Msumbiji hakuna ISIS, ni usanii na dhulma. Ukifuatana nami utajua

Haileti maana kuwa kila uovu unaotendwa kuhusishwa na Uislamu.

Wakenya wameact mara nyingi sana au wametaka nchi yao iwe uwanja wa wasanii.Mpaka leo ilikuwaje kwenye ile mall haijaeleweka.Hatutaki Tanzania iwe na usanii kama ule.
leo ndo mara ya kwanza naona mtu anajiquote halafu anajipinga
 
Mkuu Mtwara Vijijini na Tandahimba walishaua na kuchoma moto nyumba.

Kwa macho yangu kuna siku nadrive kutoka Mtwara kwenda Newala nashuka Mlima wa Nanyamba nakutana na wanavijiji wengine kwenye pikipiki na mabegi yao, wengine kwa mguu na wengine kwenye magari wakikimbia kutoka kijijini kwao walikovamiwa usiku wake (Kijiji cha Tandahimba sikikumbuki jina).. Na wao kwa kuwauliza walikiri ndugu zao kuchinjwa na wengine walitekwa.. Hiyo ilikuwa siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu..

Hapa ninavyoandika niko moja ya wilaya za Mtwara kwa kazi ya muda kidogo. Bar zinafungwa saa 4 na hauruhusiwi kutembea usiku zaidi ya saa 12 kama huna kitambulisho cha mpiga kura, lakini hauruhusiwi kabisa kutembea juu ya saa 5 usiku na kitakachokukuta usiku huo utasimulia mpaka wajukuu wako.

Acha masihara yako, haya mambo yapo. Na usitake tukutajie mpaka Makanali waliopewa kazi ya kuulinda mpaka wetu kuanzia Kilambo mpaka Nyasa huko..
Sasa mbona hamtuambii ni kina nani hao ?

Mimi kwa habari zilizo nifikia ni kuwa mauaji ya kule ni masuala ya ardhi, ya watu fulani kuingia sehemu ya wengine, ndiyo maana Jeshi la Tanzania limepelekwa kule kuwaondoa raia wa Tanzania na kuwahamisha katika hicho kijiji ambacho wamevamiwa na watu wa nchi husika. Kadhalika ni kweli watu wamepigwa marufuku kutembea usiku na mengine mfano wa hayo na kule watu imekuwa ngumu kuondoka kijiji kile sababu walishazaliana na kuwekeza shughuli zao. Wahusika wanalalama ya kuwa Jeshi la Tanzania linawatoa kule bila kuwaandalia mazingira ya kuka kuishi makazi mapya.
 
Yaani mimi hata hao wanaojinasibu na Uislamu labda kina Ilunga au Aboud Rogo ambao tulikuwa tunawaona kwa macho mpaka akauawa vile watu dizaini ile ndo naamini kweli watetezi wa dola ya kiislamu (japo wana mapungufu nao) lakini hao wengine wa kutangaziwa na 'intanashino propaganda midiaz' sitakaa niamini kabisa

Haiwezekani wahuni fulani wanaamua kuunda muvi yao kwa kuua watu kusudi na kisha kuitangazia dunia kuwa wao ni WAISLAMU wanaotetea Uislamu.

Mimi huwa najiuliza hivi ni kweli mtu aue halafu achukue dhima ya kujitangaza eti; tena mara nyingine aseme kabisa ataua sehemu fulani!!! sasa basi sawa maana hata wahalifu wengine wana huo mchezo/mtindo lakini sasa mbona wahalifu wengine hao wanashikwa mara nyingi na kuzuia/kusitishwa mipango yao vipi kwa hawa wengine vyombo vya ulinzi vinakwama wapi?

Mimi sipingi kuhusu kufa ni kweli watu wanauawa sana na watu au makundi hayo (na ninalaani kwelikweli) lakini naona kuna maelezo yanayoandaliwa juu ya mauaji hayo mengine yanaongezewaga tu kwa malengo fulani fulani

Angalia mifano hii;

1 Kuhusu Osama
-alikuwa akigeuka sura (kujibadilisha awe jiwe, mdudu, kizee nk)
-alikuwa akipotea kiajabu hata akizingirwa na majeshi
-alikuwa akilipua Wamarekani (Mfano Pentagon na baadhi ya Balozi za America)
- alikuwa...

