Jeshi la Rwanda kusalia Msumbiji

Jeshi la Rwanda kusalia Msumbiji

zwangandaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2023
Posts
750
Reaction score
1,426
Swalama wakuu!

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC inajiandaa kuondoa kikosi chake lilichoko Msumbiji kusaidia serikali kupambana na magaidi wa kiislaam ifikapo July 15 2024 baada ya kuwa huko tangu 2018 mwishoni.

Kikosi hicho kijulikanacho kama SAMIM chenye jumla ya wapiganaji 1900 kimekuwa huko kwa lengo la kupambana na magaidi, kujenga uwezo kwa majeshi ya serikali lakini pia kuongeza wigo wa misaada ya kiutu kwa raia.

Wakati SADC wakijikusanya mdogomdogo kukusanya vikosi, rais wa Msumbiji Phelipe Nyusi mwaka 2020 alifanya ziara Rwanda na kukutana na rais Kagame na kuomba msaada wa kijeshi.

Mwaka 2021 Rwanda ilipeleka askari 1000 na ndani ya miezi 3 walifaniliwa kuiteka moja ya ngome ya waasi na kukomboa miji kadhaa kutoka milononi mwa magaidi.

Jambo la kushangaza wakati SADC wanaondoa majeshi yake kutokana na ukata, Rwanda mpaka sasa imeendelea kuongeza askari kifikia 2500 nchini Msumbiji kulinganisha na 1900 wa SADC wanaotarajiwa kuondoka ili hali bado hali ya usalama haijatengemaa kwenye maeneo wanayo yaacha kwa vikosi vya serilali

Ajabu nyingine:
Wakati SADC wakitegemea michango ya AU, China na wafadhili mbalimbali, mpaka muda huu hakuna ajuaye ni nani anagharamia oparesheni za majeshi ya Rwanda yanayo onekena kuwa na vifaa bora na vya kisasa kulinganisha na kikosi cha SAMIM kinachoundwa na askari 1900, askari 1400 wakitoka Afrika ya kusini na wengine kutoka nchi za Botwana, Angola, Malawi, Tanzania na Namibia.

Majeshi ya Rwnda yamejikita maeneo ya Acube, Montepuez na pemba kutokana na maeneo hayo kuwa shuguli za madini ya graphite na gemstones pamoja na Carbo delgado eneo lenye shughuli za uchimbaji wa mafuta pamoja na mkoa wa Palma wenye utajiri wa madini mbalimbali.

Wadadisi wanadai huenda Wanyarwanda wameahidiwa kupewa mafuta na madini kama malipo ya kazi.Raisi Nyusi ametembelea Rwanda mara nyingi kuliko nchi yeyote ya SADC. Na katika moja ya ziara Nyusi alipewa na Kagame zawadi ya shamba pamoja na ng'gombe wenye pembe kubwa.

Ukaribu usio wa kawaida kati ya maraisi hawa na operation za kijeshi zinazotekelezwa bila ya kuwapo uwazi anaegharamia oparesheni za kijeshi kwa vikosi vya Rwanda nchini Msumbiji

Pia hali ya Rwanda kujikita kimkakati na kiufanisi maeneo yenye utajiri wa madini unaleta jibu kuwa huenda wanapigania kwa moyo kile walicho kubaliana kati ya Nyusi na Kagame

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama barani Afrika pia wanafananisha hali ya DR Congo ambako SAMDRC ina pambana na waassi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Ni katika hali kama hiyo, majeshi ya waasi wa m23 yameonekana kutumia silaha bora kuliko za SADC na hata mafanikio ya kikosi cha SADC nchini DRC bado ni madogo kulingana na maadui wao.

Wakati kikosi cha SADC kinagharamiwa na UN, M23 na Rwanda haijulikani nani anawafadhili kwa kiwango kikubwa kiasi hiki kuwa na uwezo wa kukabiliana na kuwapa changamoto majeshi ya SADC.

Kwa mantiki hiyo, utaona kuwa Rwanda huwa hana masihala na eneo lolote barani Afrika ilimradi pawe na raslimali.

Pia kwa kuangalia tu mifano ya nyendo za oparesheni za kijeshi za nchi ya Rwanda nchini Msumbiji na DRC , mwenye akili anapata jibu kuwa kuna wenye nguvu wako nyuma ya nchi hii ndogo ya Afrika Mashariki.

