"Msukule" wa Mapenzi...

Sina cha kuongeza ni ugonjwa huu omba usikukute unakataa dawa nyingi tu, wakati mwingine hupati dawa kabisa

...lol...Elia kila mara nikiirudia hii post yako nacheka,....!

Mbu we acha tu, saa nyingine akipiga namsikiliza namjibu tu ndio ndio mradi tu aridhike kwani sitaki kuanzisha uadui sasa binti yangu ameshakua mkubwa inaweza kumuathiri, na akiamua kumchukua sina pa kwenda kupinga kwani umri unaruhusu basi ndio hapo anapopatia kwa sababu anajua nampenda sana mtoto wangu and she is the only one i have sina mtoto mwingine masikini mie ndio ukimjibu hovyo tu anaanza naenda kumchukua nikae nae mwenyewe so inabidi nakua tu mpole, na hivi hayumo moyoni mwangu basi akishamaliza maongezi yake na mimi namsahau hapo hapo,

Halafu cha ajabu mtoto anakaa boarding ila huku mkoani ninakoishi sasa kila baada ya siku tatu simu ushaenda kumuona mtoto? jamani huyo mtoto anaonwa kila siku? Kaazi kweli kweli wandugu ila ukishakua mtu mzima kidogo ina unafuu

...dahhh, Maty sasa huo ni usumbufu usiokuwa na lazima. Yaani 'msukule' wewe anakukeep busy uwazie jinsi ya kumjibu routine ya simu kila baada ya siku tatu? ama hakutakii mema huyo. Ni aheri muda mwingine ku ignore hizo simu na kupokea wiki kwa wiki.

LOL, Mr Rocky you must have been there,...inputs zako zinaelezea hali halisi. Halafu kitu kibaya ni kwamba, jinsi anavyokuudhi nawe kuzidi kumchukia, ndivyo anavyoanza kukuganda tena kichwani....Pheewwww, what a miserable life!
Mbu hapo anakuwa kashakujua na you know anakujua udhaifu wako na wewe ulivyo so anatake advantage ya wewe kuwa vile ili azidi kukutumia na with time na unavyozidi kukasirika anajua tuu hutoacha kupokea simu zake wala sms zake hutoacha kuzijibu

...hhhahhaaaa hha, MR Rocky bana, ukweli unauma bana...! LOL...uloyaongea ni kweli tupu, angalia kina Maty, Nyamayao, Bebiii, Mbimbinho et al wanavyougulia!
 
Tulizo Mkuu kama kweli you don’t know Mapenzi ni nini ni kwamba aidha you are in deep expected trouble OR ndio moja ya wale exceptions walojaliwa (thou rare) never to fall in love….

AshaDii.. I have no idea kwanini niko sceptical na hii issue nzima ya mapenzi ambayo inasumbua vichwa wa watu. Na sielewi kwanini despite the fact that sifanyi vile wengi wanafanya ku-prove wanajua kupendana mimi, mwenza na familia yangu tunaaminiana kiasi cha kutosha kusolve bump ndogo ndogo na ku-excel smoothly na life..labda hii ndiyo inanipa kichwa kuwa hakuna mapenzi ila kuna maisha.. Ni vile wewe unaamua kuishi na ku-balance equation yako na mwenza + family. Na ukiweza hili uta-feel uchungu wa wenzako kama wa kwako..

Anyway..back to the sired.. Naamini issue na impact za msukule wa mapenzi zote ziko ndani ya uwezo wetu hadi pale tunapoziachia na kuwa juu ya uwezo wetu..ikifika wakati huu..yaani ni vigumu kuzi-control..hasa zikihusu wale malaika yaani watoto..au wazazi..
 
Asante MBU kwa mada nzuri...

Bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kugeuzwa “MSUKULE“ wa mapenzi kwa hiyo siwezi kuungana na walioguswa kusema ni kwa kiasi gani inaboa.

Nnachoweza kuwaambia ni kwamba wale ambao bado wamekamatwa amueni kwamba hamtaki kuendeshwa tena and take charge of your own life.Fikiria huyo mwenzako anapokupaisha roho kiasi hicho we unapata nini?!Surely hamna faida yoyote wa upande wako...na ukifanya mchezo hata mahusiano yako mapya (kama unayo) yanaweza kuyumbishwa au hata kuvunjika kwaajili ya mtu ambae huna deni lolote kwake.

