Tatizo wabongo tunafanya informal Business kiasi kwamba mkizuruminana hakuna pa kwenda kulilia, INATAKIWA MUWE NA CONTACT NA MNASAINI MU Memorundum of Understanding, theni mnapiga kazi
Kimsingi kila mtu anakubaliwa kuwasiliana na wenzake , kama katiba inavyuoelekeza, lakini si kila maoni ni busara , inayotokana na hekima, kwa sababu, hekima ni kipawa kinachotukuka kutokana na uzoefu.Nachelea kusema hivi, si vyema kupotosha , au kujaribu kuonyesha hisia bila ukweli kama ifutavyo:
1.ELIMU KAMA MSINGI WA UJUZI
Ikumbukwe huyu mdau tayari kesha sema anao mtaji wa 1 mil , kuanzisha na kuendesha biashara.Kwahiyo, ni vyema akanzisha biashara inayoendana na upeo wake wa ufahamu , ili kusudi asiingie gharama nyingine ya kununua ujuzi huo kutoka kwa mtu mwingine.Mtaji ni wa kiasi hicho, hivyo kuanzisha biashara ambayo inahitaji ujuzi na utaalamu mkubwa , maanake aukodi au kuununua , hiyo fedha itatoka wapi?ni vyema kuzingatia upeo wa ufahamu ili fedha ya mtaji usitoshe na kumudu vyema kusimamia.Uzoefu, ni kwamba, imekuwa ni vyema mjasiariamali awe mwenye upeo sitahiki na ujuzi wa kuendesha biashara au shughuli yake ya kiuchumi, anao uwezo mzuri wa kusimamia na kuzimudu changamoro za kiuendeshaji kirahisi.Hivyo, kuanzisha biashara kwenye upeo mwafaka, ni chanzo kizuri cha kisimamia ipasavyo.Hivyo kufahamu kiwango cha elimu katika kuanzisha biashara ni jambo la msingi mno.Kwa msitakabari huu, kwa kuwa mtaji ni wa kawaida hata biashara ambayo itapendekezwa , inatakiwa iwe inafanana na upeo huo.
2,RISK
Kimsingi kuna risks ambazo ni unpredictable, lakini huyu mdau yeye kaomba ushauri wa kuanzisha biashara. maanake, pembe zote mwafaka na sitahiki za kuanzisha, kuendesha kuthamini zinatakiwa zichambuliwe kiusahihi, ili kulinda mtaji usipotee kirahisi kwa sababu vigezo fulani vya risk mgt havikuzingatiwa.Mfano, kuanzisha biashara bila kuchambua soko , huku ukitegemea kupata soko circmsitancially, huo, itakuwa upofu.Ni vyema kuzingatia kuwa soko linashikika, lipo kwa kiasi kukubwa na pana , lisilobadilikabadilika.Ni jambo la msingi mno.Au kufanya biashara ambazo purely ni risk involved , for sake zinalipa, huo ni upofu pia.ikumbukwe huyu mdau ndo fedha pekee , inatakiwa kulindwa kama mboni hivyo kuingia kufanya biashara bila kupima na kutathimi ipasavyo, ni kumtakia msongo.
3.UMRI
Ni muhimu kwa biashara ya mtaji wa namna hiyo .Kuna aina za biashara ambazo umri si jambo la msingi hasa kama mtaji ni mkubwa unaozingatia economies of scale kwa kuweka stable equlibrium of investment/firm, umri si kigezo.hapa umri ni muhimu.sababu huwezi kuanzisha biashara ya kuuza kahawa kwa mzee wa miaka 60, atawezaje kuzunguka mabarabarani?ni vyema umri ukafahamika ili kusudi kupanga biashara katika umri huo, muda huo, na mtaji tajwa ambao ndo concerpt.
4.KUSAFIRI
Mtaji tunaozungumza, ndo unaoazisha biashara.Hivyo kimsingi bado haujakuwa mkubwa kimanagement, hakuna uzoefu, bado changamoto hazijajulikana, ni vyema mjasiriamali huyo kuwa karibu na mtaji akisimamia, hivyo kama kuna biashara kwenye mtaji huo ni wazi unakuwa unazunguka hapa nchini, ni lazima aambatane nao kufuatilia kupata uzoefu, kujua changamoto zake, kuliko kama itakuawa biashara ya kusafiri yeye anaaigiza tu;mfano wamletee mchele wa kyela , yeye kalala, hapo mtaji atakuwa ameuuza.Kwahiyo kunafursa za kibiashra za kusafiri, zikipatikana, vyema akawa pamoja karibu na mtaji wake.Kuna gharama ambazo kama angekuwa karibu angeweza kuzipunguza, kuzikataa,lakini akiwa mbali ni lazima zitaongezeka hao anaowatuma nao watajipa kamshahara .
5.MZUNGUKO
Siku zote mtaji mzuri ni ule unaozunguka haraka, kuleta mafao mapema, kuliko unaozunguka taratibu kwa muda mrefu.Mtaji tunaozungumzia hapa ni 1mil, hivyo vyema kukawa na biashara ya mzunguko wa haraka, kumtia hamasa ya kuzungusha mapema zaidi kuliko biashara za mzunguko mrefu.Ikumbukwe dunia imezungukwa na mambo mengi, kama mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kisosholojia, nk.Hivyo kuchagua biashara ya mzunguko mrefu, ni risk , sababu kukitokea mabadliko unakumbwa na mafuliko.
napenda kuwasihi sote ni wadau, si vyema kutoa uzoefu wa kupotosha sababu tupo kwenye mtadao, tuelimishane, ili tufanikiwe.