2. Kuhusu Idd Amin
-alikuwa anabaka wasichana na kujilimbikizia/kujimilikisha wanawake wazuri
-alikuwa akila watu nyama
-alikuwa akiwabinulia baharini kwa lori (tipa) watu wasiojiweza mfano wazee sana watoto na walemavu
-alikuwa muuaji

3. Kuhusu Al-Qaeda, Al-Shabaab na wengineo
-wanaua yeyote ambaye si Mwislamu
-wanalazimisha watu kutii sheria za kiislamu
-wanajitoa mhanga (kujilipua mabomu) kwenye kadamnasi kama masokoni na viwanjani
-wanateka watu (hasa watoto) na kuwafundisha Qur'an na uhalifu unaofahamika kama ugaidi
-wanateka watu na kuwafanyia interview (kutaja majina, kusoma Qur'an na kadhalika) na atakayethibitika kufeli wanamuua
-wana makao yao ya siri ambayo hata majeshi halali hayapatambui
-wanateka watu/watoto wengi sana na kuwaficha kusikojulikana
-wanachinja watu kwa kuanzia nyuma (nyuma ya shingo)
Na kadhalika na kadhalika.
 
Tabia za ISIS kote duniani zinafanana.. sijaona kipy hapo hao ni wauaji tu..
Mi nadhani mwandishi angejikita zaidi kwenye kuitoa ISIS na mfungamano wa uislamu.
 
Usanii wenyewe ni huu wa kupewa habari bila ushahidi wa maana.Watu wa Cabo wengi wanajua Kiswahili.Hebu hizi taarifa ziwanukuu kwa sura na maneno yao tuwasikie. Isiwe kila siku tunasoma taarifa zinazoandikwa studio tu.
Mkuu kuna video iliwekwa humu iliwaonesha wanaongea kiswahili safi cha Tanzania.
Tunakijua kiswahili cha watu wa Msumbiji.

Wewe unataka kugeuza huu uhalifu kama suala la kidini na kutetea kidini dini.

Juhudi hizi unazotumia kukanusha ungezitumia kuwafundisha wanachofanya siyo sahihi wala siyo sunna huenda wangeacha ule ukatili wa kijinga.
 
Mimi nasema hawapo na siwaamini.Wewe unasema itasemwa wamenituma.Watu wasiojulikana watamtuma nani.Na kama kuna wajinga watajitokeza kusema ndio wao basi sina muda ya kukutana na watu wajinga.Kwa sababu Uislamu hauna nafasi kwa watu wapuuzi wanaotumikia mabeberu,wanapewa ajenda halafu wanatoa mwanya wa kuuliwa waislamu na kunyang'anywa maeneo yao.
Kwa hiyo wewe usipoamini ndio iwe uwongo? Iwe ni ISIS au siyo wenyewe jua kuna kikundi cha kigaidi cha kiislam huko Msumbiji kinachoua watu. Ukiangalia bendera yao, ukataji vichwa huku wakisema Allah Akbar, basi wala huhitaji kujiuliza mengi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Nilivyoona kiarabu katikati nimeacha kusoma hapo hapo... kesi ya nyani haiamuliwi na kima
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kule Zanzibar siku hiyo na ya nyuma yake yalitokea makubwa kuliko hayo uliyoshuhudia huko Mtwara.Jee nako kulikuwa na ISIS.
Haileti maana kuwa kila uovu unaotendwa kuhusishwa na Uislamu.
una maslahi gani na hao ISIS..

umeonyesha kuwasemea,kuwatetea na hata kukanusha uovu wanaowatendea raia wa Mtwara.!?

*Mkuu Ami ingefaa vyombo vya usalama 'wakutafute upate kuwasaidia'...maana tangia wako Kibiti ulikuwa unawatetea na kuwapa kichwa
 
Tabia za ISIS kote duniani zinafanana.. sijaona kipy hapo hao ni wauaji tu..
Mi nadhani mwandishi angejikita zaidi kwenye kuitoa ISIS na mfungamano wa uislamu.
Kote duniani wapi !. Wapi unapajuwa ndio kwao hao ISIS .Kila shirika na taasisi zina anuwani yao.Hawa ISIS mbona anuwani yao ni kwenye vinywa na majarida tu.Na pamoja na kwamba wanatajwa ni waislamu lakini hawana ndugu wanayejuwana nao.Ndugu zao wenye uwezo wa kuwafafanua wamefanya nini ni akina Macron,Penagon na wengine huko Ulaya.
 
una maslahi gani na hao ISIS..

umeonyesha kuwasemea,kuwatetea na hata kukanusha uovu wanaowatendea raia wa Mtwara.!?