Ukweli ni kwamba mpaka mtu akupelekeshe na kukusumbua na simu za ajabu ajabu iwe usiku au mchana anakua ameshakusoma na kujua kwamba huna ujanja kwake. Anakuchukulia kwamba wewe ni DHAIFU mbele yake...sasa amua kwamba hutaki tena na ubadilishe mtazamo alio nao juu yako.

Kama hamna mtoto ni kiasi tu cha kumkatia mawasiliano once and for all...unamwambia kabisa akae mbali na wewe akiendelea kusumbua unaweza block namba yake...au akikupigia na nyingine unakata tu bila hata kumuuliza habari.Kama mnashea mtoto mnapanga namna ya yeye kumuona/wewe kwenda kumwangalia....na ratiba inafuatwa kuendana na makubaliano...zaidi ya hapo hata akija kwako kama sio muda/siku mlizokubaliana unamwambia una mambo mengine na kumuaga.
Yote haya unatakiwa useme ukimaanisha...USIMUOMBE bali MUAGIZE unachotaka afanye/asifanye kwasababu ni maisha yako na wewe ndio mwamuzi!
 
...hhhahhaaaa hha, MR Rocky bana, ukweli unauma bana...! LOL...uloyaongea ni kweli tupu, angalia kina Maty, Nyamayao, Bebiii, Mbimbinho et al wanavyougulia!
[/QUOTE]

Mkuu kucontrol emotional ni ngumu na feelings za someone you love and just note that she is not just a past but someone ambaye mshaspend life together na love na mshashere mengi in your real life. So ni ngumu sana kucontrol mkuu na tatizo sio kuwa wewe ndio unayezianzisha ila kuna some forces behind zinafanya zitokee. So hapo unaona taabu zake na madhara yake usipokuwa makini zinaweza kukuangusha
 
AshaDii.. I have no idea kwanini niko sceptical na hii issue nzima ya mapenzi ambayo inasumbua vichwa wa watu. Na sielewi kwanini despite the fact that sifanyi vile wengi wanafanya ku-prove wanajua kupendana mimi, mwenza na familia yangu tunaaminiana kiasi cha kutosha kusolve bump ndogo ndogo na ku-excel smoothly na life..labda hii ndiyo inanipa kichwa kuwa hakuna mapenzi ila kuna maisha.. Ni vile wewe unaamua kuishi na ku-balance equation yako na mwenza + family. Na ukiweza hili uta-feel uchungu wa wenzako kama wa kwako..

Anyway..back to the sired.. Naamini issue na impact za msukule wa mapenzi zote ziko ndani ya uwezo wetu hadi pale tunapoziachia na kuwa juu ya uwezo wetu..ikifika wakati huu..yaani ni vigumu kuzi-control..hasa zikihusu wale malaika yaani watoto..au wazazi..

Dahhhh!!!!...Tulizo naomba somo juu ya hilo. Inaonyesha ni somo lenye akili sana. Mapenzi yana fit wapi kwenye Ndoa/Maisha? Kwa utambulisho huu nadhani nimegundua mtazamo pia wa maoni baina ya tuliokumbwa na broken hearts, na wale waliojaaliwa kuoana na childhood/sweethearts wao bila kupitia makasheshe ya 'kuzikwa kabla ya siku zako' kisha kuja kufanywa "Misukule!"
 
Friends with reason and hidden agenda always. Be careful sana mkuu maana we have friends but hatujui ndani ya mind zao wanawaza nini kwa ajili yetu au wanatuwazia nini kama ni mema au mabaya hatujui. Always hizo agenda zao za siri huwa wanazificha hawazionyeshi hata ukikutana nae umuulize what is in your mind hawezi kukupa jibu la nini anachokuwazia ila ndani mwake ana dirty mind. So be careful mkuu.

