Msumbiji hakuna ISIS, ni usanii na dhulma. Ukifuatana nami utajua

Habari za ISIS na mauwaji nchini Msumbiji zimesambaa sana na zimeanza kujadiliwa mpaka Umoja wa Mataifa.Bila kujali ukubwa wa taarifa hizo na umbali zilikofika tujaribu kuwa watulivu ili tujadiliane na tufikie pazuri kuepusha madhara zaidi.

Waislamu tuna maelekezo tunapofikiwa na taarifa ya jambo kabla hatujaanza kuchukua hatua za kushughulikia taarifa hizo
{ {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ} } [الحجرات 6]
Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari yoyote msimkubalie tu, bali pelelezeni kwanza, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda}

Kutokana na ukubwa wa habari,madhara yanayotokea na zaidi yale yatakayofuatia ni muhimu kujadiliana kwa undani kuona kasoro ya hoja ya kuwepo kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kinachosemekana kinauwa watu hovyo na kuwazidi nguvu majeshi ya nchi hiyo na pia wamewahi hata kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kuuwa watu.

Hoja zangu za kufanya upembuzi zinaweza kuwa nyingi na ndefu lakini kwa ufupi tu ni kuwa kikundi hicho kinasemekana ni cha waislamu wenye msimamo mkali na kimekula kiapo kuwa chini ya ISIS wale tuliowahi kuwasikia nchini Iraq na maeneo mengi ya Mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Kwa hivyo hawa ISIS wa Msumbiji ni kama tawi la ISIS ya kimataifa. Na kwa huku kusini mwa Afrika walianzia kuwa Alshabab halafu wakwa karibu na Aboud Rogo halafu wakavuka mpaka wakafika Kibiti na baadae kufika Cabo del Gado nchini Msumbiji ambako wamekuwa wengi na kupata nguvu pengine kuliko Alshabaab na Alqaeda.

1.Ikiwa picha ni hiyo,kiongozi wao ni nani na wapi ndio makao yao makuu wanakopeleka taarifa za utiifu na mafanikio ya mashambulio yao?

2.Wapi wanapata silaha na gharama za kuendesha harakati zao?

3.Eneo la Cabo ni misitu minene kama ya Kongo na mapango kama Afghanistan au ni tambarare na vichaka vya mikorosho vinavyofanana na maeneo ya Mtwara nchini Tanzania ?

4.Jeshi la Msumbiji limepata mafunzo wapi na silaha zao wanauziwa na nani kiasi kwamba hawafui dafu kwa vijana hao wa ISIS ambao baadhi ya watoa taarifa husema ni wahuni wanaotokana na vijana waliokosa ajira na wenye njaa.

5.Kwanini hao ISIS wanapouwa huwa hawapati upinzani kutoka kwa wanavijiji ambao kama hawana silaha za kijeshi basi wana silaha za jadi na watu wa makabila ya kimakonde ni maarufu kwa matumizi ya silaha za jadi wanapovamiwa.

6.Hao ISIS wa Msumbiji kama wapo hawaoni kwamba wanapoteza muda bure hilo lengo wanalohusishwa nalo eti kuanzisha dola ya kiislamu itakayokuwa na bendera ya rangi nyeusi,kwa sababu wenzao wote kuanzia Iraq,Ufaransa,Mali mpaka Somalia hakuna walipofanikiwa.Ni wapambanaji gani wajinga hao watakaokuwa kila siku hawabadili mbinu za kivita hata wanaposhindwa.

7. Kama ni kikundi cha waislamu kweli mbona wanafanya kinyume na Uislamu na tofauti sana na wale wanaodaiwa ni wenzao wa nchi nyengine. Mbona wao wamekuwa ovyo sana katika mapambano yao wanauwa tu hata hawajachokozwa.Wana tatizo gani na ndugu zao na majirani zao.

Maswali yote hayo hapo juu majibu yake yanaweza kutoa majibu kuwa kikundi cha ISIS cha Msumbiji na yale yanayotajwa kutendwa nao ni vitu hewa na haviingii akilini kwa watu wenye nia thabiti ya kujua ukiondoa wale wanaoshabikia kwa ujinga na chuki zao.

View attachment 1624211
Nimepitia hoja zako lakin Bado hujatoa hoja zenye mashiko na kusem haingii akilini , hoja zako Bado Ni futile.
Na jib kwa maswali baadh ya hoja zako Kama ifuatavyo:-

1: Una uhakika mashambulizi yaliyofanywa na Islamist militants msumbiji yamehusisha silaha za jadi tu?

2: Siyo wapambanaji wajinga kwa kubadili mbinu wanaposhindwa hata Alshabab, Boko Haram, ISIS hubadilili mbinu wanaposhindwa basi nao Ni wapambanaji wa kiislamu wajinga kma hao wa Msumbiji

3: Jeshi la Nigeria lipo rank ya juu, Ni moja ya nchi zenye uwezo mkubwa wa kijesh Afrika lakin wanaelemewa na kushindwa fua dafu dhid ya Boko Haram Kuna matukio kadhaa wanaelemewa je na wenyewe wanapata mafunzo wap na silaha wanapata wapi sawsawa na Somalia na hushindwa hadi kuitaj msaada wa nje je nao hupata wapi mafunzo na silaha nakushindwa kwao haimanish waasi si wakiislamu na hivyo basi hata msumbiji inaweza kuwa hivyohivyo

4: ISIS, Al shabab , Bokoramu hupata wapi silaha, basi hata waasi wa msumbiji hivyohivyo.

5: Kama unasema hawa wa msumbiji wanaenda tofauti na uislam tofaut na wale wa ISIS, Al shabab , Bokoharam ambao hawaendi kinyume na uislam kama hoja yako je una mtazamo gani kuwa uislam kuhisishwa na ugaidi Kama hao wengine wanatenda sawasawa na uislam kama ulivoeleza?
 
Back
Top Bottom