Msokotano mpya wazuka Zanzibar

Msokotano mpya wazuka Zanzibar

Wengine hatuna iyo katiba tuwekeeni hata link tuisome kwanza kuliko kuchangia vitu tusivovijua
 
Jecha ngoma yake kashaicheza na kuimaliza walivyompangia, sasa zamu ya wanasheria kupewa ngoma waicheze kuhakikisha katiba inaendana na matakwa ya ccm, kazi ni kwao sasa kufuata misingi ya sheria au kuabudu ulafi wa ccm.
 
Waungwana, hivi mnatambua kwamba koti la muungano hawa ndugu zetu linawabana,
Wazanzibar kwa ujumla hawautaki muungano,Walishamaliza mchezo tangu25/10/2015 kwa kuipa CUF.
Tatizo Tanganyika wakaingilia kati,wanalazimisha muungano.

Hapo hakuna chakukosea wala nini.
Wazanzibar ni wamoja.
Wazanzibar walishadai Zanzibar ni nchi, tukasema sawa isiwe shida! Sasa wamekabana koo huko wakaanza kukimbilia kwa Magufuli, akawaambia kayamalizeni nchini mwenu na tume yenu ya uchaguzi!
 
Soma katiba ya Zanzibar, usipaparike. Kwa mazingira ya Zanzibar, wakati wanaandika katiba haikufikiriwa kuwa kuna siku itatokea chama kimoja kinaweza kupata kura zaidi ya 90%.

Inaonekana hata hujui kwa nini ilionekana kuna haja ya kuwa na SUK. Sababu iliyosababisha kuwepo na SUK ni ukweli ambao wahusika wote walikubaliana nao kuwa kwa siasa za Zanzibar, vyama hivi viwili vikuu vina wafuasi karibia 50% by 50%. Jambo ambalo halikufikiriwa wakati wa kuandika katiba ni kuwa Jecha na CCM, kwao katiba na sheria siyo kitu. Waandikaji wa katiba hawakufikiria kuwa kuna siku kunaweza kutokea mshenzi mmoja kuamua kuwaondoa wagombea wengine kwa hila za wazi na akaungwa mkono na serikali.

Hatuongelei ushabiki, tunaongelea katiba na mazingira ya uundwaji wa SUK. Wabakaji wa demokrasia wamemtumia mwizi asiye na akili maana angekuwa na akili angeuboresha wizi wake ili ukidhi vigezo vya katiba, na ndivyo madikteta wengi Duniani wanavyofanya.

Open up your mind and argue intelligently!
Pole! Naona huna uwezo wa kuelewa! Katiba ya Zanzibar iko wazi! Imeweka masharti ya kuunda hiyo serikali ya UMOJA wa kitaifa! Masharti hayajatimia kwa hiyo haiwezi kuundwa, vinginevyo ni kuvunja katiba! Kwa heri!
 
Mkuu Ugunyu namaanixha ukanjanja usiogope kiswahili ni muunganiko wa lahaja mbalimbali zikiwemo za vijiweni
 
Wataendelea kutumia hela za wanyonge hadi lini wanatowa wapi hela za uchaguzi
 
Mara zote ukifanya jambo ukiwa na nia ya mashaka lazima uchemshe upande fulan bila hata kujua, Lakini kama suala la uchaguzi wa marejeo limewezekana nafikiri wanaweza kufanya maamuzi mengine ya kushangaza tena.
 
katiba ya zanzimbar inasema hivi cha upinzani kilichoshika nafasi ya pili na kina asilimia kumi au zaidi kwenye chama hicho ndiko atatoka makamu wa raisi ikiwa hakuna chama kilichofikisha asilimia 10 basi chama cha upinzani chenye wawakilishi wengi ndiko makamu wa raisi atatoka . Sasa waliopo zanzibar ni chama kipi kimepata wawakilishi wengi?
 
si dhani kama CCM suala la mahitaji ya kikatiba linawanyima usingizi..
katiba ni maandishi tu kama yale yaliyoandikwa kwenye vitabu vinavyoitwa..
*serikali ya kidemokrasia
*utawala wa sheria na haki
*misingi ya utawala bora
 
tunamshukuru Mungu kwa kusikia dua za wazanzibar , usifanye mchezo na ubani ndani ya chetezo .
 
Hivi ccm unawajua kwa ujuha wao? Ngoja uone sasa watakwambia hamad rashid alipata 12% sema walikosea kujumlisha, na ushahidi utaletwa, ccm zaidi ya fisi kwa uchu
 
Kama katiba imevunjwa,hapo kuna doa kwa nchi
katiba waliitunga wenyewe,na kwa mahesabu ya karibu
ililenga endapo chama chochote kibwa kitakosa urais
basi kihusishwe kwenye utawala,sasa ona madhara yake
sheria imekuwa tanzi,basi wapika matokeo
walitakiwa kuhakikisha aMadi RasHin anapata hiyo 10%
angalau apachikwe huo umakamu rais
sasa mahesabu ziro amezaa ziro.

Lakini msemo unasema "Mbwa kala mbwa"
 
Hivi ccm unawajua kwa ujuha wao? Ngoja uone sasa watakwambia hamad rashid alipata 12% sema walikosea kujumlisha, na ushahidi utaletwa, ccm zaidi ya fisi kwa uchu
Labda sema vile vyama vyote 12 ambavyo vinaunda sisiemuB
vitaambiwa viunganishe nguvu viitwe kambi rasmi ya upinzani.
Japokuwa naona kuvunja katiba ya zanzibar,siyo shida
kwa wanaokumbuka kipindi cha bunge maalum la katiba,
mwanasheria mkuu wa zanzibar aliyesimama kidete katiba ya zanzibar
isichezewe,aliporudi nyumbani kibarua kiliota nyasi.

Nadhani hata katika hili mwanasheria mkuu
atatafuta mahali pa kuongeza kipengere fulani
na mambo yataendelea kama kawa.

Nawaomba wazanzibar wasitulaumu tena watanganyika
nimegundua kikulacho ki nguoni mwako.
ukiwasingizia waliokaa karibu na wewe unawaonea.
 
Ni kweli unavyosema, lakini kubadilisha katiba ni lazima ipigwe kura ya maoni Zanzibar, na kwa maana hiyo, uchaguzi mwengine ni lazima, kubadilisha katiba ama kuendelea na katiba! Kuendelea kutawala bila ya SUK ni kinyume cha sheria na kumchaguwa Makamo kutoka kwa wagombea ambao hawajatimiza ikadi nayo ni kuvunja sheria. Uchaguzi mpya unahitajika mpaka ikadi ipatikane. Venginevyo, CCM wanakula kiti moto mwezi wa Ramadhani mchana na hio wameona haitoshi, wameagiza kreti za bia. Haramu juu ya haramu. They put too much attention on cents while loosing shillings at the other end!
Ccm wakiamua jambo lao hata iweje watalitimiza tuuu.kwa ccm katiba na sheria ni upuuzi usio takiwa fuatwa.

Wanatamani hata kusingekua na katiba na sheria,lau wangelikua wanatambua uwepo wa katiba na sheria kuna upuuzi mwingi unaofanyika kinyume cha katiba na sheria.

Muda wowote,mahali popote,namna yeyote,kwa yeyote ccm wakiamua jambo lao wanafanya.labda wasitake tu.mark my word.
 
Back
Top Bottom