Ni kweli mkuu you never know with people..., lakini kuliko kuishi maisha ya kuogopa the inevitable rafiki atabaki kuwa rafiki yangu mpaka pale atakaponipa sababu ya mimi kufikiria vinginevyo... Mkuu kuna msemo mmoja ambao huwa ninakaa nao sana na kwa kuutegemea huu hujikuta kwamba ninaishi maisha ya amani na bila kulaumu...

"Tenda wema uende zako na usingoje kurudishiwa"..., kwahiyo chochote ninachofanya hakiji na Price Tag na kama nitalipwa wema kwa wema hio ni Bonus lakini sio kwamba nilitegemea wema..., kwahiyo kama huyo Ex atataka msaada tampa popote pale lakini within reason na hata siku akiniambia nikashindwa itabidi akubali kwamba nimeshindwa (na urafiki wetu utaendelea pale tu ambapo hata-abuse urafiki wetu).., na urafiki wetu utaendelea au kufa kutokana na actions zake (kama urafiki wetu utazidi mpaka kurudiana itakuwa kwamba sio sababu yeye ametaka bali na mimi nimependa....) "It Takes Two to Tango" na kama sitaki anavyofanya na yeye akaendelea huyo sasa atakuwa stalker...
 
Lizzy...inakera kwa kweli, mtu anafanya jitihada zote ili mradi mwingine akose amani. anabadili no za cm kila akikucal, msg za ajabu ndio ucseme, unajaribu kila njia kumuonyesha kwamba "it was" but bado tu..mpaka nimefikia kufikiria nictumie tena mobile.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
AshaDii.. I have no idea kwanini niko sceptical na hii issue nzima ya mapenzi ambayo inasumbua vichwa wa watu. Na sielewi kwanini despite the fact that sifanyi vile wengi wanafanya ku-prove wanajua kupendana mimi, mwenza na familia yangu tunaaminiana kiasi cha kutosha kusolve bump ndogo ndogo na ku-excel smoothly na life..labda hii ndiyo inanipa kichwa kuwa hakuna mapenzi ila kuna maisha.. Ni vile wewe unaamua kuishi na ku-balance equation yako na mwenza + family. Na ukiweza hili uta-feel uchungu wa wenzako kama wa kwako..

.

From the above mtazamo... ni dhahiri you have never fallen... Ila tu the way mnaishi na mwenza wako ndio the way most couples wanaishi.... as if having a certain understanding... a compromise... well fitted glove; with bumbs ndogo ndogo... I really wish ungekua umewahi pitia... It is a wonderful feeling as much as in most cases inaishia kuuma. Enways hongera kwa kukwepa hilo....

Anyway..back to the sired.. Naamini issue na impact za msukule wa mapenzi zote ziko ndani ya uwezo wetu hadi pale tunapoziachia na kuwa juu ya uwezo wetu..ikifika wakati huu..yaani ni vigumu kuzi-control..hasa zikihusu wale malaika yaani watoto..au wazazi..

Tulizo the above Blue... naongea from experience... iko ndani ya uwezo wetu pale akili ikitengamaa na uka realise kua una burutwa... otherwise, ni an on going tatizo ambalo mhusika linamtokea (kama ulivo comment your first post... ) bila hata yeye kujitambua... sasa kama hajitambui, ni vipi itakua ndani ya uwezo wake?? Ni vigumu kwa kweli, na kama akijitambua tu! Believe me you anageuka mbogo as if sio yule....
 
Ni kweli mkuu you never know with people..., lakini kuliko kuishi maisha ya kuogopa the inevitable rafiki atabaki kuwa rafiki yangu mpaka pale atakaponipa sababu ya mimi kufikiria vinginevyo... Mkuu kuna msemo mmoja ambao huwa ninakaa nao sana na kwa kuutegemea huu hujikuta kwamba ninaishi maisha ya amani na bila kulaumu...

"Tenda wema uende zako na usingoje kurudishiwa"..., kwahiyo chochote ninachofanya hakiji na Price Tag na kama nitalipwa wema kwa wema hio ni Bonus lakini sio kwamba nilitegemea wema..., kwahiyo kama huyo Ex atataka msaada tampa popote pale lakini within reason na hata siku akiniambia nikashindwa itabidi akubali kwamba nimeshindwa (na urafiki wetu utaendelea pale tu ambapo hata-abuse urafiki wetu).., na urafiki wetu utaendelea au kufa kutokana na actions zake (kama urafiki wetu utazidi mpaka kurudiana itakuwa kwamba sio sababu yeye ametaka bali na mimi nimependa....) "It Takes Two to Tango" na kama sitaki anavyofanya na yeye akaendelea huyo sasa atakuwa stalker...

Mkuu wanasema "never argue with a fool as u might turn out to be a fool than a fool himself". Ila wapi utakapojua kuwa unaargue na fools ni pale utakapojikuta ulishaingizwa kwenye mtego muda mrefu sana na umeshikwa bila mwenyewe kujua na ukashikika. Nakubali " tenda wema uende zako usingoje shukrani" but under what circumstance huo wema unaufanya na umetoka wapi mpaka uufanye huo wema. Maana unaweza jikuta kumbe ushaulipia sehem bila wewe kujijua.

Mkuu kumjua mtu undani wake ni issue sana na ni ngumu sana hasa kwa dunia ya leo maana hata wale expected friends wamegeuka kuwa balaa na wana miiba inayochoma kupita maelezo. Wana kila utu na ubinadamu na wana busara over mitume na manabii wa zamani ila ni wanafiki kuliko mbwa mwitu na sio rahisi kuona wala kutambua action zao. Wanajua kuact kuliko actor wa movie na wana kila sababu ya kuwa wasanii ila sio wasanii. Friends with reasons. So waliposema si kila king'aacho ni dhabahu hawakukosea na mkuu kujua kuwa someone anaabuse urafiki kati yako sometime ni ngumu sana na unaweza kujikuta umeingizwa kwenye mtego bila wewe mwenyewe kujua au ukiwa kabisa unajua.
 
Asante MBU kwa mada nzuri...

Bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kugeuzwa "MSUKULE" wa mapenzi kwa hiyo siwezi kuungana na walioguswa kusema ni kwa kiasi gani inaboa.

Nnachoweza kuwaambia ni kwamba wale ambao bado wamekamatwa amueni kwamba hamtaki kuendeshwa tena and take charge of your own life.Fikiria huyo mwenzako anapokupaisha roho kiasi hicho we unapata nini?!Surely hamna faida yoyote wa upande wako...na ukifanya mchezo hata mahusiano yako mapya (kama unayo) yanaweza kuyumbishwa au hata kuvunjika kwaajili ya mtu ambae huna deni lolote kwake.

Ukweli ni kwamba mpaka mtu akupelekeshe na kukusumbua na simu za ajabu ajabu iwe usiku au mchana anakua ameshakusoma na kujua kwamba huna ujanja kwake. Anakuchukulia kwamba wewe ni DHAIFU mbele yake...sasa amua kwamba hutaki tena na ubadilishe mtazamo alio nao juu yako.

Kama hamna mtoto ni kiasi tu cha kumkatia mawasiliano once and for all...unamwambia kabisa akae mbali na wewe akiendelea kusumbua unaweza block namba yake...au akikupigia na nyingine unakata tu bila hata kumuuliza habari.Kama mnashea mtoto mnapanga namna ya yeye kumuona/wewe kwenda kumwangalia....na ratiba inafuatwa kuendana na makubaliano...zaidi ya hapo hata akija kwako kama sio muda/siku mlizokubaliana unamwambia una mambo mengine na kumuaga.

Yote haya unatakiwa useme ukimaanisha...USIMUOMBE bali MUAGIZE unachotaka afanye/asifanye kwasababu ni maisha yako na wewe ndio mwamuzi!

