UPDP imepata kiti kimojaZanzibar Post
.......
Na kama hakuna chama kilichofika 10% katiba inataka nafasi hiyo kupewa chama kilichopata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi endapo ingekuwa mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani, lakini katika uchaguzi wa marejeo CCM ilikuwa na wapinzani 12 katika nafasi ya uraisi.
Ili kukidhi matakwa ya katiba inabidi aidha katiba kubadilishwa na hilo lina ghamara kubwa kwa sababu kubadilisha kifungu chochote cha katiba ni lazima marekebisho hayo yapelekwe katika baraza la wawakilishi na hoja kupita kwa theluthi mbili na kisha yapigiwe kura ya maoni na wanzanzibari wote kwa wingi wa theluthi mbili kuondoa vifungu vya katiba vinavyoweka masharti hayo ya kikatiba.
Vinginevyo uchaguzi unapaswa kuitishwa upya (fresh election) kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura ili kukidhi matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Vinginevyo Zanzibar itaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba tangu katiba ya Zanzibar ilipoasisiwa mwaka 1984.
Chanzo : Mwandishi Wetu Zanzibar Post
Where is my popcorn bag! Manake hii shughuli pevu
Hivi hao watoto wamepiga kura kweli au utani? Kama ni kweli walio bariki ujinga huo walikuwa wanafikiria nini, au ndio kulewa madaraka kwenyewe!!!
Ni jimbo la Ziwani huko pembaPole kilishanyang'anywa siku nyingi rafiki kimenyakuliwa na CCM
Siyo hivyo tu lakini pia Hamad Rashid anahesabika hivi sasa kuwa ni msaliti no. 1 ya wazanzibari na hiyo dhambi ya usaliti wake itamtafuna hadi siku ya mwisho ya maisha yake hapa duniani.
Si hivyo tu lakini pia huyo Hamad atahukumiwa nayo hiyo dhambi 'kesho' kwa Mwenyezi Mungu siku ya kiama.
Samahani Kada mwenzangu..mtoa mada amezungumzia two third kama itapitishwa na baraza la wawakilishi ili ipigwe kura ya maoni kubadili katiba kuondoa SUK..kama itafanyika hivyo basi wananchi wa Zanzibar two third haitafika hata kama tufanye hujuma. Lakini two third kwa Baraza mbona ipo tayari shekhe..mtiti ni kwa wananchi wenyewe wa Zanzibar..CUF watakataa na sisi tutakubali lakini hatuzidi NUSU ya Wazanzibar wote.Mbona nyinyi hamtaki kuelewa? CCM imeshinda kwa kishindo katika nafasi mbalimbali za Uongozi mara baada ya uchaguzi wa marejeo. Ina wawakilishi wengi hadi huko Barazani ambako ndiko wataamua kuendelea na SUK au kuitupilia mbali. Hiyo two third sio issue kabisa. CUF wajiandae kuisoma namba tu.
Naomba wachambuzi mahiri mtusaidie sisi mbumbumbu. Hivi hali y kisiasa ya Zanzibar inatofautiana kiasi gani na hali aliyojenga Nkurunziza nchini Burundi?Hiyo concept ya wahafidhina wa CCM ya kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia, wakati in reality Mwenyezi Mungu ametoa hati miliki kwa kila mtanzania kuweza kuongoza nchi hii baada ya kupata ridhaa kutoka kwa wananchi walio wengi, na hiyo dhambi kubwa ndiyo itakayowatafuna Dr Shein na company yake ya jecha na wahafidhina wenziwe hadi siku ya mwisho ya maisha yao hapa diniani.
Laana hiyo itakayowakumba wahafidhina wa CCM, watanzania hatuna sababu ya kuwaonea huruma hata kidogo kwa kuwa hiyo ni laana ya kujitakia kutokana na kupuuza matakwa ya wazanzibari waliyoyafanya kwenye sanduku la kura hapo tarehe 25/10/2015.
Ee Mungu iokoe Zanzibar na kwa ukuu wako ambao hauwezi kufananishwa na kitu chochote, tumia uwezo wako kuwapa wazanzibari wengi wanachokitaka.