Msumbiji hakuna ISIS, ni usanii na dhulma. Ukifuatana nami utajua

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
Habari za ISIS na mauwaji nchini Msumbiji zimesambaa sana na zimeanza kujadiliwa mpaka Umoja wa Mataifa.Bila kujali ukubwa wa taarifa hizo na umbali zilikofika tujaribu kuwa watulivu ili tujadiliane na tufikie pazuri kuepusha madhara zaidi.

Waislamu tuna maelekezo tunapofikiwa na taarifa ya jambo kabla hatujaanza kuchukua hatua za kushughulikia taarifa hizo
{ {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ} } [الحجرات 6]
Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari yoyote msimkubalie tu, bali pelelezeni kwanza, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda}

Kutokana na ukubwa wa habari,madhara yanayotokea na zaidi yale yatakayofuatia ni muhimu kujadiliana kwa undani kuona kasoro ya hoja ya kuwepo kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kinachosemekana kinauwa watu hovyo na kuwazidi nguvu majeshi ya nchi hiyo na pia wamewahi hata kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kuuwa watu.

Hoja zangu za kufanya upembuzi zinaweza kuwa nyingi na ndefu lakini kwa ufupi tu ni kuwa kikundi hicho kinasemekana ni cha waislamu wenye msimamo mkali na kimekula kiapo kuwa chini ya ISIS wale tuliowahi kuwasikia nchini Iraq na maeneo mengi ya Mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Kwa hivyo hawa ISIS wa Msumbiji ni kama tawi la ISIS ya kimataifa. Na kwa huku kusini mwa Afrika walianzia kuwa Alshabab halafu wakwa karibu na Aboud Rogo halafu wakavuka mpaka wakafika Kibiti na baadae kufika Cabo del Gado nchini Msumbiji ambako wamekuwa wengi na kupata nguvu pengine kuliko Alshabaab na Alqaeda.

1.Ikiwa picha ni hiyo,kiongozi wao ni nani na wapi ndio makao yao makuu wanakopeleka taarifa za utiifu na mafanikio ya mashambulio yao?

2.Wapi wanapata silaha na gharama za kuendesha harakati zao?

3.Eneo la Cabo ni misitu minene kama ya Kongo na mapango kama Afghanistan au ni tambarare na vichaka vya mikorosho vinavyofanana na maeneo ya Mtwara nchini Tanzania ?

4.Jeshi la Msumbiji limepata mafunzo wapi na silaha zao wanauziwa na nani kiasi kwamba hawafui dafu kwa vijana hao wa ISIS ambao baadhi ya watoa taarifa husema ni wahuni wanaotokana na vijana waliokosa ajira na wenye njaa.

5.Kwanini hao ISIS wanapouwa huwa hawapati upinzani kutoka kwa wanavijiji ambao kama hawana silaha za kijeshi basi wana silaha za jadi na watu wa makabila ya kimakonde ni maarufu kwa matumizi ya silaha za jadi wanapovamiwa.

6.Hao ISIS wa Msumbiji kama wapo hawaoni kwamba wanapoteza muda bure hilo lengo wanalohusishwa nalo eti kuanzisha dola ya kiislamu itakayokuwa na bendera ya rangi nyeusi,kwa sababu wenzao wote kuanzia Iraq,Ufaransa,Mali mpaka Somalia hakuna walipofanikiwa.Ni wapambanaji gani wajinga hao watakaokuwa kila siku hawabadili mbinu za kivita hata wanaposhindwa.

7. Kama ni kikundi cha waislamu kweli mbona wanafanya kinyume na Uislamu na tofauti sana na wale wanaodaiwa ni wenzao wa nchi nyengine. Mbona wao wamekuwa ovyo sana katika mapambano yao wanauwa tu hata hawajachokozwa.Wana tatizo gani na ndugu zao na majirani zao.

Maswali yote hayo hapo juu majibu yake yanaweza kutoa majibu kuwa kikundi cha ISIS cha Msumbiji na yale yanayotajwa kutendwa nao ni vitu hewa na haviingii akilini kwa watu wenye nia thabiti ya kujua ukiondoa wale wanaoshabikia kwa ujinga na chuki zao.

1605095496416.png
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,667
2,000
Maswali yote hayo hapo juu majibu yake yanaweza kutoa majibu kuwa kikundi cha ISIS cha Msumbiji na yale yanayotajwa kutendwa nao ni vitu hewa na haviingii akilini kwa watu wenye nia thabiti ya kujua ukiondoa wale wanaoshabikia kwa ujinga na chuki zao.
Nilidhani umekuja na data kuonyesha kwamba hakuna ISIS huko, kumbe umekuja na maswali ili kwamba wengine wakuhakikishie kuwa ni vinginevyo
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
Nilidhani umekuja na data kuonyesha kwamba hakuna ISIS huko, kumbe umekuja na maswali ili kwamba wengine wakuhakikishie kuwa ni vinginevyo
Unaniuliza data mimi.Hebu waulize wale wanaosema wapo wakupe hizo data.Mbona ni habari za viroja viroja tu.Mfano hao ISIS ni wangapi na jeshi la Msumbiji ni wangapi.
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,667
2,000
Unaniuliza data mimi.Hebu waulize wale wanaosema wapo wakupe hizo data.Mbona ni habari za viroja viroja tu.Mfano hao ISIS ni wangapi na jeshi la Msumbiji ni wangapi.
Basi title yako haikutakiwa kuwa hivyo, maana ulivyoiweka ni kama vile unaleta habari, kumbe unatafuta habari! Pole mkuu, ila washauri waumini wako wajikite katika mambo ya kiroho zaidi, kuliko kupigania dola
 

Zeus1

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
4,640
2,000
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
ISIS wanasema wao ndio wahusika

halafu nyumbu1 alinayejificha nyuma ya keyboard anakanusha..

kwani wewe ndiye msemaji wa ISIS tawi la Del Carbo.!?
Basi title yako haikutakiwa kuwa hivyo, maana ulivyoiweka ni kama vile unaleta habari, kumbe unatafuta habari! Pole mkuu, ila washauri waumini wako wajikite katika mambo ya kiroho zaidi, kuliko kupigania dola
Hujui kusoma vichwa vya habari sijui umeishia darasa la ngapi.Nimekwambia fuatana nami.Ule ni muhtasari tu.Endelea kufuatilia.
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
ISIS wanasema wao ndio wahusika

halafu nyumbu1 alinayejificha nyuma ya keyboard anakanusha..

kwani wewe ndiye msemaji wa ISIS tawi la Del Carbo.!?
Ukisema wao wamesema. ni wapi walisema?.Lete link ya website yao au tupe frequency za redio yao ili tusikilize.
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
Mkuu hakuna upembuzi wowote wa maana hapo.

Yani hamna kitu.
Jaribu kuwa na kichwa cha kiutu na uwe na subra.Huu ni mjadala na tunajifunza kwa mtindo wa mtaala wa kizungu sio huu mtaala huu wetu majibu yote mezani. Mtaala wa wakubwa mwalimu hata akiwa na majibu hakupi kwa kijiko.

Kuonesha kuwa kichwani wewe ni mtupu kabisa hujaweza hata kuleta shaka au kujibu swali lolote unaloona wewe una jibu sahihi.Umeishia kulaumu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom