Ila Kiukweli bange Ina madhara na inaleta ht uchizi kwa wengine,na inakufanya unakuwa kibri,au bwege kwa wengine, au mwingine akivuta anapenda kuchekacheka ht kwa jambo la kipuuzi, mi nilikuwa navuta wakati nna 25yrs, ,,kiukweli haifai hata kidogo, ila kuna wengine wakivuta inawachukua poa kabisa,,,,,mi nimevuta katika Mapito ya uvulana, nna ushaidi haifai ht kidogo,,,,,,faida zake ni chache kuliko madhara yake, NA MIRUNGI PIA INALETA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA SEVENTY PERCENT,,,,
Wewe hauko peke yako,tatizo lenu akili zenu zimelalia kwenye uvutaji tu wa bangi.Wengi wanaopinga kuhalalishwa kawa bangi humu wamekazana kuzungumzia uvutaji tu,hii inatokana na ukosefu wa uelewa sahihi wa matumizi ya bangi na historia ya matumizi ya bangi bila kusahau sababu halisi iliyofanya bangi kuharamishwa.
Watu wengi wanadhani bangi imeharamishwa kutokana na madhara yanayotokana na uvutaji wake,hapa ndipo watu wanapokosa elimu sahihi.Fuatilia marijuana act ya mwaka 1937 iliyoanzishwa na serikali ya marekani na baadaye kuwa enforced UNO kama sheria ili itumike duniani kote kuharamisha bangi.Sheria ya kuharamisha bangi Tanzania haijatungwa na serikali ya Tanzania,Tanzania tumelazimishwa kuifuata tu.Pia wengi hawajui hata hiyo sheria inasemaje.
Nikupe mfano tu:Salimia ni dawa inayotumika kuchua misuli ili kupunguza maumivu,na imeandikwa 'for external use only',ukinywa salimia utakufa.Pia kisu hutumika kukatia matunda na vitu vingine,lakini ukimchoma mwenzako kisu tumboni waweza kumwua,kazi ya kisu si kuua.Mpaka hapo utakuwa umeelewa kwamba uharamu wa kitu hutegemea matumizi yake.
Sasa tunakuja kwenye matumizi sahihi na yenye faida ya bangi:
1.Bangi hutumika kutengenezea kamba ngumu zaidi ya katani,zilitumika kipindi cha zamani kwenye majahazi.Ulikuwa unajua hili?
2.Bangi ilitumika kutengenezea karatasi zenye ubora kuliko hizi za sasa.Ulikuwa unajua hili?
3.Bangi ilitumika kutengeneza bodi ngumu za magari na hata kuta za nyumba.Ulikuwa unajua hili?
4.Mchakato wa bangi unaweza kutengenezea/kuzalisha methanol na gesi ya kupikia.Ulikuwa unajua hili?
5.Bangi inarutubisha ardhi iliyochoka pale inapopandwa.Ulikuwa unajua hili?
6.Mafuta ya mbegu za bangi hutumika kama kipodozi cha asili cha ngozi na kuikinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua.Ulikuwa unajua hili?
Sasa kuna matumizi mawili ambayo ndiyo yamefanya bangi iharamishwe.Matumizi haya ndiyo yanaifanya bangi iitwe mmea mtakatifu.
1.Bangi inaweza kuchakatwa na kutengeneza dawa ya cancer/saratani na magonjwa lukuki kama mchangia mmoja alivyobainisha humu.Kama ulikuwa hujui,hii hii sigara/tumbaku ambayo imehalalishwa,wakati inaposababisha madhara kwenye mapafu bangi inaweza kurudisha mapafu katika hali yake ya kawaida.Pia kama ulikuwa hujui,pale Ocean Road CI,kuna dawa za kuzuia kichefuchefu na kupunguza/kutuliza maumivu kwa wagonjwa wa cancer,dawa hizi zimetengenezwa kwa kutumia bangi,wanakuua kwa chemo na mionzi lakini wanakutuliza kwa bangi.Ulikuwa unajua hili?Hata mimi naweza kutengeneza dawa ya cancer kwa kutumia cannabis/bangi.Haya mambo sio ya kufikirika,ni uelewa tu,wengi hatuna uelewa ndio maana tunapinga hovyo.Soma/uliza utajua tu.
2.Ekari moja ya bangi huzalisha lita zaidi ya 1500 za diesel.Diesel inayotokana na bangi ina faida nyingi zaidi ya petroleum diesel.Hebu fikiria jinsi ambavyo tungeitumia bangi kuzalisha umeme na kuendesha mashine kubwa viwandani.Hatuna uelewa ndio maana tunapata shida.Hata mimi naweza kukutengezea cannabis biodisel na ukatumia kwenye generator yako.Jambo hili si la kufikirika,ni uelewa tu,ndio maana tunasema someni vitabu,na education is power lakini watu wanadharau na kupinga hovyo.Misaafu inasema,"watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".
Engine za kwanza kabisa kutengenezwa na Henry Ford na Rudolf Diesel miaka ya 1890 ziliendeshwa kwa mafuta ya diesel yaliyotokana na bangi/cannabis/hemp.Soma/uliza utajua tu.
Sasa matumizi haya mawili ndio mwiba kwa wafanyabiashara wakubwa wa kimarekani ambao ndio walikuwa wameshikilia serikali kipindi kile cha miaka kuanzia 1910.Kina Rockefeller,Morgan,Carnegie na wengine wakalazimisha kuanzishwa kwa sheria hiyo ili kudhibiti mass production ya cannabis.
Ukitaka kujua kama kweli bangi inazalisha diesel kwa wingi,usipinge,badala yake usome/uulize.Ukitaka kujua kama kweli bangi inatibu cancer,usipinge,badala yake usome/uulize.
Huyu mbunge aliyeanzisha hoja hii yuko sahihi kabisa,lakini ameanzisha hoja hii wakati bado uelewa wake kuhusu bangi ni mdogo.Kama ningekuwa mimi basi watu wengi ule ndio ungekuwa muda wao kuelewa ukweli uliojificha kuhusu bangi.
Fahamu kwamba uhalali na uharamu wa kitu chochote kile hutegemea na matumizi yake.Natoa rai kwa wote mpende kosoma vitabu na vyanzo vingine ili tuondokane na ujinga na ushabiki usio na faida.