Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Hao watakuwa wamechanganya na madawa mengine ya kulevya. Pia bangi inahitaji usiwe na stress...ule vizuri, chakula kisiwe cha mawazo.

Usiniulize nimejuaje....
Pamoja na majibu mazuri ya muheshimiwa waziri mimi kama spika nafunga huu mjadala hakuna swali la nyongeza
 
Nina uhakika maana familia yangu na familia rafiki ni waadhirika wa haya majani.
Aisee basi hao hawali ganja aisee ,sijui wanavuta nini ,mimi kuna familia moja naijua yaani sio baba,mama,watoto wote watumiaji ila hamna kichaa ,mmoja ni mwanasheria,mwingine ni Daktari ,mwingine ni physcologist pata picha unakutana na mwana saikolojia ni mla ganja
 
1454345609114.jpg

Wana mapinduzi wakistua kidogo ile roho inapenda. Msukuma ameona faida za Bhangi.
Tibaigana akisikia hili atafurahi kweli.
 
Wako watu wengi na heshima zao wanatumia huu mmea,na bado wana-perform poa kwenye kazi zao. Fika night clubs,makambi ya mandata,utashangaa wanaotumia. Fuata maneno yao,si matendo
 
Inaonekana yeye ni mvutaji mzuri sana wa majani haya yanayopingwa sana.
 
Hao watakuwa wamechanganya na madawa mengine ya kulevya. Pia bangi inahitaji usiwe na stress...ule vizuri, chakula kisiwe cha mawazo.

Usiniulize nimejuaje....

'asikuulize umejuaje' hahahaa nimeipenda iyo mama. Akili kumkichwa, ajiongeze eeh? lol
 
Katika hali isiyo ya kawaida mbunge wa geita vijijini"Msukuma,amesema haoni sababu ya serekali kuzuia bangi na mirungi kuwa zao la biashara maana haoni madhara yake.
Ameenda mbali zaidi kwa kusema wasukuma wakivuta bangi wanalima zaidi na inahitaji uchunguzi ili kuhalalisha mimea hiyo kuwa ya biadhara.
Bora katoa wazo ili kodi iongezeke
 
Huyu msukuma huwa haongei Mara kwa Mara ila siku akiongea lazima achafue hali ya hewa
 
TCC na TBL wanafahamu madhara ya sigara na pombe lakini bado wanatengeza na kutuuzia tena kwa bei ghali ; isitoshe kuna maneno yenye onyo kama vile 'Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako na mengine Unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako' respectively kwa nini bhangi ndo izuiliwe?
Mbona mataifa makubwa yameruhusu bangi kwani wao hafahamu madhara yake?
Bunge lialalishe bangi na watu tuvute kwa raha tena bila kujificha!!
 
Therapeutic value ya mirungi na bangi ipoje dhid ya pombe. Infact ni kwamba pombe ni dawa 'drug' kuliko bangi na mirungi
 
Katika kile kinachoonekana kukurupuka na kutojielewa leo mbunge musukuma kasheku ameomba serikali ihalalishe matumizi ya bangi ili iweze kuongeza pato la serikali. Hii inaonesha ni aina gani ya wabunge tulionao katika awamu hii. Naomba serikali ipige marufuku wabunge wa namna hii.
Licha ya bangi, Gongo na miring Kupigwa marufuku takwimu za watumiaji hakijawahi kushuka tokea 1961 wavuta bangi wapo wengi sana hata baadhi ya wabunge na viongozi wanavuta bangi kwa wingi sana, hivyo hata bangi ikiruhusiwa hawatavuta wote Kama ilivyokuwa sigara hawavuti wote hata gongo hawanywi watu wengi, huyo Mbunge kaangalia takwimu za watumiaji kagundua kuwa watumiaji hayapungui licha ya Sheria kukataza kuvuta bangi.
 
Back
Top Bottom