Msumbiji hakuna ISIS, ni usanii na dhulma. Ukifuatana nami utajua

Habari za ISIS na mauwaji nchini Msumbiji zimesambaa sana na zimeanza kujadiliwa mpaka Umoja wa Mataifa.Bila kujali ukubwa wa taarifa hizo na umbali zilikofika tujaribu kuwa watulivu ili tujadiliane na tufikie pazuri kuepusha madhara zaidi.

Waislamu tuna maelekezo tunapofikiwa na taarifa ya jambo kabla hatujaanza kuchukua hatua za kushughulikia taarifa hizo
{ {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ} } [الحجرات 6]
Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari yoyote msimkubalie tu, bali pelelezeni kwanza, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda}

Kutokana na ukubwa wa habari,madhara yanayotokea na zaidi yale yatakayofuatia ni muhimu kujadiliana kwa undani kuona kasoro ya hoja ya kuwepo kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kinachosemekana kinauwa watu hovyo na kuwazidi nguvu majeshi ya nchi hiyo na pia wamewahi hata kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kuuwa watu.

Hoja zangu za kufanya upembuzi zinaweza kuwa nyingi na ndefu lakini kwa ufupi tu ni kuwa kikundi hicho kinasemekana ni cha waislamu wenye msimamo mkali na kimekula kiapo kuwa chini ya ISIS wale tuliowahi kuwasikia nchini Iraq na maeneo mengi ya Mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Kwa hivyo hawa ISIS wa Msumbiji ni kama tawi la ISIS ya kimataifa. Na kwa huku kusini mwa Afrika walianzia kuwa Alshabab halafu wakwa karibu na Aboud Rogo halafu wakavuka mpaka wakafika Kibiti na baadae kufika Cabo del Gado nchini Msumbiji ambako wamekuwa wengi na kupata nguvu pengine kuliko Alshabaab na Alqaeda.

1.Ikiwa picha ni hiyo,kiongozi wao ni nani na wapi ndio makao yao makuu wanakopeleka taarifa za utiifu na mafanikio ya mashambulio yao?

2.Wapi wanapata silaha na gharama za kuendesha harakati zao?

3.Eneo la Cabo ni misitu minene kama ya Kongo na mapango kama Afghanistan au ni tambarare na vichaka vya mikorosho vinavyofanana na maeneo ya Mtwara nchini Tanzania ?

4.Jeshi la Msumbiji limepata mafunzo wapi na silaha zao wanauziwa na nani kiasi kwamba hawafui dafu kwa vijana hao wa ISIS ambao baadhi ya watoa taarifa husema ni wahuni wanaotokana na vijana waliokosa ajira na wenye njaa.

5.Kwanini hao ISIS wanapouwa huwa hawapati upinzani kutoka kwa wanavijiji ambao kama hawana silaha za kijeshi basi wana silaha za jadi na watu wa makabila ya kimakonde ni maarufu kwa matumizi ya silaha za jadi wanapovamiwa.

6.Hao ISIS wa Msumbiji kama wapo hawaoni kwamba wanapoteza muda bure hilo lengo wanalohusishwa nalo eti kuanzisha dola ya kiislamu itakayokuwa na bendera ya rangi nyeusi,kwa sababu wenzao wote kuanzia Iraq,Ufaransa,Mali mpaka Somalia hakuna walipofanikiwa.Ni wapambanaji gani wajinga hao watakaokuwa kila siku hawabadili mbinu za kivita hata wanaposhindwa.

7. Kama ni kikundi cha waislamu kweli mbona wanafanya kinyume na Uislamu na tofauti sana na wale wanaodaiwa ni wenzao wa nchi nyengine. Mbona wao wamekuwa ovyo sana katika mapambano yao wanauwa tu hata hawajachokozwa.Wana tatizo gani na ndugu zao na majirani zao.

Maswali yote hayo hapo juu majibu yake yanaweza kutoa majibu kuwa kikundi cha ISIS cha Msumbiji na yale yanayotajwa kutendwa nao ni vitu hewa na haviingii akilini kwa watu wenye nia thabiti ya kujua ukiondoa wale wanaoshabikia kwa ujinga na chuki zao.

View attachment 1624211
Skiza wale wa Msumbiji wantumia kuran na wanamtaj allah the same to IS....
shida ni kuwa hamtakakagi waonekane kama hawa ni imani moja na nyinyi ila hawa ni fanatics au pervert worshipers....mbona wale ant Baraka wa Central Afrika tuliwakubali kuwa ni wakristo wenzetu lakini hatufurahii waliyokuwa wanafanya........huwezi kuwakana tena wale ansemwa kuwa ndo wanaijua dini yenu kuliko nyinyi
 
Ukisema wao wamesema. ni wapi walisema?.Lete link ya website yao au tupe frequency za redio yao ili tusikilize.
kila wakikata kichwa wanasema 'Allah Akbaru' na kupeperushwa bendera lao jeusi
 
Njoo nikupe nauli uende Cabo Delgado ujeshwaini utupe mrejesho kama hujatatuliwa Malinda wewe.

Watu wanakufa unaleta upumbavu wako.
Watu yawezekana kweli wanakufa.Nani anayewauwa.Jee ni ISIS ndio mada yetu.
 
