Msomaji alitolea uvivu 'Raia Mwema'

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
Niwapatie background kidogo: Gazeti la Jumatano la Raia mwema lilipata matangazo toka Hazina kuhusu masuala haya ya malipo ya walimu na hivyo likachapisha matangazo hayo na ndiyo msingi wa email hii:


Mwandishi bulogu yake: kijana; nyegerage, karibuni, hiki ndo kijiwe chetu sema utakachokusema!!

My Take:
Natumaini Raia Mwema watachapa hiyo barua.
 
Wewe uliyandika ujumbe huu hauna maana hata blogu yako sitembelei -- kama kutangaza blogu ni kwa hoja kama hizi na lugha hizi basi wabongo tuna safari ndefu za mafanikio nina uhakika wewe utakuwa ni mhitimu wa mlimani
 
Hoja anayo, tena hakuishia hapo tu ametoa pendekezo kwa Raia Mwema...hasa hilo la kupunguza bei kwa siku ambayo gazeti lina matangazo mengi.
 
Wewe uliyandika ujumbe huu hauna maana hata blogu yako sitembelei -- kama kutangaza blogu ni kwa hoja kama hizi na lugha hizi basi wabongo tuna safari ndefu za mafanikio nina uhakika wewe utakuwa ni mhitimu wa mlimani

Kuwa wee bwana mdogo, Kama kasoma mlimani so what?
 
Je ana hoja?
Msomaji ana haki ya kulalamika lakini uandishi wa namna hii pia haujakaa kiungwana, gazeti lingekuwa langu ningeweza kuifanyia marekebisho hoja ya mlalamikaji na ikasomeka vema na wazi kuwa ni malalamiko lakini ikiwa katika mtiririko ambao naweza kumwomba radhi akanielewa.

Inasikitisha kama alichoandika mhusika ndicho kilichotokea lakini bado sishangai kwani natambua safari bado ni ndefu, yani hata wao (Raia Mwema) yawezekana wakawa wanatumiwa bila wao kujua kuwa ndio hivyo wanatumiwa ama uchumi ndio unaochangia hali hii. Haya pia yanawezekana kuwa yaleyale kwa mwandishi wa barua pepe hii.

Mwanakijiji, katika Cheche unaandika kila unachotumiwa?
 

good question!
 
Jamaa anaonekana kuwa na machungu, lakini anajua Lula huyo ni nani? Si Mhariri wa gazeti hilo? I do get his/her concern lakini nachelea kuegemea upande wake ama upande wa Raia Mwema...
 
Wewe uliyandika ujumbe huu hauna maana hata blogu yako sitembelei -- kama kutangaza blogu ni kwa hoja kama hizi na lugha hizi basi wabongo tuna safari ndefu za mafanikio nina uhakika wewe utakuwa ni mhitimu wa mlimani

Hivi kama huna cha ku-comment si unaweza kukaa kimya tu?Na si lazima kuandika chochote ili ku-hit posts elfu kadhaa.It's the substance contained in x numbr of posts that matters most than the actual number of posts.
 

Umeleta hoja nzuri sana hapa.

Suala la kutumiwa bila wewe kujua, ni suala nyeti sana.
Unapewa ule kisha wakati wewe unakula watu wanakula kila kitu.

Nijiulizacho kila siku ni hiki.
Big Boss mwenyewe nyuma ya karibu kila mtu kutumiwa ni nani?

uzoefu wangu wa kuongea na viongozi wazito ndani ya serikali, ikiwa ni pamoja na mashushu wa muda mrefu sana unaonyesha kwamba kuna kundi la watu au wanao ogopwa siku zote na kila mtu.
Nijuavyo mimi watu hao si wana siasa wala wanajeshi ila ni watu waliojizazia nguvu nyingi za ajabu. Walitakalo kamwe halipingwi.

Huyo Big Boss wa kumfanya kila mtu ndani na nje ya CCM kijakazi ni nani au ni kina nani??
 

Mara nyingi watu wa aina hii utengenezwa na system yenyewe. Na ni kutokana na wengi waliopo kwenye madaraka, wafanyabiashara wakubwa kubwa kutopenda baadhi ya shughuli zao kujulikana. Hivyo uwapa kazi hawa mabig boss. Baada ya muda mabig boss hawa huwa wanajua mengi na hasa udhaifu wa kila aliye mtumia.

Katika hatua hii ndio uaanza kuogopwa, na system yenyewe na waliokuwa nje ya system. Ni katika hatua hii ambapo uweza hata kutoa ushauri katika system, na ni katika hatua hii ambapo hata vyombo vya dola uwa vijakazi wao.
 
Tusiojua kusoma shida kweli, hata magazeti hatununui!!!!! kwani hayo matangazo yanahusu nini???

hamna kwayo ujumbe kwa wanainji???
Yana tofauti sana na matokeo ya mitihani ambayo huwa yanatolewa ktk magazeti mengi tu??


Huyo mlalamikaji, ana hoja anapozungumzia punguzo la bei (japo angekuwa sahihi zaidi aongelee kuongezwa karatasi kwa ajili ya hayo matangazo [ya biashara] ili makala na taarifa ziendelee kuwa covered na zile kurasa za kawaida). Hata hivyo yaonekana malalamiko yake yamevuka mipaka ya kutomtilia mtu mashaka kuwa ana lake jambo!!!!

Kama alivyosema Invisible, kuwa raia mwema yaweza kutumiwa bila kujijua, vivyo hivyo huyo ndugu aweza akawa anataka kututumia dhidi ya raia mwema bila sisi kujijua!!


WAJINGA NDIO WALIWAO

Nawahi lindo!!!
 
ukishakuwa big boss mpaka ukawa unaitishia "system" hatua
inayofuata ni "kupopolewa" tu na unabaki historia.
 
hata sielewi...
Gazeti ni biashara ya mtu na inategemea unataka kuwatangazia wananchi kitu gani.. Hupendi Matangazo usinunue, tafuta gazeti lenye kurasa nyingi za habari unazotaka wewe kusoma.
Inawezekana kabisa Raia mwema wana wateja wengi wanaotaka kununua vitu, kutafuta kazi, kutafuta wachumba na kadhalika, hivyo soko lao la biashara limehama toka habari za Kudanganyana kwenda habari za maisha halisi..
It's all business!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…