Dahhh, Lizzy wewe ni kiboko. Sina hata la kusema, ahsante sana kwa mchango wako huu, naamini utawasaidia sana dada zako wengi humu ndani wanaougulia. Ila kuwkuwa experiences zinatofautiana kama Elia alivyosema hapa;

Sina cha kuongeza ni ugonjwa huu omba usikukute unakataa dawa nyingi tu, wakati mwingine hupati dawa kabisa

...kuna mijitu kwa makusudi kabisa inapindisha hizo sheria mlizokubaliana... Wewe hata uwe na msimamo kiasi gani, watavunja miiko tu.
  • chukulia 'kesi' ya Nyamayao na hizo unwanted Calls,
  • chukulia 'kesi' ya Maty na hizo Routine Calls za mtoto,...
  • chukulia 'kesi' ya Mbimbinho na 'the deal too tempting to refuse' la ex wake
... kwani unadhani tunapenda basi?...Mr Rocky anasema, jinsi unavyozidi kumchukia kwa kuvunja viapo vya makubaliano, Ex wako nae anautumia udhaifu wa kuchukizwa kwako kukuchokoza almuradi wewe kila siku/wiki/ mwezi una homework tu how to handle him/her... ndio ushafanywa msukule hivyo.
 
Dahhhh!!!!...Tulizo naomba somo juu ya hilo. Inaonyesha ni somo lenye akili sana. Mapenzi yana fit wapi kwenye Ndoa/Maisha? Kwa utambulisho huu nadhani nimegundua mtazamo pia wa maoni baina ya tuliokumbwa na broken hearts, na wale waliojaaliwa kuoana na childhood/sweetherts wao bila kupitia makasheshe ya 'kuzikwa kabla ya siku zako' kisha kuja kufanywa "Misukule!"

Mbu mimi nakubaliana na Tulizo katika hio ulo red bold.... ndoa nyingi saana zinaishi katika msingi huo, ila kikubwa nio kwamba woote katika there life time wesha wahi penda... au hata wao kupendana. Kwani ni dhahiri mkioana tu mapenzi yanakua moto moto saana mpaka hata mnafurahi... BUT with time, yanakuja majukumu, watoto na mambo mengi ndoa stress related mpaka mnakuja realise mliaga mapenzi siku nyiiingi na sasa imebaki tu maisha..... Na hata hao wanaoana childhood sweethearts.... mara nyingi hu face kitu inaitwa "Rut" mapema kuliko hata wa ukubwani.
 
Lizzy...inakera kwa kweli, mtu anafanya jitihada zote ili mradi mwingine akose amani. anabadili no za cm kila akikucal, msg za ajabu ndio ucseme, unajaribu kila njia kumuonyesha kwamba "it was" but bado tu..mpaka nimefikia kufikiria nictumie tena mobile.

Hahahhaha...Nyamayao kuacha kutumia simu itakua unajikomoa wewe na wale walio karibu na wewe kuliko hata huyo MHUSIKA.Na mawazo kama hayo ndo yanaonyesha kwamba ni kwa kiasi gani yeye anakuamulia jinsi ya kuishi...mood gani uwe nayo...siku ipi iwe nzuri kwako na ipi iwe mbaya n.k.

Cha muhimu ni wewe kumnyang‘anya hiyo nguvu aliyonayo juu yako....yani inabidi umwonyeshe you mean business..usicheke na kima usije ukaishia kuvuna mabua mwaya!
 
...Lizzy umemjibu vizuri sana Nyamayao...lol...kweli kabisa.
 
Mkuu wanasema "never argue with a fool as u might turn out to be a fool than a fool himself". Ila wapi utakapojua kuwa unaargue na fools ni pale utakapojikuta ulishaingizwa kwenye mtego muda mrefu sana na umeshikwa bila mwenyewe kujua na ukashikika. Nakubali " tenda wema uende zako usingoje shukrani" but under what circumstance huo wema unaufanya na umetoka wapi mpaka uufanye huo wema. Maana unaweza jikuta kumbe ushaulipia sehem bila wewe kujijua.
Mkuu so long as unafanya hicho kitu kwa mapenzi yako who cares!!??, Kama unafurahia kutoa huo msaada kwa moyo mmoja inaeffect gani (tatizo ni kama unayemsaidia hajui umuhimu wa ule msaada au anakuletea wewe karaha kama ndio hivyo basi hii ni case nyingine). Mkuu huo wema au msaada unaufanya kama binadamu kwa mtu ambae ulishamjua before na kama huo wema hautapelekea ndoa yako kuvunjika who cares?

Mkuu kumjua mtu undani wake ni issue sana na ni ngumu sana hasa kwa dunia ya leo maana hata wale expected friends wamegeuka kuwa balaa na wana miiba inayochoma kupita maelezo. Wana kila utu na ubinadamu na wana busara over mitume na manabii wa zamani ila ni wanafiki kuliko mbwa mwitu na sio rahisi kuona wala kutambua action zao. Wanajua kuact kuliko actor wa movie na wana kila sababu ya kuwa wasanii ila sio wasanii. Friends with reasons. So waliposema si kila king'aacho ni dhabahu hawakukosea na mkuu kujua kuwa someone anaabuse urafiki kati yako sometime ni ngumu sana na unaweza kujikuta umeingizwa kwenye mtego bila wewe mwenyewe kujua au ukiwa kabisa unajua.
Mkuu we cant stop making friends, being close na watu au kuwatendea watu wema sababu tunaogopa kwamba huenda wana lao jambo au watatuumiza baadae "Cherish the Moment" Rafiki yao leo sio lazima awe rafiki yako Kesho kutokana na circumstances..., kwahiyo cha maana ni kufanya lile jambo ambalo yako inakutuma kwamba ni kitu cha maana wala usifanye kitu kwa shinikizo..., sababu kama kweli huyo mtu ni rafiki yako hatakulazimisha ufanye jambo ambalo wewe hutaki kulifanya.
 
Dahhh, Lizzy wewe ni kiboko. Sina hata la kusema, ahsante sana kwa mchango wako huu, naamini utawasaidia sana dada zako wengi humu ndani wanaougulia. Ila kuwkuwa experiences zinatofautiana kama Elia alivyosema hapa;

...kuna mijitu kwa makusudi kabisa inapindisha hizo sheria mlizokubaliana... Wewe hata uwe na msimamo kiasi gani, watavunja miiko tu.
  • chukulia 'kesi' ya Nyamayao na hizo unwanted Calls,
  • chukulia 'kesi' ya Maty na hizo Routine Calls za mtoto,...
  • chukulia 'kesi' ya Mbimbinho na 'the deal too tempting to refuse' la ex wake
... kwani unadhani tunapenda basi?...Mr Rocky anasema, jinsi unavyozidi kumchukia kwa kuvunja viapo vya makubaliano, Ex wako nae anautumia udhaifu wa kuchukizwa kwako kukuchokoza almuradi wewe kila siku/wiki/ mwezi una homework tu how to handle him/her... ndio ushafanywa msukule hivyo.

Asante MBU!!

Kuhusu kesi za dada zangu hapa zinaweza kumalizika kirahisi tu wakiamua kwamba sasa wamechoka na hawataki tena kuendelea kufanywa/kuishi kama misukule.

MATY dearest ni kiasi cha wewe tu kufanya maamuzi na kumpa taarifa kwamba ni wakati gani utakua unamjulisha kuhusu hali ya mtoto!!Mtoto anasoma boarding hivyo humuoni kila siku...let say unapiga simu shuleni mara mbili/tatu kwa wiki kumjulia hali....sasa wewe fanya mara moja ya kumjulisha mzazi mwenzio hali ya mtoto.Unamwambia kabisa kwamba mimi ndio ntakaekutafuta nikujulishe anaendeleaje kila siku fulani...na iwapo litatokea tatizo siku tofauti na hii basi ntakujulisha kwahiyo wewe huna haja ya kunitafuta mimi.Ukiona kimya jua ni mzima na anaendelea vizuri.Ni maisha yako..ni muda wako...na ni simu yako amua wewe unataka kuvitumiaje vitu hivi.

Swala la yeye kukutisha kwamba sijui atamchukua usiruhusu ndo kiwe kifungo chako.Atakunyanyasa nacho sana mpaka mtoto akue utaishia kukondeana na kuishi kwa simanzi kama vile unafiwa kila siku.Hana sababu ya msingi kukunyang‘anya mtoto hivyo mwambie awe reasonable.
 
Dahhhh!!!!...Tulizo naomba somo juu ya hilo. Inaonyesha ni somo lenye akili sana. Mapenzi yana fit wapi kwenye Ndoa/Maisha? Kwa utambulisho huu nadhani nimegundua mtazamo pia wa maoni baina ya tuliokumbwa na broken hearts, na wale waliojaaliwa kuoana na childhood/sweetherts wao bila kupitia makasheshe ya 'kuzikwa kabla ya siku zako' kisha kuja kufanywa "Misukule!"

Mkuu ..mimi naamini mapenzi ni "theory" lakini maisha ni "practical" ..

Mapenzi yanaendana na principle ambazo jamii imezitengeneza..lakini maisha yanaendana na principle ambazo unatengeneza wewe mwenyewe.. Kama utaamua kuchukua baadhi ya theory nzuri za mapenzi na kuingiza kwenye maisha..basi unazifanya ziwe part n' parcel ya practical life ambayo jamii inaweza kukushangaa...

Naamini kuna baadhi ya misekule hiko positive..kwa mfano..(ambao najua kuna watu wameshafanya) una-decide kuingia katika Longterm relatioship na mwenza ambaye utamkubali akipata point 55% tu kati ya 100%. Utavumilia yote mabaya ambayo yamo katika zile 45%. Kama decision hii umefanya na ukaondoka nayo na mweza kwa miaka 10...yaani kila atakapo-demonstrate zile negative 45% utajiona lazima ukubali yaishe..uliyataka mwenyewe na uliamua iwe hivyo...lakini naamini jamii itakuchukulia wewe kama "super" msekule uliopewa libwata la hali ya juu,,hakuna mapenzi..mwanamke au mume ovyo kwanini unaendelea kuwa nae..Hapa naamini Theory ya mapenzi iliyowekwa na jamii imeshindwa kutambua ..it's a practical life that just needs to be fine tuned to be aligned with your custom made principle of "sweet and sour love"
 
Asante MBU kwa mada nzuri...

Bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kugeuzwa "MSUKULE" wa mapenzi kwa hiyo siwezi kuungana na walioguswa kusema ni kwa kiasi gani inaboa.

Nnachoweza kuwaambia ni kwamba wale ambao bado wamekamatwa amueni kwamba hamtaki kuendeshwa tena and take charge of your own life.Fikiria huyo mwenzako anapokupaisha roho kiasi hicho we unapata nini?!Surely hamna faida yoyote wa upande wako...na ukifanya mchezo hata mahusiano yako mapya (kama unayo) yanaweza kuyumbishwa au hata kuvunjika kwaajili ya mtu ambae huna deni lolote kwake.

Ukweli ni kwamba mpaka mtu akupelekeshe na kukusumbua na simu za ajabu ajabu iwe usiku au mchana anakua ameshakusoma na kujua kwamba huna ujanja kwake. Anakuchukulia kwamba wewe ni DHAIFU mbele yake...sasa amua kwamba hutaki tena na ubadilishe mtazamo alio nao juu yako.

Kama hamna mtoto ni kiasi tu cha kumkatia mawasiliano once and for all...unamwambia kabisa akae mbali na wewe akiendelea kusumbua unaweza block namba yake...au akikupigia na nyingine unakata tu bila hata kumuuliza habari.Kama mnashea mtoto mnapanga namna ya yeye kumuona/wewe kwenda kumwangalia....na ratiba inafuatwa kuendana na makubaliano...zaidi ya hapo hata akija kwako kama sio muda/siku mlizokubaliana unamwambia una mambo mengine na kumuaga.
Yote haya unatakiwa useme ukimaanisha...USIMUOMBE bali MUAGIZE unachotaka afanye/asifanye kwasababu ni maisha yako na wewe ndio mwamuzi!

Unafaa sana wewe! Very firm and not wishy-washy. Just the way I like it. Do they make your kind anymore? If no, can I clone you? Dayuuuuum.....coz that right there is just unadulterated truth.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hahahhaha...Nyamayao kuacha kutumia simu itakua unajikomoa wewe na wale walio karibu na wewe kuliko hata huyo MHUSIKA.Na mawazo kama hayo ndo yanaonyesha kwamba ni kwa kiasi gani yeye anakuamulia jinsi ya kuishi...mood gani uwe nayo...siku ipi iwe nzuri kwako na ipi iwe mbaya n.k.

Cha muhimu ni wewe kumnyang‘anya hiyo nguvu aliyonayo juu yako.
...yani inabidi umwonyeshe you mean business..usicheke na kima usije ukaishia kuvuna mabua mwaya!

how my dia?.....ucku mmelala call hiyo no huijui na mwenza coz ameshakuwa nawacwac bac mackio juu juu kutaka kujua kulikoni, ukikata baada ya kumtambua mhucka ni yule msumbufu bac mgogoro tayari, kucall mchana ni nadra sana, ucku wa kati ili mradi uharibifu tu...inachosha sana sana....kuna cku nilimcal nilipokuwa ofcn kuongelea juu ya hili, niliongea na ukorofi wangu wote mpaka mate yakanikauka nilijibiwa"nia yangu kuharibu, ulikuwa wangu utaendelea kuwa wangu"..ucku call kama kawaida, namhurumia mr anavyojickia kweli hata ingekuwa ni mie ananifanyia hivyo nicngemuamini na kasheshe lake analijua but sasa nitafanyaje ili aniamini kwamba huyu mtu ana nia ya kuniharibia na c vinginevyo?
 
Mkuu so long as unafanya hicho kitu kwa mapenzi yako who cares!!??, Kama unafurahia kutoa huo msaada kwa moyo mmoja inaeffect gani (tatizo ni kama unayemsaidia hajui umuhimu wa ule msaada au anakuletea wewe karaha kama ndio hivyo basi hii ni case nyingine). Mkuu huo wema au msaada unaufanya kama binadamu kwa mtu ambae ulishamjua before na kama huo wema hautapelekea ndoa yako kuvunjika who cares?

Mkuu we cant stop making friends, being close na watu au kuwatendea watu wema sababu tunaogopa kwamba huenda wana lao jambo au watatuumiza baadae "Cherish the Moment" Rafiki yao leo sio lazima awe rafiki yako Kesho kutokana na circumstances..., kwahiyo cha maana ni kufanya lile jambo ambalo yako inakutuma kwamba ni kitu cha maana wala usifanye kitu kwa shinikizo..., sababu kama kweli huyo mtu ni rafiki yako hatakulazimisha ufanye jambo ambalo wewe hutaki kulifanya.

Mkuu nakubaliana na wewe na huwezi kuacha kutoa msaada as long as huna unachopungukiwa unapotoa msaada huo. Ila la muhimu ni kuangalia ni wapi ambapo hujawa msukule hujawa mtumwa wa kutoa bila wewe kujitambua kuwa yule unayempa msada husika au anayekuja kukuomba msaada hajakufanya mtumwa wa kile unachokifanya yaani sauti yake imekuwa command na sio ombi. Yaani unajikuta unatekeleza bila hata kuuliza mara mbili mbili na wakati huo akili yako inakutuma kuwa unafanya jambo jema kumbe hujijui kuwa ushakuwa mtu wa ndio mzee. Na inafikia mkuu mambo mengine unafanya bila hata kumuulizamwenza wako ushauri kuw aje nitoe msaada huu. Na tena unajikuta unamkwepa mwenza wako kwa kuwa unajua kabis aukimuuliza mwenza wako utakutana na kizingiti.

Yeah mkuu nakubaliana na wewe we cant stop having friends and lover ones but under what circumstances tunakutana na hao tunaojidai wanatupenda na je katika makutano hayo hakukuwa na reasons za kutukutanisha. We cannot run from our own shadow but most of our friends of today is like shadow to us au tunaweza kusema ni kupe kwetu maana wametuganda kwa kuwa they know kuna benefits ambazo zinaendana na urafiki na na kuna mafanikio kuwa na mtu kama wewe kwenye list yake ya watu muhimu. Ila in case of knowing the true friends ni yupi wa kukaa nae na kushikamana nae hapo ni mtihani maana as i told u wengi wamevaa ngozi za kondoo ila ni mbwa mwitu wa hatari. Sijakataa we can not run away from the reality but we have a chance of preparing our own destiny and choose the right friends kutoka kwenye lundo la wanafiki
 
Back
Top Bottom