*Mkuu Ami ingefaa vyombo vya usalama 'wakutafute upate kuwasaidia'...maana tangia wako Kibiti ulikuwa unawatetea na kuwapa kichwa
Hao vyombo vya usalama wakiona maneno yako haya watakwambia wewe ni mbea tu kwani huna muda wa kutafakari anachoongelea mtu. Wapi nimewahi kuwatetea.Mimi nasema hawapo.Kama ni mauwaji watafutwe watu wengine wapewe majina mengine sio kuwahusisha na uislamu.
 
Kwa hiyo wewe usipoamini ndio iwe uwongo? Iwe ni ISIS au siyo wenyewe jua kuna kikundi cha kigaidi cha kiislam huko Msumbiji kinachoua watu. Ukiangalia bendera yao, ukataji vichwa huku wakisema Allah Akbar, basi wala huhitaji kujiuliza mengi.

Yaani mimi hata hao wanaojinasibu na Uislamu labda kina Ilunga au Aboud Rogo ambao tulikuwa tunawaona kwa macho mpaka akauawa vile watu dizaini ile ndo naamini kweli watetezi wa dola ya kiislamu (japo wana mapungufu nao) lakini hao wengine wa kutangaziwa na 'intanashino propaganda midiaz' sitakaa niamini kabisa

Haiwezekani wahuni fulani wanaamua kuunda muvi yao kwa kuua watu kusudi na kisha kuitangazia dunia kuwa wao ni WAISLAMU wanaotetea Uislamu.

Mimi huwa najiuliza hivi ni kweli mtu aue halafu achukue dhima ya kujitangaza eti; tena mara nyingine aseme kabisa ataua sehemu fulani!!! sasa basi sawa maana hata wahalifu wengine wana huo mchezo/mtindo lakini sasa mbona wahalifu wengine hao wanashikwa mara nyingi na kuzuia/kusitishwa mipango yao vipi kwa hawa wengine vyombo vya ulinzi vinakwama wapi?

Mimi sipingi kuhusu kufa ni kweli watu wanauawa sana na watu au makundi hayo (na ninalaani kwelikweli) lakini naona kuna maelezo yanayoandaliwa juu ya mauaji hayo mengine yanaongezewaga tu kwa malengo fulani fulani

Angalia mifano hii;

1 Kuhusu Osama
-alikuwa akigeuka sura (kujibadilisha awe jiwe, mdudu, kizee nk)
-alikuwa akipotea kiajabu hata akizingirwa na majeshi
-alikuwa akilipua Wamarekani (Mfano Pentagon na baadhi ya Balozi za America)
- alikuwa...

2. Kuhusu Idd Amin
-alikuwa anabaka wasichana na kujilimbikizia/kujimilikisha wanawake wazuri
-alikuwa akila watu nyama
-alikuwa akiwabinulia baharini kwa lori (tipa) watu wasiojiweza mfano wazee sana watoto na walemavu
-alikuwa muuaji

3. Kuhusu Al-Qaeda, Al-Shabaab na wengineo
-wanaua yeyote ambaye si Mwislamu
-wanalazimisha watu kutii sheria za kiislamu
-wanajitoa mhanga (kujilipua mabomu) kwenye kadamnasi kama masokoni na viwanjani
-wanateka watu (hasa watoto) na kuwafundisha Qur'an na uhalifu unaofahamika kama ugaidi
-wanateka watu na kuwafanyia interview (kutaja majina, kusoma Qur'an na kadhalika) na atakayethibitika kufeli wanamuua
-wana makao yao ya siri ambayo hata majeshi halali hayapatambui
-wanateka watu/watoto wengi sana na kuwaficha kusikojulikana
-wanachinja watu kwa kuanzia nyuma (nyuma ya shingo)
Na kadhalika na kadhalika.
Umeona viashiria vya fitna hivyo.Wengi wanashindwa kuving'amua na wanaacha watu wanaumizwa kwa visingizio mbali mbali.Hasa jamii ya kiislamu inaathirika sana na uzushi wa aina hiyo kutoka kwa majirani zao na kutoka vyombo vya dola.
 
mkuu funguka wengine tupo kujifunza sio kubishana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kifupi tu, hali si nzuri.. Jeshi liko on patrol 24 hours.. Kuna kambi kambi ndogo nyingi tu alongside Ruvuma River kuulinda mpaka..

