Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Mkuu mimi nilishuhudia kijana wa jirani yangu
alichanganyikiwa akawa anapiga kelele anasema kuna watu
wanamtoa utumbo,jirani akaniita tukasaidiana kumpeleka hospitali
tulipomfikisha amana wakamchech wakasema tumpeleke kitengo cha magonjwa
ya akili,walipompima wakasema anatumia madawa ya kulevya
wakampa dawa na alipopata ufahamu alikiri kuwa huwa anavuta bangi.
Huu ndo ushuhuda nilio ushuhudia.

Na wewe naomba uniwekee madhara ya biashara ya meno ya tembo
kwa binadamu,mbona inapigwa marufuku?
Haha mkuu ile kitu sio kila mtu inamkubali ni sawa tu na chakula kuna watu wakila sea foods wanavimba au kuku ,sasa kama kitu hukiwezi unalazimisha nini ?? Acha wenye vichwa vyao wavitumie ,hilo la tembo aisee sijui ila kuna makatibu wa vyama wanahusishwa nadhani ingekua vyema ukawaulize wao kwanini wanaona hiyo biashara haina tatizo
 
Mkuu na mimi nina elimu ya hapa na pale
Hebu kwa faida ya wenzangu kama Msukuma naomba unitajie madhara ya bangi ??
Hukumsikia Dr Kigwangala? Azam TV. Ho ho ho au subiri kipindi kitakachoandaliwa na Nape TBC Kama mlivyoshabikia.
 
TCC na TBL wanafahamu madhara ya sigara na pombe lakini bado wanatengeza na kutuuzia tena kwa bei ghali ; isitoshe kuna maneno yenye onyo kama vile 'Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako na mengine Unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako' respectively kwa nini bhangi ndo izuiliwe?
Mbona mataifa makubwa yameruhusu bangi kwani wao hafahamu madhara yake?
Bunge lialalishe bangi na watu tuvute kwa raha tena bila kujificha!!
Ivi madhara yapo kwenye ule moshi au kwenye content iliyoko kwenye mmea husika?
 
Mb
Asifiaye mvua jua imemnyea.Baadhi ya wah.Wabunge wapimwe akili.Inawezekana baadhi yao matendo wanayotenda na kuyashabikia wao ni sehemu ya tatizo.
mbona wabunge wasomi maprofesa ndiyo wezi wakubwa watu wa Michango kwani huvuta bangi kabla ya kupanga dili la kuiba pesa? Kuwa na Akili za ajabu si lazima uvute bangi wapo watu wenye matendo ya ajabu hawavuti Bangi wala kutafuna mirungi.
 
Hukumsikia Dr Kigwangala? Azam TV. Ho ho ho au subiri kipindi kitakachoandaliwa na Nape TBC Kama mlivyoshabikia.
Sijakuelewa Mkuu ,kasema nini Kigwangala kuhusu bangi au ?? Nilivyoshabikia nini ??
 
Hao ndio wabunge Lumumba. Bangi na mirungi anaipenda yeye, lakini anasingizia wengine.
 
Haha umenitajia Glaucoma nikakumbuka Movie ya due date ,Anyway sasa hizo side effects za bangi linganisha na side effects za quinine, sigara,Cocacola, nk ipi ina afadhali ??
Sigara na Pombe vina athari kubwa kuliko bangi kwanza watumiaji wapo wengi kulinganisha na watumiaji wa bangi.
 
Dr Kigwangala Alimjibu Msukuma bungeni kuhusu madhara ya bangi na mirungi. Azam TV ilikuwa live
 
Dokta Silaa alipogusia gongo kufanyiwa utafiti na kuhalalishwa matusi yalivuma toka kila kona ya Tanzania.......ngoja tuone kwa Msukuma
 
Mkuu na mimi nina elimu ya hapa na pale
Hebu kwa faida ya wenzangu kama Msukuma naomba unitajie madhara ya bangi ??
unabishana na mtu ambaye huwa anasikia tu kuwa bangi ni mbaya lakini sigara na pombe ni nzuri.
 
Hao watakuwa wamechanganya na madawa mengine ya kulevya. Pia bangi inahitaji usiwe na stress...ule vizuri, chakula kisiwe cha mawazo.

Usiniulize nimejuaje....
nasikia bangi inaleta sana appetite mkuu?
 
Msukuma anawakilisha hoja za jimbo lake... pamoja na kwamba simpendi, lakini kwa uzoefu bangi siyo mbaya kihivyo. Mirungi ndiyo kabisaa
 
huyo jamaa inaonekana mibange ndiyo biashara yake. Wavuta bangi siyo wasemaji kivile. Wavutaji ni wazee wa peace and love!
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Geita Vijijini"Msukuma, amesema haoni sababu ya Serikali kuzuia bangi na mirungi kuwa zao la biashara maana haoni madhara yake.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema wasukuma wakivuta bangi wanalima zaidi na inahitaji uchunguzi ili kuhalalisha mimea hiyo kuwa zao la biashara.
Wananchi wameaka uchaguzi ujao ATAISOMA namba
 
Back
Top Bottom