuatilia mawasiliano ya simu kwa mpenzi wako,,unayempenda sana,,
kunataka uwe na roho ngumu haswa,,
Vinginevyo utakuja kuaibika mwishoni.

Kuna rafiki yangu fulani alikuwa na msichana wake ,,
ambaye alikuwa anampenda sn ,,
hata kwa kuangalia mapenzi yao kwa macho tu,
jamaa alikufa na kuoza kwa yule msichana mwanachuo..
jamaa alimpenda Sana yule demu..

Baada ya jamaa kupigwa sn matukio na yule demu Kwa muda mrefu,,
Akaamua adukuwe mawasiliano ya mchumba wake,,
Basi sms pamoja na calls zote msichana akipigiwa na jamaa nae anazipata tena bila msichana wake kujuwa.

Siku Moja msichana akaaga atatoka kwenda chuo,,
Jamaa akamruhusu atoke lakini awahi kurudi,,
Yote hayo jamaa ni ktk kutaka kujikaza kiume,,
Lakini alikuwa anajuwa kila kitu demu wake anakwenda kwa msela kupigwa mbupu,,
Lengo lake ni kutaka kumkamata Kwa ushahidi akiwa na yule msela.

Demu kaita bodaboda,,,jamaa kuona bodaboda imefika,,,demu wake yupo juu ya bodaboda,,
Jamaa uzalendo ukamshinda akazuia bodaboda isiondoke.
Jamaa akaanza kupaza sauti Kwa kelele hata kujaza mtaa mzima,,
"Najuwa Kila kitu kwamba unakwenda kwa jamaa.."
Jamaa akaanza kulia kabisa mbele ya demu ,
"Nini umekosa kwangu"

Ikawa vurugu tupu...
Huwezi amini pamoja na matukio yote hayo,,Bado jamaa amemuoa hyo demu na ana watoto nae 2 tayari.
Ila amejiapiza kutodukuwa tena simu ya mkewe,,
Japokuwa bado hamuamini.
 
Hii michezo ilinifanya kumkamata demu akiingiza njemba geto kwangu kwa kuzuga kuwa dadaake anakuja kumtembelea na atapenda afikie geto kwake. Tulikuwa tunaishi pamoja kiunyumba kama kawaida ya mchezo wa wanachuo ili kujihakikishia all time supply ya utelezi.

Nikaona nimpe chance alale na ndugu yake, kufuatilia convo kwenye tambo kumbe kuna njemba ilikuwa inaandaliwa shoo! Nlichokifanya nikawahi eneo la tukio nikabana chocho nikishuhudia chezo lote hadi njemba inaingizwa geto. Baada ya njemba kuingia tu nkavuta pumzi nkaenda kushika kitasa mara demu anafungua haamini kama ni mimi ndio nmemfumania.

Jamaa alikuwa ndo anaandaliwa maji ya kuoga chumba knanukia maua rose balaa, sitakaa nisahau ile siku. Bila demu kukimbia leo ningekuwa selo nanyea debe.
 
Hii michezo ilinifanya kumkamata demu akiingiza njemba geto kwangu kwa kuzuga kuwa dadaake anakuja kumtembelea na atapenda afikie geto kwake. Tulikuwa tunaishi pamoja kiunyumba kama kawaida ya mchezo wa wanachuo ili kujihakikishia all time supply ya utelezi.

Nikaona nimpe chance alale na ndugu yake, kufuatilia convo kwenye tambo kumbe kuna njemba ilikuwa inaandaliwa shoo! Nlichokifanya nikawahi eneo la tukio nikabana chocho nikishuhudia chezo lote hadi njemba inaingizwa geto. Baada ya njemba kuingia tu nkavuta pumzi nkaenda kushika kitasa mara demu anafungua haamini kama ni mimi ndio nmemfumania.

Jamaa alikuwa ndo anaandaliwa maji ya kuoga chumba knanukia maua rose balaa, sitakaa nisahau ile siku. Bila demu kukimbia leo ningekuwa selo nanyea debe.
Ahahhaahah duh hatari
 
Back
Top Bottom