Wewe ndo wala huijui Dar es salaam!!! Kama unadhani Mikocheni, Masaki, Mbezi, Oysterbay and the like ndio Dar es salaama basi huijui Dar es salaam!!!
Huwezi kuitenganisha Dar es salaam na Uswahilini Max au Uswahilini Pro ambako nakuita Ushenzini!!!
Huko Ushenzini ndo unapata flavor halisi ya Dar, na sio kule ambako videmu na vivulana vinaongea Kiswahili kwa lafudhi ya kizungu wakati hata Nairobi hawajawahi kufika... fvck them all!!
Huwezi kusema upo Dar es salaam au umewahi kufika Dar es salaam wakati huijui Dar es salaam Asili!
Hujawahi kuuona wala kuusikia mdundiko, vigodoro unapata kuvisikia tu Instagram, hujawahi ona mwanamama mtu mzima anaendewa na vigoma kwake kusutwa mbele ya familia yake kwamba aache umbeya; halafu unasema unaijua Dar es salaam?!
Enzi hizo, mdunduko unaanzia Temeke Mikoroshini hadi Mwananyamala kwa Waswahili wenzetu and all the way to Mwananyamala watu wanaunga tela njiani...!!
Na kama kuna ndugu wengine say pande za Msasani huko (sio Msasani ya Kishua) basi mdundiko hautaishia Mwanyamala!!
Hiyo ndo Dar es salaam, na mambo mengine yoooote ni fake!! Huwezi kuitenganisha Dar es salaam na Uswahili au na uhuni wa Kiswazi!!
I miss Temeke, ndo vile tu ili kupambana na maisha wanaume tunatakiwa kuwa mbali na familia na ndugu!!!
Nimeona hapo juu
Jason Statham2 akisema "hiyo ndo TMK yetu, mtuache", nami nakazia, tuachieni Temeke yetu!!