Kwa mantiki hii, huenda amani DRC isipatikane kwa njia ya vita bali mazungumzio juu ya meza.
 
Rwanda Wana siraha Gani Bora kuzidi za SAMIM!?.

Huko DRC kati ya M23 na SAMIDRC nani ana casualties kubwa kuzidi mwenzie?

Upo ulinganifu wa idadi ya askali vifaa, hasara, majeruhi na advancement ya Kila mmoja?.

Hao askali wa congo ni wahuni tu wa mtaani ndio maana congo. Vikisi vya Mizinga, vifaru, super infantry. Havi shiriki mapigano. Hao askali wa congo unao wanna hata Kinshasa haiwaamini. Ukiona special forces za congo eastern congo ujue Kuna afisa muandamizi katembelea na huwezi kusikia Yuko ambushed.
 
Mnajazana ujinga sana juu ya mkoa wa Rwanda. Hawana maajabu yeyote kimedani zaidi ya kuvizia.

Tena nikutaarifu vikosi vya Tanzania vinaogopwa kuliko kikosi chochote huko congo, hao M23 hofu Yao ni askali wa Tanzania kuliko wa south na wengineo.
 
80% ya oparation za SADC inategemea South Africa kwa sababu angalau ndio wana silaha za kisasa lakini ukweli ni kwamba SANDF yenyewe kwa sasa inapitia kipindi kigumu cha ukata kwa kutopewa fungu la kutosha na serikali ili kuboresha zana.

Kwa mfano zile helikopta za kushambulia zilizotumiwa mwaka 2013 na FIB( Force Intervention Brigade) dhidi ya M23 kwa sasa hazipo maana serikali ya S.A haina fedha za kuwalipa wazabuni waliokuwa wakizikarabati.

Hii imepelekea vikosi vya SAMIDRC kuwa hatarini muda mwingi dhidi ya adui mwenye silaha bora.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili m23 walionekana kumiliki mitambo ya kudungulia ndege ya kisasa SAM ambayo nchi nyingi za ukanda huu hazimiliki isipokuwa Rwanda na Kenya.
Hata hivyo ilipelekea Marekani kuingilia kati kiitaka serikali ya Rwanda iondoe silaha hizo maramoja

Wachambuzi wa maswala ya kiulinzi na kiusalama wanasema ubora wa silaha za adui ndio kikwazo cha vikosi vya SAMIDRC katika kusonga mbele kukabiliana na waasi ama kuwarudisha nyuma
 
Mnajazana ujinga sana juu ya mkoa wa Rwanda. Hawana maajabu yeyote kimedani zaidi ya kuvizia.

Tena nikutaarifu vikosi vya Tanzania vinaogopwa kuliko kikosi chochote huko congo, hao M23 hofu Yao ni askali wa Tanzania kuliko wa south na wengineo.
We acha historia ya hadithi ya vita vya Idi Amini.

Adui atakuogopa tu kwa uwezo wako kwenye uwanja wa mapambano na uwezo wa kumtia adui hasara na sio hadithi za mababu ama stori za vijiweni.

Katika medani, moja ya njia za kupata ushindi ni kutambua uwezo na nguvu za adui. Kama utakosea hesabu hizo na kutumia mazoea ya jana, hilo litakuwa kosa kubwa
.
 
80% ya oparation za SADC inategemea South Africa kwa sababu angalau ndio wana silaha za kisasa lakini ukweli ni kwamba SANDF yenyewe kwa sasa inapitia kipindi kigumu cha ukata kwa kutopewa fungu la kutosha na serikali ili kuboresha zana.

Kwa mfano zile helikopta za kushambulia zilizotumiwa mwaka 2013 na FIB( Force Intervention Brigade) dhidi ya M23 kwa sasa hazipo maana serikali ya S.A haina fedha za kuwalipa wazabuni waliokuwa wakizikarabati.

