Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

Huo ina maana utqkuwq unagonga mademu mpaka basi
 
Watoto wa Kishua bhana...

Sie wengine tumehama hizo pande kwa sababu tushakuwa watu wazima na tunahitaji kujitegemea na kuwa mbali na wazazi or else, unahama vipi pande hizo?!

Tatizo la huku, ukiishi jirani na familia... mtaa mzima unakuta pale mjomba, pale shangazi; mtaa wa pili ma' mdogo... yaani inakuwa taabu tupu! Na kama umeshaenda kuwa brainwashed na elimu ya kikoloni ndo full udhia!

Ndo kuna mtoto mmoja hivi wa Magomeni.. enzi hizo alikuwa mshikaji sana! Siku akanipigia simu kuniuliza Kwa Kindande ndo wapi, nikamwambia ndo pande hizi ninazoishi; we niambie unaenda Kwa Kindande kwa nani au sehemu gani manake kwa Kindande ni kubwa!

Akanitajia mitaa danger zaidi!

Siku ya siku mshikaji akaja home, na kwa roho safi, nikampeleka hadi kwa ndugu yake ambako kulikuwa na harusi! Kwa bahati mbaya, nilikuwa na mishe zangu kwahiyo nikamwacha, nikasepa!

Nusu saa nyingi, jamaa namuona huyu hapa wakati aliahidi angerudi baadae sana! Namuuliza hoya vp, mbona mapema! Jamaa nasikia "argh, washikaji wa kule sijui vp, kila muda naona wananiangalia kwa kukonyezana huku wakiambiana kwa sauti ya chini ng'ombe hilo... ng'ombe hilo!"

Bila kutarajia, nikajikuta namwangalia dressing code yake, nikaishia kucheka tu!!

Kwa Kindande sio Uswahilini bali ni Ushenzini... unaendaje Ushenzini na masuruali yako ya kitambaa huku ukiwa umechomokea na shati lako la mikono mirefu?!
 
Ukifika Temeke kuna mtaa unaitwa Mji mpya ndani yake kuna kamtaa korofi kanaitwa KINDANDE.

Kindande kuna maskani maarufu inaitwa Lebanon.

Huu mtaa kwa kindande ni mtaa ambao unaogopeka kupita bila taadhari kwa saa 24..Mambo yote maovu yapo hapo kuanzia wizi kukaba mchana umalaya uvutaji bangi ulio kubuhu.

Katika maisha yangu yote sijawai kuona wanawake wanavuta bangi kupita wanaume ni mewaona kwa Kindande.

Mabinti wa kwa Kindande wanatabia ya kukaa nje wakikuomba hela ukakataa kutoa hayo matusi yake ni balaaha.

Mabinti wa kwa Kindande wanaongoza kucheza vigodoro wakiwa uchi sometimes wanakodishwa kwenda kusasambua kwenye vigodoro vya majirani zao Mtongani,Tandika,Wailes, na Mbagala.

Hawa mabinti wana tabia ya kukodi boda boda usiku mishale ya saa 7 usiku na kuendelea wana tegesha sehemu za starehe ukijiroga ukampakia mkifika tu kwa Kindande kuna makaburi mitaa hiyo litakuja kundi litakupiga piki piki inaondoka.

Kwa Kindande ukimpenda demu ukichepuka kazi unayo utapigwa na kundi lake plus matusi juu hila yeye kuchepuka ruksa.

Wana maskani yao inaitwa Lebanon hiyo na polisi ni kufukuzana kila siku hapo unawapata madogo wa miaka 12 waliopinda wapiga bangi hatari.

Huku unakuta dogo naye ni baba vibinti vidogo navyo ni single mother.

Huu mtaa unaongoza kwa matusi kwa lika zote hakuna heshima kwa mkubwa wala mdogo.

Hiki kimtaa kimepakana na Tandika Kwa Aziz Ally Temeke mwisho na Mtoni mtongani.

Kama sio mtu wa vulugu usipange mtaa huu...
c kweli hayo mambo zamani sana ila sasa hv yamepungua sana kiukweli miaka ya 2003 to 2014 palikua hapafai ila nowdays yamepungua Sanaa yapo ila kwa uchache sana. temeke wailes ,mtongani ,mitaa ya kombora,kwa aziz ali ,kwa kabuma ,kitomondo,dabo kibini.
 
c kweli hayo mambo zamani sana ila sasa hv yamepungua sana kiukweli miaka ya 2003 to 2014 palikua hapafai ila nowdays yamepungua Sanaa yapo ila kwa uchache sana. temeke wailes ,mtongani ,mitaa ya kombora,kwa aziz ali ,kwa kabuma ,kitomondo,dabo kibini.
Yah, upo sahihi kwa 100%! Enzi kwa Kindande pako moto hata kwa Azizi Ally pale kituoni kupita usiku ni hadi uwe mwenyeji... enzi Kilwa Rd ni barabara moja iliyojaa mashimo kibao, na kituoni kwa Azizi Ally full vibanda!! Ile Madafu yenyewe ilikuwa full utata! Ukienda Sifa, kwa Kabuma, Relini taabu tupu. Temeke Mwisho yenyewe unaibiwa mchana ng'ombe anakula majani..

Hapo hujagusa kwa Kindande yenyewe hadi Tandika bila kusahau Mikoroshini!

Ikipigwa Fiesta au mechi za usiku pale taifa, inakuwa sikukuu kwa Masela wa Wailes!!

Lakini kote huko, hivi sasa kupo cool sana!
 
Mwaka 88 baada ya kupata kazi idara moja ya serikali nilipata chumba maeneo ya Manzese Midizini, wezi wote wa kwenye mitumba walikua wanakaa midizini. Nilikua nikirudi saa kumi sitoki ndani mpaka kesho yake kwa kuogopa vibaka. Siku moja kaja dogo mmoja kuniambia, shoferi usipende kukaa ndani kama dem. Njoo nikuyembeze. Basi nikatoka nae break ya kwanza kwenye banda la gongo. Enzi zile kituo cha polisi cha karibu ni urafiki. Basi nikaagiza kijeti kilipoisha nikaagiza cha pili. Wahuni walikunywa mpaka wakasema shoferi basi. Kuanzia hapo niliyembea Manzese yote mida yoyote bila kuulizwa na mtu. Ila wakikuomba kistaarabu kifanta au fegi wape tu. Nikaja kugundua kwamba kumbe hakuna mhuni ambae hana utu.
"Hakuna Muhuni Ambae Hana Utu"
 
Tatizo ukiishi uswailini kuna life flani apeche sana unalisoma. Japo na yote hayo izo amsha amsha ndo zinanifanya nashindwa kuhama uswailini, yani kama angekua mwanamke basi mngesema nimepewa limbwata
 
Back
Top Bottom