Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Habarini za asubuhi ndugu wadau wa JF.
Samahanini sana wengine ndio kwanza kwa mara ya kwanza tunaingia kwenye upande huu wa Biashara.
Nianze kwa kusema mimi Nina kiasi cha TSh 2 Mil. Nimejikusanya na kuhakikisha nimezipata japo kwakuvuja jasho. Toka week iliyopita nimekuwa nikijaribu kuwaza nini chakufanya na pesa hii ili isije ikayayuka kutokana na ukata uliopo nikawaza niifanyie kazi ili izunguke na kuongezeka. Mpka sasa sijajua nini chakufanya ili hii pesa izunguke kama kufanya biashara izae na si kupungu.

Dhima ya kuja hapa ni kutaka kupata wazo la biashara yoyote kutoka kwenu wadau wazuri wa biashara ,niko hapa ndugu yenu nitasikiliza ushauri wa yeyote yule na bila kuupuuzia na niko tayati kusikiliza .karibuni.
 
Wapendwa katika pilikapilika zangu za mtaa, mpaka sasa Nimejaaliwa na kiasi cha Tsh 1 0000 000/= Milioni 1. Ushauri wenu utakuwa muhimu sana kwangu, kwani naamini humu kuna wazoefu wengi wa Biashara. Sihitaji kukurupuka. Maoni yenu biashara gani itafaa kwa Mtaji huo?? Nipo Arusha.
Tuanze na hobby yako
Je?kuna wazo lolote La biashara ulikuwa nalo,kipindi unaweka hizo pesa

Kama lipo fanyia kazi,pia muhimu kujua ni biashara gani unazipendelea unaweza kuziorodhesha then wenye ushauri na ujuzi wa biashara hizo watakushauri kutokana na uzoefu

Mtu hawezi kukushauri tu,bila kujua unapenda nn ili ushauri usiwe nje ya mipango yako.
 
Niliamua kutafuta mtaji kwa udi na uvumba mpaka nikazifuata hela mikoa ya nyanda za juu kusini mtoto wa kike. Sasa nimerudi jijini nikiwa na mtaji kidogo tu ambao kichwa kinaniwaka sijui nifanyie biashara ipi kati ya hizi

1. Nifungue grocery ya kisasa
2. Nifungue mgahawa
3. Nifungue saloon ya kike
4. Nifungue duka la nguo za mitumba
5. Nifungue genge la kisasa

Mtaji wangu ni zaidi ya mil 5.
Naomba mawazo yenu wajasiriamali mliotutangulia. Nahitaji na mchanganuo kama itawezekana maana nahitaji na nipo tayari kujisimamia

Karibuni sana
ulifanikiwa my dear
 
mjini utapata wateja gan .... labda uuze mahindi ya makande
Mkuu unajua miji mingapi?Mie nimeongelea "mijini" wewe unaongelea "mji" labda unaangalia mji mmoja ambao wewe una uzoefu nao. Mfano mie najua mwanamama ambaye anafanya hii kazi na anapiga hela za kutosha.
 
wadau wenzangu, mimi mwanafunzi wa chuo kikuu anyetarajia kuhitimu mwakani, kwa katika biashara zangu ndogondogo in the past four years nimefanikisha kusave milioni 4. kwahiyo hapa naomba ushauri wenu niaze bishara gani ambao ni nzuri na itaniiletea faida. mimi mara nyingi huwa nafikiria sana kuanza biashara ya bodaboda/ au kununua bajaji second hand. so now ningependa munipe ushauri wenu je ni biashara gani inanifaa kulingana na mtaji wangu. thank you
 
Habari wapendwa. Naomba kuuliza ni fursa zipi au biashara zipi naweza kufanya kwa mtaji wa Million 1. Nimemaliza chuo mwaka huu, hali ni ngumu mtaani, nimepata mkopo wa Million 1 kama kianzio cha biashara. Natanguliza shukurani.
 
Back
Top Bottom