Hii imepelekea vikosi vya SAMIDRC kuwa hatarini muda mwingi dhidi ya adui mwenye silaha bora.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili m23 walionekana kumiliki mitambo ya kudungulia ndege ya kisasa SAM ambayo nchi nyingi za ukanda huu hazimiliki isipokuwa Rwanda na Kenya.
Hata hivyo ilipelekea Marekani kuingilia kati kiitaka serikali ya Rwanda iondoe silaha hizo maramoja

Wachambuzi wa maswala ya kiulinzi na bwakiusalama wanasema ubora wa silaha za adui ndio kikwazo cha vikosi vya SAMIDRC katika kusonga mbele kukabiliana na waasi ama kuwarudisha nyuma
Mkuu hoja ya kuitegemea south Africa sio timilifu japo Ina matter. Operation nyingi za SADEC huwa zina back up ya mataifa makubwa.

SAMIM mchina alijitolea kufund nje ya bajet ya SADEC France the same. Pia nikujuze France inafanya juhudi kubwa kuli hozi soko la silaha la Tanzania, Kwa kutaka kuipiku NATO community weapon deployed in Tanzania. Kwa Muda mrefu Tanzania wasambazaji wakubwa wa silaha walikua ni Russia,China, North Korea,UK,na turkey.

Ila kwasasa mfumo wa wa ugavi silaha wa bongo umejikita zaidi. Uchina Kwa silaha hasa land force na Navy Air for. Russia Air defense na strategy weapon hasa hasa makombola. France Air force na Navy. Israel light weapon na Uturuki Kwa bunduki na drone.

Pia Kuna masoko ya kimkakati kama. Italy Kwa transport mfano ni Iveco na Sasa tume oder C-27J Spartan 2. Kuzisaidia zile Shaanxi Y8 na An 12 zinazoenda kuretire. Amerika Kwa mifumo ya mawasiliano, India nk.

Hivyo hoja ya kusema Rwanda Wana air defense Kali sio kweli hizo unazosema, WZ551 6×6 IFV mobile SAM system. Ni silaha za kujikinga na object ndogo ndogo na zinazo fly chini chini kama helicopter na drone ambazo jeshi la congo na Un wamekua wakizitumia. Either ktk surveillance au attack Kwa waasi wa M23.

South Africa sio wazuri ktk gorilla 🦍 warfare. Ndio maana hata kimajukumu Tanzania ndio inayo hold zaidi jungle to jungle battle, pia hapo hapo ktk SAMIDRC hawapigani pamoja Kila mtu anapewa majukumu yake hivyo ukinzani wanao kutana nao M23 Kwa Tanzania hata wewe unapokea habari zake pia najua unajua south hawafanyi operation za aina hiyo wao haswa ni air attack. Halipingwi hili.

Unasema story za Kagera war wakati fact zipo mkuu. Kubali ukatae JWTZ singe wanachoma kweli kweli.
 
We acha historia ya hadithi ya vita vya Idi Amini.

Adui atakuogopa tu kwa uwezo wako kwenye uwanja wa mapambano na uwezo wa kumtia adui hasara na sio hadithi za mababu ama stori za vijiweni.

Katika medani, moja ya njia za kupata ushindi ni kutambua uwezo na nguvu za adui. Kama utakosea hesabu hizo na kutumia mazoea ya jana, hilo litakuwa kosa kubwa
.
Hii ni SAMIM bunduki Israel gear za mchina.

Mkuu kubali ukatae JWTZ ni wajuzi wa hizi kazi, Kagera war haipingiki. Ni experience inayo ishi ktk vizazi vya wapiganaji na makamanda. Kama kweli we ni mfatiliaji utajua kua hata upigaji wa Mizinga wa Tanzania ni waki Russia. Ambayo ni experience tuliyo ipata Toka enzi za harakati za ukombozi. Fatilia video zinazo onyesha askali wa Tanzania wakifanya live fire🔥. Hata Bm21 bavuor machine upigaji wa Tanzania ni ule ule wa kirusi na hata uchina upigaji wake ni tofauti na sisi.
 
Attachments

  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    52.4 KB · Views: 40
Total anamradi mkubwa sana huko kwanini yeye Total asiwalipe Askari wanaopambana na Magaidi.

Na ni kwanini Nchi za SADC zisiaidie kulijenga Jeshi la Mozambique ili liweze kupambana na Magaidi bila kuhitaji msaada.
 
Mkuu hoja ya kuitegemea south Africa sio timilifu japo Ina matter. Operation nyingi za SADEC huwa zina back up ya mataifa makubwa.

SAMIM mchina alijitolea kufund nje ya bajet ya SADEC France the same. Pia nikujuze France inafanya juhudi kubwa kuli hozi soko la silaha la Tanzania, Kwa kutaka kuipiku NATO community weapon deployed in Tanzania. Kwa Muda mrefu Tanzania wasambazaji wakubwa wa silaha walikua ni Russia,China, North Korea,UK,na turkey.

Ila kwasasa mfumo wa wa ugavi silaha wa bongo umejikita zaidi. Uchina Kwa silaha hasa land force na Navy Air for. Russia Air defense na strategy weapon hasa hasa makombola. France Air force na Navy. Israel light weapon na Uturuki Kwa bunduki na drone.

Pia Kuna masoko ya kimkakati kama. Italy Kwa transport mfano ni Iveco na Sasa tume oder C-27J Spartan 2. Kuzisaidia zile Shaanxi Y8 na An 12 zinazoenda kuretire. Amerika Kwa mifumo ya mawasiliano, India nk.

Hivyo hoja ya kusema Rwanda Wana air defense Kali sio kweli hizo unazosema, WZ551 6×6 IFV mobile SAM system. Ni silaha za kujikinga na object ndogo ndogo na zinazo fly chini chini kama helicopter na drone ambazo jeshi la congo na Un wamekua wakizitumia. Either ktk surveillance au attack Kwa waasi wa M23.

South Africa sio wazuri ktk gorilla warfare. Ndio maana hata kimajukumu Tanzania ndio inayo hold zaidi jungle to jungle battle, pia hapo hapo ktk SAMIDRC hawapigani pamoja Kila mtu anapewa majukumu yake hivyo ukinzani wanao kutana nao M23 Kwa Tanzania hata wewe unapokea habari zake pia najua unajua south hawafanyi operation za aina hiyo wao haswa ni air attack. Halipingwi hili.

Unasema story za Kagera war wakati fact zipo mkuu. Kubali ukatae JWTZ singe wanachoma kweli kweli.
Saluti kwako mkuu umeongea kitaalam sio kishabiki japo sikubaliani nawewe kwenye baadhi ya vipengele lakini niseme:
Napokea taarifa!
 
Total anamradi mkubwa sana huko kwanini yeye Total asiwalipe Askari wanaopambana na Magaidi.

Na ni kwanini Nchi za SADC zisiaidie kulijenga Jeshi la Mozambique ili liweze kupambana na Magaidi bila kuhitaji msaada.
Kwenye taarifa iliyo tolewa na SAMIM iliainisha majukumu Yao yaliyo wapeleka, ambapo pamoja na kuludisha hali ya amani Kwa wananchi pia walikua na jukumu la kulijenga jeshi la msumbiji ki mbinu na medani.

Lakini ushirikiano hafifu baina ya SAMIM na serikali ya Msumbiji imeifanya SAMIM kuona Kuna walakini wa dhamira yao kurudisha hali ya usalama.

Kulikua na intelligence and information sharing lakini ikitaka kufanyika operation unakuta magaido washaondoka eneo la tukio. Ikafikia kipindi Hadi Polisi wakawa wanapeleka taarifa Sasa Kwa SADEC badala ya police msumbiji. Kumbuks Polisi sio sehemu ya SAMIM.

Ilifika kiwango taarifa zinabidi ziende man to man maana uaminifu ulipungua. Sasa sehemu kama hiyo unaendelea na operation ya nini wakati muhanga hataki msaada wako?.
 
Attachments

  • images (5).jpeg
    images (5).jpeg
    60.7 KB · Views: 43
Swalama wakuu!

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC inajiandaa kuondoa kikosi chake lilichoko Msumbiji kusaidia serikali kupambana na magaidi wa kiislaam ifikapo July 15 2024 baada ya kuwa huko tangu 2018 mwishoni.

Kikosi hicho kijulikanacho kama SAMIM chenye jumla ya wapiganaji 1900 kimekuwa huko kwa lengo la kupambana na magaidi, kujenga uwezo kwa majeshi ya serikali lakini pia kuongeza wigo wa misaada ya kiutu kwa raia.

Wakati SADC wakijikusanya mdogomdogo kukusanya vikosi, rais wa Msumbiji Phelipe Nyusi mwaka 2020 alifanya ziara Rwanda na kukutana na rais Kagame na kuomba msaada wa kijeshi.

Mwaka 2021 Rwanda ilipeleka askari 1000 na ndani ya miezi 3 walifaniliwa kuiteka moja ya ngome ya waasi na kukomboa miji kadhaa kutoka milononi mwa magaidi.

Jambo la kushangaza wakati SADC wanaondoa majeshi yake kutokana na ukata, Rwanda mpaka sasa imeendelea kuongeza askari kifikia 2500 nchini Msumbiji kulinganisha na 1900 wa SADC wanaotarajiwa kuondoka ili hali bado hali ya usalama haijatengemaa kwenye maeneo wanayo yaacha kwa vikosi vya serilali

Ajabu nyingine:
Wakati SADC wakitegemea michango ya AU, China na wafadhili mbalimbali, mpaka muda huu hakuna ajuaye ni nani anagharamia oparesheni za majeshi ya Rwanda yanayo onekena kuwa na vifaa bora na vya kisasa kulinganisha na kikosi cha SAMIM kinachoundwa na askari 1900, askari 1400 wakitoka Afrika ya kusini na wengine kutoka nchi za Botwana, Angola, Malawi, Tanzania na Namibia.

Majeshi ya Rwnda yamejikita maeneo ya Acube, Montepuez na pemba kutokana na maeneo hayo kuwa shuguli za madini ya graphite na gemstones pamoja na Carbo delgado eneo lenye shughuli za uchimbaji wa mafuta pamoja na mkoa wa Palma wenye utajiri wa madini mbalimbali.

Wadadisi wanadai huenda Wanyarwanda wameahidiwa kupewa mafuta na madini kama malipo ya kazi.Raisi Nyusi ametembelea Rwanda mara nyingi kuliko nchi yeyote ya SADC. Na katika moja ya ziara Nyusi alipewa na Kagame zawadi ya shamba pamoja na ng'gombe wenye pembe kubwa.

Ukaribu usio wa kawaida kati ya maraisi hawa na operation za kijeshi zinazotekelezwa bila ya kuwapo uwazi anaegharamia oparesheni za kijeshi kwa vikosi vya Rwanda nchini Msumbiji

Pia hali ya Rwanda kujikita kimkakati na kiufanisi maeneo yenye utajiri wa madini unaleta jibu kuwa huenda wanapigania kwa moyo kile walicho kubaliana kati ya Nyusi na Kagame

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama barani Afrika pia wanafananisha hali ya DR Congo ambako SAMDRC ina pambana na waassi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Ni katika hali kama hiyo, majeshi ya waasi wa m23 yameonekana kutumia silaha bora kuliko za SADC na hata mafanikio ya kikosi cha SADC nchini DRC bado ni madogo kulingana na maadui wao.

Wakati kikosi cha SADC kinagharamiwa na UN, M23 na Rwanda haijulikani nani anawafadhili kwa kiwango kikubwa kiasi hiki kuwa na uwezo wa kukabiliana na kuwapa changamoto majeshi ya SADC.

Kwa mantiki hiyo, utaona kuwa Rwanda huwa hana masihala na eneo lolote barani Afrika ilimradi pawe na raslimali.

Pia kwa kuangalia tu mifano ya nyendo za oparesheni za kijeshi za nchi ya Rwanda nchini Msumbiji na DRC , mwenye akili anapata jibu kuwa kuna wenye nguvu wako nyuma ya nchi hii ndogo ya Afrika Mashariki.

Kwa mantiki hii, huenda amani DRC isipatikane kwa njia ya vita bali mazungumzio juu ya meza.

..DRC na Msumbiji ni miradi ya kutajirisha genge linalotawala Rwanda.

..Madini na rasilimali nyingine zinazovunwa huko mauzo yake yanatajirisha watu wachache walioko ktk jeshi na serikali ya Rwanda.
 
Kulikua na intelligence and information sharing lakini ikitaka kufanyika operation unakuta magaido washaondoka eneo la tukio. Ikafikia kipindi Hadi Polisi wakawa wanapeleka taarifa Sasa Kwa SADEC badala ya police msumbiji. Kumbuks Polisi sio sehemu ya SAMIM.
Jeshi la Mozambique lilikuwa imara lakini liliporojeshwa na Serikali ya Makaburu walipoiasisi RENAMO na kumsaidia Alfonso Dlakama.

Jeshi lilikuwa limetoka Msituni likiwa likiwa chini ya FRELIMO kusema na ule ukweli lilikuwa bado liko katika muundo wa kupigana Vita vya Guerilla halikupata fursa ya kutulia na kujijenga kuwa Jeshi lililo na weledi.

Kujenga Jeshi imara lenye nidhamu sio kazi ndogo mfano mzuri angalia RPF hadi leo Jeshi la Rwanda lilikuwa Rag tag Millitias few years ago leo hii linafanya kazi ambayo Jeshi la Mozambique lilishindwa kwa zaidi ya Miaka miwili.
 
Huu uzi unahusu Msumbiji na magaidi ya kiislamu kule, mumeugeuza na kujadili M23
 
Rwanda Wana siraha Gani Bora kuzidi za SAMIM!?.

Huko DRC kati ya M23 na SAMIDRC nani ana casualties kubwa kuzidi mwenzie?

Upo ulinganifu wa idadi ya askali vifaa, hasara, majeruhi na advancement ya Kila mmoja?.

Hao askali wa congo ni wahuni tu wa mtaani ndio maana congo. Vikisi vya Mizinga, vifaru, super infantry. Havi shiriki mapigano. Hao askali wa congo unao wanna hata Kinshasa haiwaamini. Ukiona special forces za congo eastern congo ujue Kuna afisa muandamizi katembelea na huwezi kusikia Yuko ambushed.
We bwana umenikumbusha kitu,mjomba aliwahi nisimulia kuhusu comando wa Congo ni balaa wale wana uwezo mkubwa sana nasikia basi tu sijui inakuaje pale
 
Rwanda Wana siraha Gani Bora kuzidi za SAMIM!?.

Huko DRC kati ya M23 na SAMIDRC nani ana casualties kubwa kuzidi mwenzie?

Upo ulinganifu wa idadi ya askali vifaa, hasara, majeruhi na advancement ya Kila mmoja?.

Hao askali wa congo ni wahuni tu wa mtaani ndio maana congo. Vikisi vya Mizinga, vifaru, super infantry. Havi shiriki mapigano. Hao askali wa congo unao wanna hata Kinshasa haiwaamini. Ukiona special forces za congo eastern congo ujue Kuna afisa muandamizi katembelea na huwezi kusikia Yuko ambushed.
Kuna jambo ambalo watu wengi hawajui kuhusu Congo na SADEC
Jeshi la SADEC kule Congo limezuiliwa kupigana vita badala yake wanatoa msaada kwa jeshi la Congo.
Mwazoni Jeshi la SADEC lilikuwa linapigana kuna mashambulizi yalifanyika Jeshi la Tanzania, M23 wakapeleka malalamiko UN maamuzi yaliyofanyika na America pia akaingilia. SADEC ikazuiwa kufanya mashambulizi hata mashambulizi kwa kutumia ndege wamezuia.
Shida ndipo ilipo
 
Hiyo Project ya Total Mozambique ni zaidi ya Dola za Kimarekani Billioni 30 Mozambique itafaidika na huo mradi ni pesa nyingi sana Askari wa Rwanda walipwe Direct na Total ili Gesi ichimbwe ipelekwe sokoni
 
Kuna jambo ambalo watu wengi hawajui kuhusu Congo na SADEC
Jeshi la SADEC kule Congo limezuiliwa kupigana vita badala yake wanatoa msaada kwa jeshi la Congo.
Mwazoni Jeshi la SADEC lilikuwa linapigana kuna mashambulizi yalifanyika Jeshi la Tanzania, M23 wakapeleka malalamiko UN maamuzi yaliyofanyika na America pia akaingilia. SADEC ikazuiwa kufanya mashambulizi hata mashambulizi kwa kutumia ndege wamezuia.
Shida ndipo ilipo
Yale ni maslahi ya watu
 
Back
Top Bottom