Mnatuchosha na blah blah zenu, mlianza kusema hakuna uchaguzi utakao rudiwa, - umerudiwa,
maalim lazima atangazwe mshindi-shein katangazwa, na sasa mmeanza kuja na story za kuendelea kuwapotezea muda wa Tanzania, wakati kesho shein anaapishwa na maisha yanaendelea ... you guys better admit it and move on ... mjipange upya kivingine ... its over.
Walishaamua kutofuata sheria kwa kufuta uchaguzi halali na hata hili la sasa (percentage) hawatafuata sheria. Wataikanyaga tu katiba mradi wako madarakani
Hapo ujanja Jecha atafuta matokeo kwenye jimbo moja alafu watarudia na ADC atashinda kwa kishindo kisha Hamad atateuliwa kuwa Makamu wa kwanza wa rais. Wapi Jechaaaaa mze wa kuokoa jahazi?
kwani jecha si ajitokeze hadharani atanganze matokeo upya? Kwann nini bwana Zanzibar Post
BAADA YA CCM KUKOSEA KUKOKOTA TARAKIMU NA KUTOA TAARIFA RASMI YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MAJEREO MATOKEO RASMI HAYAKIDHI MATAKWA YA KATIBA YA ZANZIBAR YA SASA NA HIVYO UNAPASWA KUFANYIKA UPYA SIO MAREJEO TENA. - SHENI NI MKOSI !
Kufuatia matokeo rasmi yaliotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kutokidhi matakwa ya kikatiba uchaguzi wa Zanzibar unapaswa kuitishwa upya na sio marejeo tena.
CCM wanapenda namba lakini hawajui kukukota, walipaswa kujua athari za matokeo rasmi waliyotangaza, inashangaza Tume ya Uchaguzi Zanzibar mkurugenzi wake ni mtu wa mahesabu na makamishna wawili ni watu wa mahesabu lakini bado wamefanya makosa yatakayoligharimu taifa fedha nyingi.
Kwa kukidhi matakwa ya katika ya sasa uchaguzi unapaswa huitishwa upya, yaani uandikishaji wapiga kura upya, uteuzi wa wagombea upya, kampeni nyengine na upigaji kura upya (fresh election).
Na hii inatokana na CCM kuwa "rigid" kupanga matokeo ya wao kusomba viti vyote, kwa mujibu wa masharti ya katiba raisi mteule baada ya kuapishwa atatakiwa kuteuwa makamu wawili wa raisi ndani ya siku saba, na mmoja katika makamu wa raisi ni makamu wa kwanza wa raisi ambaye atatokana na na chama kilichopata nafasi ya pili katika idadi ya kura kwa angalau 10% na hakuna chama kilichoshiriki uchaguzi wa marejeo kilichofika 10%.
Na kama hakuna chama kilichofika 10% katiba inataka nafasi hiyo kupewa chama kilichopata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi endapo ingekuwa mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani, lakini katika uchaguzi wa marejeo CCM ilikuwa na wapinzani 12 katika nafasi ya uraisi.
Ili kukidhi matakwa ya katiba inabidi aidha katiba kubadilishwa na hilo lina ghamara kubwa kwa sababu kubadilisha kifungu chochote cha katiba ni lazima marekebisho hayo yapelekwe katika baraza la wawakilishi na hoja kupita kwa theluthi mbili na kisha yapigiwe kura ya maoni na wanzanzibari wote kwa wingi wa theluthi mbili kuondoa vifungu vya katiba vinavyoweka masharti hayo ya kikatiba.
Vinginevyo uchaguzi unapaswa kuitishwa upya (fresh election) kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura ili kukidhi matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Vinginevyo Zanzibar itaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba tangu katiba ya Zanzibar ilipoasisiwa mwaka 1984.
Asilimia kubwa ya wanasiasa wetu ni wachumia tumbo,muangalie huyo Hamad Rashid kwa alichokifanya,
Pili kama Jecha alijua fika kuwa serikali ya umoja wa kitaifa inatambulika kikatiba na ili kumpata makamu wa Rais unahitaji angalau 10% ya kura zote basi wangechakachua kwa kumpa Hamad Rashid hiyo 10% ili awe makamu wa kwanza wa Rais,kama hawakuliona hilo na katiba ndivyo inavyotamka,je watampata wapi makamu wa Rais ilhali hakuna ailefikia hicho kiwango?watupe jibu.
Hapo ujanja Jecha atafuta matokeo kwenye jimbo moja alafu watarudia na ADC atashinda kwa kishindo kisha Hamad atateuliwa kuwa Makamu wa kwanza wa rais. Wapi Jechaaaaa mze wa kuokoa jahazi?
Asilimia kubwa ya wanasiasa wetu ni wachumia tumbo,muangalie huyo Hamad Rashid kwa alichokifanya,
Pili kama Jecha alijua fika kuwa serikali ya umoja wa kitaifa inatambulika kikatiba na ili kumpata makamu wa Rais unahitaji angalau 10% ya kura zote basi wangechakachua kwa kumpa Hamad Rashid hiyo 10% ili awe makamu wa kwanza wa Rais,kama hawakuliona hilo na katiba ndivyo inavyotamka,je watampata wapi makamu wa Rais ilhali hakuna ailefikia hicho kiwango?watupe jibu.
Nilimsikia Mtoto wa Karume akisema wanataka Bunge la chama kimoja ili wabadili Katiba ya Zanzibar ikidhi haja ya CCM kwa kuondoa nafasi ya URAIS kugombewa na vyama vingine,nafasi urais ibakiwe kwa CCM tu,hao wengine labda wagombee Udiwani.
Huyu mwanasheria anayedai matokeo hayajakidhi matakwa ya kikatiba hivyo unapaswa kurejewa ni jipu lililooza inabidi atumbuliwe mapema! Ni aibu kwa mwanasheria kudai hivyo!
Ukweli ni kwamba matokeo hayajakidhi kuundwa kwa serikali ya UMOJA wa kitaifa! Kwa hiyo itaundwa serikali ya chama kimoja!
Mantiki ya serikali ya UMOJA wa kitaifa ni matokeo ya uchaguzi kutokutofautiana kwa kiasi kikubwa. Lakini kwa matokeo ambayo mgombea mmoja amezoa zaidi ya asilimia 90 katiba iliona hakuna mantiki ya kuunda serikali ya UMOJA wa kitaifa! Ndiyo maana katiba haisemi katika mazingira hayo serikali ya UMOJA wa kitaifa itaundwaje, maana haipaswi kuundwa katika mazingira hayo!
Ndiyo maana Hamad Rashid ameangukia pua!
Kama Shein akichagua Makamu wa kwanza wa rais katika mazingira haya, atakuwa amevunja katiba na baraza la wawakilishi wanaweza kumwajibisha!

ah sasa, niwekeni nuruni! inamaana uchaguzi wa zanzibar tayar comfirmed kwamba utafanyika upya? au hii thread ni wazo tu la mwandishi? kama ni wazo bs asahau kabsa, mana FISIEM hawawez fanya wala kuafki kitu hcho. as long as wanauwezo mkubwa kiamri ndani ya nchi, bs that's impocble.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.