Aisee wewe jamaa, hili jambo hauna detail nalo vizuri,ni heri uliache usije onekana kama wamekutuma na hao ISIS,ushauri tu wa bure kwako.
Mimi nasema hawapo na siwaamini.Wewe unasema itasemwa wamenituma.Watu wasiojulikana watamtuma nani.Na kama kuna wajinga watajitokeza kusema ndio wao basi sina muda ya kukutana na watu wajinga.Kwa sababu Uislamu hauna nafasi kwa watu wapuuzi wanaotumikia mabeberu,wanapewa ajenda halafu wanatoa mwanya wa kuuliwa waislamu na kunyang'anywa maeneo yao.
 
Umeandika huko Msumbiji hakuna Isis ila kuna usanii ila hujatuambia huo usanii ni upi?
Usanii wenyewe ni huu wa kupewa habari bila ushahidi wa maana.Watu wa Cabo wengi wanajua Kiswahili.Hebu hizi taarifa ziwanukuu kwa sura na maneno yao tuwasikie. Isiwe kila siku tunasoma taarifa zinazoandikwa studio tu.
 
Skiza wale wa Msumbiji wantumia kuran na wanamtaj allah the same to IS....
shida ni kuwa hamtakakagi waonekane kama hawa ni imani moja na nyinyi ila hawa ni fanatics au pervert worshipers....mbona wale ant Baraka wa Central Afrika tuliwakubali kuwa ni wakristo wenzetu lakini hatufurahii waliyokuwa wanafanya........huwezi kuwakana tena wale ansemwa kuwa ndo wanaijua dini yenu kuliko nyinyi
Ukisema wanamtaja Allah the same as ISIS .Wewe umewaona wapo hao ISIS wa asili na makao makuu yao yapo wapi hapa duniani ?
 
Nadhani it does not matter wanaitwa nini bali kile wanachokifanya kwa vile hakiendani na kuishi kwa utulivu na amani basi wanapaswa kutokomezwa...
 
Nadhani it does not matter wanaitwa nini bali kile wanachokifanya kwa vile hakiendani na kuishi kwa utulivu na amani basi wanapaswa kutokomezwa...
Maneno gani hayo kuwa it does not matter wanaitwa nani?. It matters alot as long as they are associated with islamic faith.They should be called another name relevant to them.
Unajuwa ubaya uko wapi hapa. Huko mbele kuna makubwa kuliko hayo yanayotajwa kukatwa vichwa yanaweza kutokea .Sasa wale watakaoguswa na hilo watakuwa na chuki na kila muislamu na hatimae kupelekea ugomvi na uonevu na mauwaji kwa watu wasiokuwa na hatia, Tumeshuhudia yaliyotokea kule Myamar taarifa za uongo ziliibua makundi kwenda kushambulia waislamu na kuuliwa kwa maelfu.Kwa nini tusizibainishe dalili zinazopelekea huko.
Wauwaji wa Msumbiji kama wapo wapewe majina mengine wanayostahiki na yapo mengi. Wahuni,wasiojulikana na kadhalika ila neno islamic lisiwepo kwani ni jina linalobeba imani ya dini tukufu na isikubali matendo ya kijinga na dini inayofuatwa na watu mabilioni duniani.
 
Mkuu hakuna upembuzi wowote wa maana hapo.

Yani hamna kitu.
IMG_20201109_212859.jpg
 
Wanapewa majina au wanajipa; wewe kama unajua imani yako haendani na matendo yao basi imani endelea kukemea, na waislamu wote waendelee kuwakana na kuwakemea na kuwatenga (sidhani kama kuna mtu anapinga hicho)
 
Usanii wenyewe ni huu wa kupewa habari bila ushahidi wa maana.Watu wa Cabo wengi wanajua Kiswahili.Hebu hizi taarifa ziwanukuu kwa sura na maneno yao tuwasikie. Isiwe kila siku tunasoma taarifa zinazoandikwa studio tu.
Mkuu Mtwara Vijijini na Tandahimba walishaua na kuchoma moto nyumba.

Kwa macho yangu kuna siku nadrive kutoka Mtwara kwenda Newala nashuka Mlima wa Nanyamba nakutana na wanavijiji wengine kwenye pikipiki na mabegi yao, wengine kwa mguu na wengine kwenye magari wakikimbia kutoka kijijini kwao walikovamiwa usiku wake (Kijiji cha Tandahimba sikikumbuki jina).. Na wao kwa kuwauliza walikiri ndugu zao kuchinjwa na wengine walitekwa.. Hiyo ilikuwa siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu..

Hapa ninavyoandika niko moja ya wilaya za Mtwara kwa kazi ya muda kidogo. Bar zinafungwa saa 4 na hauruhusiwi kutembea usiku zaidi ya saa 12 kama huna kitambulisho cha mpiga kura, lakini hauruhusiwi kabisa kutembea juu ya saa 5 usiku na kitakachokukuta usiku huo utasimulia mpaka wajukuu wako.

Acha masihara yako, haya mambo yapo. Na usitake tukutajie mpaka Makanali waliopewa kazi ya kuulinda mpaka wetu kuanzia Kilambo mpaka Nyasa huko..
 
Mtoa mada nakuunga mkono japo wengi hawaelewi unachomaanisha. Kuna mmoja hapo juu amesema kwamba dunia ina mengi tusiyoyajua na mimi nakazia kabisa kwa kusema DUNIA INA WENGI LAKINI WANAOIFAHAMU (NA KUIFAIDI) NI WACHACHE SANA
 
Back
Top Bottom