Wapo Makanali ambao ndio wanacoordinate hiyo kazi chini ya brigade kubwa ya Songea na Kambi nyingine ndogo za Nachingwea na Naliendele Mtwara.

Hao watu wanaweza wasiwe ISS lakini ni magaidi waliojificha kwenye dini ya kiislamu. Muda mfupi badala ya shambulio la Kwanza la Kitaya walikamatwa watu makazi yao yakiwa Msikitini kijiji cha Msimbati na wengine Kijiji cha Madimba ilipo Plant ya kuchakata gesi.

Vifaa vingi tu vya kisasa vishapelekwa huko mpakani na msitu mkubwa ulioko Msumbiji wanakodhaniwa hao watu wanajificha unafyekwa kidogo kidogo kusaidia operation. Hali huku si nzuri, watu saa 1 jioni wako ndani
 
Habari za ISIS na mauwaji nchini Msumbiji zimesambaa sana na zimeanza kujadiliwa mpaka Umoja wa Mataifa.Bila kujali ukubwa wa taarifa hizo na umbali zilikofika tujaribu kuwa watulivu ili tujadiliane na tufikie pazuri kuepusha madhara zaidi.

Waislamu tuna maelekezo tunapofikiwa na taarifa ya jambo kabla hatujaanza kuchukua hatua za kushughulikia taarifa hizo
{ {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ} } [الحجرات 6]
Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari yoyote msimkubalie tu, bali pelelezeni kwanza, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda}

Kutokana na ukubwa wa habari,madhara yanayotokea na zaidi yale yatakayofuatia ni muhimu kujadiliana kwa undani kuona kasoro ya hoja ya kuwepo kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kinachosemekana kinauwa watu hovyo na kuwazidi nguvu majeshi ya nchi hiyo na pia wamewahi hata kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kuuwa watu.

Hoja zangu za kufanya upembuzi zinaweza kuwa nyingi na ndefu lakini kwa ufupi tu ni kuwa kikundi hicho kinasemekana ni cha waislamu wenye msimamo mkali na kimekula kiapo kuwa chini ya ISIS wale tuliowahi kuwasikia nchini Iraq na maeneo mengi ya Mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Kwa hivyo hawa ISIS wa Msumbiji ni kama tawi la ISIS ya kimataifa. Na kwa huku kusini mwa Afrika walianzia kuwa Alshabab halafu wakwa karibu na Aboud Rogo halafu wakavuka mpaka wakafika Kibiti na baadae kufika Cabo del Gado nchini Msumbiji ambako wamekuwa wengi na kupata nguvu pengine kuliko Alshabaab na Alqaeda.

1.Ikiwa picha ni hiyo,kiongozi wao ni nani na wapi ndio makao yao makuu wanakopeleka taarifa za utiifu na mafanikio ya mashambulio yao?

2.Wapi wanapata silaha na gharama za kuendesha harakati zao?

3.Eneo la Cabo ni misitu minene kama ya Kongo na mapango kama Afghanistan au ni tambarare na vichaka vya mikorosho vinavyofanana na maeneo ya Mtwara nchini Tanzania ?

4.Jeshi la Msumbiji limepata mafunzo wapi na silaha zao wanauziwa na nani kiasi kwamba hawafui dafu kwa vijana hao wa ISIS ambao baadhi ya watoa taarifa husema ni wahuni wanaotokana na vijana waliokosa ajira na wenye njaa.

5.Kwanini hao ISIS wanapouwa huwa hawapati upinzani kutoka kwa wanavijiji ambao kama hawana silaha za kijeshi basi wana silaha za jadi na watu wa makabila ya kimakonde ni maarufu kwa matumizi ya silaha za jadi wanapovamiwa.

