Mtafutaji hachoki akichoka basi kapata. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtafutaji hachoki akichoka basi kapata.

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by king kigama, Feb 17, 2017.

 1. king kigama

  king kigama Member

  #1
  Feb 17, 2017
  Joined: May 11, 2015
  Messages: 65
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 25
  Ni mara nyingi sana najitokeza hapa JF kutafuta nafasi za kazi.

  Mimi ni kijana mtanzania ambae siku zote nilikuwa na maono ya kuwa mtangazaji mkubwa ila maono hayo yamekuwa hafifu kwa vile kila nigusapo kutafuta ajira pamekuwa pakinitoa machozi (napata kazi ila malipo hakuna)
  ,Na kwa maisha ya sasa nimekuwa nikihaha kila kona bila ya mafanikio kwani kila sehemu nikienda wanataka nianze kazi kwa kujitolea ,kwa kweli hali hii inaumiza sana moyo wangu kwani huu ni mwaka wa tatu nimefanya kazi kama mtu wa kujitolea ila hakuna malipo nipatayo.

  Nimeangalia muda niliowekeza kupata nafasi ya kazi pamoja na masomo yangu kiukweli ni miaka mingi sana ila hali iko vile vile, najua mambo mazuri hatahitaji haraka ila kwangu mimi nahitaji kusukumwa ili niende haraka maana majukumu yanazidi kunivaa kila kuchapo.

  Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nimejitokeza hapa kuomba kazi yeyote ambayo itanipa kipato (kazi ya halali) nimechukua maamuzi haya kwani nashindwa sasa nifanye nini maana kila sehemu ugusapo wanasema jitolee na miaka mitatu imekatika nikiwa mtu wa kujitolea.

  Kwa sasa nipo arusha kwa yeyote mwenye sehemu ambayo anaweza kuniajiri naomba anisaidie natanguliza shukrani kwa yeyoye yule.

  Kejeli pia ni sehemu ya mchango nipo tayari kuzipokea.
   
 2. Sir_Mimi

  Sir_Mimi JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2017
  Joined: Jun 21, 2013
  Messages: 3,616
  Likes Received: 4,187
  Trophy Points: 280
  Pole sana bro....Mungu akugeuzie uso wake ukapate hitaji la moyo wako.ngoja wadau waje watakusaidia,nchi ngumu sana hii utadhani raia tupo kwenye “world war III".
   
 3. king kigama

  king kigama Member

  #3
  Feb 17, 2017
  Joined: May 11, 2015
  Messages: 65
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 25
  Shukran sana kwa mchango wako
   
 4. Blessed wild

  Blessed wild Member

  #4
  Feb 18, 2017
  Joined: Feb 16, 2017
  Messages: 18
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  aisee ajira nowdays ni ngumu ila mtafuta hachoki ni kuomba mungu
   
Loading...