Fahamu yaliyomo katika Ripoti Kuu ya Ukaguzi ya Mifumo ya TEHAMA 2021/22

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1. Kutokuwepo kwa Ufuatiliaji wa miamala ya simu za mkononi isiyofanikiwa
Niligundua kuwa ufuatiliaji wa miamala ya simu za mkononi isiyofanikiwa haufanywi katika mfumo wa TTMS. Nilielezwa kuwa muundo wa TTMS haukuzingatia miamala hi sababu haipaswi kuwa na ada zaidi ya gharama za mtandao zinazohusiana na matumizi ya njia za USSD

Walakini, TCRA imepewa jukumu la kufuatilia na kutoa uhakikisho wa mapato kwa huduma za mawasiliano kulingana na Kifungu cha 4 - (2) (i) na 4 - (2) (j) cha Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Tele-Traffic), 2021. Hii ni pamoja na ada zote zinazotozwa na gharama za wandeshaji kwa madhumuni ya uhakiki wa kodi na uwazi wa serikali

Ninapendekeza TCRA kuimarisha mfumo wa TTMS ili kujumuisha ufuatiliaji miamala isiyofanikiwa "Rollback Transactions"

2. Kukosekana kwa mikataba na makubaliano ya viwango vya huduma na watoa huduma za TEHAMA
Ukaguzi wa usimamizi watoa huduma za TEHAMA umebaini kwamba taasisi nyingi za serikali nchini Tanzania hazina mikataba na makubaliano ya viwango vya huduma na watoa huduma wao wa TEHAMA

Kukosekana kwa mikataba na makubaliano na watoa huduma za TEHAMA kunaweza kusababisha hatari kwa taasisi za serikali, ikiwamo kukatika kwa huduma, uvujaji wa data, na kuwa tegemezi kwa mtoa huduma

3. Mashine za POS TEMESA
Niligundua mashine za POS zinazotumika katika vituo vya kukusanya mapato vya TEMESA hazikuwa zimeunganishwa kwenye mtambo mkuu wawa kuhifadhi data (Server). kwahiyo mashine ikiharibika, taarifa za mapato hupotea na haziwezi kufuatiliwa. Hii inaweza kusababisha uwezekano wa upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya vifaa hivyo.

4. Msaada duni wa huduma kwa wateja
Mapitio yangu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) umebainisha masuala mawili muhimu ambayo yanahitaji kuangaliwa kwa umakini: Msaada usioridhisha wa huduma kwa wateja, pamoja na ufuatiliaji usioridhisha wa uridhishwaji wa wateja kwenye huduma wanazopewa na mamlaka.

Kulikuwa na matukio 216 ambapo mamlaka ilichukua zaidi ya siku 30 kufanyia kazi malalamiko ya wateja. Hii ni kinyume na Mkataba wa Huduma kwa Mteja unaoitaka mamlaka kutatua malalamiko ya wateja kati ya saa 72 hadi siku 30. Ucheleweshaji huo wa kutatua malalamiko ya wateja unaweza kusababisha taasisi za umma kuchelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

5. Mifumo ya RITA
RITA ina mifumo minne tofauti ya maombi ya usajili wa vizazi na vifo. Nayo ni: Mfumo wa Usajili wa Kiraia (CRS), mfumo wa usajili wa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, mfumo wa usimamizi wa taarifa za usajili wa raia (CRIMS), na mfumo wa usajili wa mtandaoni. Urudufu huu wa mifumo huongeza gharama za usimamizi, matengenezo, na usaidizi na uendeshaji.

Ninapendekeza kwamba Menejimenti ya RITA iandae usanifu wa kiutendaji ili kuwianisha mifumo ya TEHAMA, na kuhakikisha matumizi ya mfumo mmoja wa usajili wa Kuzaliwa na Vifo nchini kote.Pia, iandae mpango wa uhamishaji taarifa unaofaa kutoka kwa mifumo mingine Kwenda kwenye mfumo uliyochaguliwa.

6. Kukosekana kwa Udhibiti wa Utumiaji wa Mifumo kwa Watoa Huduma za TEHAMA
Katika ukaguzi wangu wa TTCL-PESA na TASAC, niligundua kuwa wazabuni wa mifumo hawana kikomo cha matumizi kwenye kanzidata pamoja na mtandao wa taasisi

Kutokuwapo kwa udhibiti wa wazabuni katika mifumo kunaweza kusababisha taarifa kunakiliwa, kusambazwa, na kutumika isivyo na wazabuni au wafanyakazi wake

Napendekeza TTCL na TASAC kuwaondolea wazabuni haki za kuingia kwenye mifumo na kuwapa pale tu panapohitajika ili kuhakikisha usalama kwenye mifumo.
 

Attachments

  • Tehama.pdf
    9.1 MB · Views: 10
Back
Top Bottom