6.Hao ISIS wa Msumbiji kama wapo hawaoni kwamba wanapoteza muda bure hilo lengo wanalohusishwa nalo eti kuanzisha dola ya kiislamu itakayokuwa na bendera ya rangi nyeusi,kwa sababu wenzao wote kuanzia Iraq,Ufaransa,Mali mpaka Somalia hakuna walipofanikiwa.Ni wapambanaji gani wajinga hao watakaokuwa kila siku hawabadili mbinu za kivita hata wanaposhindwa.

7. Kama ni kikundi cha waislamu kweli mbona wanafanya kinyume na Uislamu na tofauti sana na wale wanaodaiwa ni wenzao wa nchi nyengine. Mbona wao wamekuwa ovyo sana katika mapambano yao wanauwa tu hata hawajachokozwa.Wana tatizo gani na ndugu zao na majirani zao.

Maswali yote hayo hapo juu majibu yake yanaweza kutoa majibu kuwa kikundi cha ISIS cha Msumbiji na yale yanayotajwa kutendwa nao ni vitu hewa na haviingii akilini kwa watu wenye nia thabiti ya kujua ukiondoa wale wanaoshabikia kwa ujinga na chuki zao.

View attachment 1624211
Chama cha CCM nao wanasema Tz hakuna anayetishiwa usalama wa maisha yake miongoni mwa washindani wao, nawe unasema Msumbiji hakuna magaidi wa ISIS,ukweli hupotoshwa ila unaonekana wazi
 
Sasa mbona hamtuambii ni kina nani hao ?

Mimi kwa habari zilizo nifikia ni kuwa mauaji ya kule ni masuala ya ardhi, ya watu fulani kuingia sehemu ya wengine, ndiyo maana Jeshi la Tanzania limepelekwa kule kuwaondoa raia wa Tanzania na kuwahamisha katika hicho kijiji ambacho wamevamiwa na watu wa nchi husika. Kadhalika ni kweli watu wamepigwa marufuku kutembea usiku na mengine mfano wa hayo na kule watu imekuwa ngumu kuondoka kijiji kile sababu walishazaliana na kuwekeza shughuli zao. Wahusika wanalalama ya kuwa Jeshi la Tanzania linawatoa kule bila kuwaandalia mazingira ya kuka kuishi makazi mapya.
Si kweli.. suala la ardhi sio sababu. Kwahiyo unataka kusema wamakonde ndio wanamiliki mpaka bandari huko ambayo hao magaidi walishawahi kuiteka na ikawa chini yao?

Kama ni ardhi mbona wengine wengi tu wanauliwa ambao sio wa Tanzania? Kama tatizo ardhi ambayo ipo Msumbiji kwanini waje kuua mpaka huku kwetu na kusema wanataka kusimamisha dola yao??
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kote duniani wapi !. Wapi unapajuwa ndio kwao hao ISIS .Kila shirika na taasisi zina anuwani yao.Hawa ISIS mbona anuwani yao ni kwenye vinywa na majarida tu.Na pamoja na kwamba wanatajwa ni waislamu lakini hawana ndugu wanayejuwana nao.Ndugu zao wenye uwezo wa kuwafafanua wamefanya nini ni akina Macron,Penagon na wengine huko Ulaya.
Sikatai kwamba ISIS ni zao la US na genge lake Kama saudia, France, nk lakini hao ISIS Wana matawi yao ambayo duniani kote hawajiiti Tena ISIS Bali Boko Haram, alshabab ya msumbiji na kule Indonesia na Philippines Wana jina lao pia..
Lakini pia naomba nifahamishe Hili ISIS ya Iraq na Syria ni ile ambayo ipo kwa malengo ya kuzipinga serikali za kishiite za Iraq na Syria hasa baada ya kukua kwa influence ya Iran hususan katika nyanja za kijeshi na kiuchumi katika nchi tajwa
 
Hao vyombo vya usalama wakiona maneno yako haya watakwambia wewe ni mbea tu kwani huna muda wa kutafakari anachoongelea mtu. Wapi nimewahi kuwatetea.Mimi nasema hawapo.Kama ni mauwaji watafutwe watu wengine wapewe majina mengine sio kuwahusisha na uislamu.

kama hawapo

hao wanaochinja kuanzia nyuma ya shingo na kutamka allah akbar ni akina nani.?

kwa nini
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom