Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
- Thread starter
- #81
Umetoa tamko kuonesha uelewa halafu umeturudisha kule kule.Kwanini kama ni magaidi wajifiche ndani ya dini ya kiislalmu.Kwani nani kasema dini ya kiislamu ni dini ya magaidi.Kwa kifupi tu, hali si nzuri.. Jeshi liko on patrol 24 hours.. Kuna kambi kambi ndogo nyingi tu alongside Ruvuma River kuulinda mpaka..
Wapo Makanali ambao ndio wanacoordinate hiyo kazi chini ya brigade kubwa ya Songea na Kambi nyingine ndogo za Nachingwea na Naliendele Mtwara.
Hao watu wanaweza wasiwe ISS lakini ni magaidi waliojificha kwenye dini ya kiislamu. Muda mfupi badala ya shambulio la Kwanza la Kitaya walikamatwa watu makazi yao yakiwa Msikitini kijiji cha Msimbati na wengine Kijiji cha Madimba ilipo Plant ya kuchakata gesi.
Vifaa vingi tu vya kisasa vishapelekwa huko mpakani na msitu mkubwa ulioko Msumbiji wanakodhaniwa hao watu wanajificha unafyekwa kidogo kidogo kusaidia operation. Hali huku si nzuri, watu saa 1 jioni wako ndani
Wapiganaji gani ambao wanaweza kupigana kuuwa na hata kukimbizana na jeshi halafu wakajifiche msikitini.Misikiti inakuwa kwenye mitaa watu wanaoswali wanajuwana.Kama walikutwa watu misikitini hii ni kwa vile watu wakipatwa na hofu mara nyingi wanakimbilia nyumba za ibada kudhani watapata amani kama ilivyokuwa misikiti ya Rwanda miaka ile.Na hata watu waovu nao wakiona usalama wao uko hatarini hukimbilia huko.Lakini huwezi kusema ukikuta mtu muovu yumo humo ukasema ndio kambi yake ya kufanyia uovu.Ukiwa na mawazo hayo wewe mwenyewe itakuwa una chuki na hiyo nyumba.