Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Zanzibar Post
BAADA YA CCM KUKOSEA KUKOKOTA TARAKIMU NA KUTOA TAARIFA RASMI YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MAJEREO MATOKEO RASMI HAYAKIDHI MATAKWA YA KATIBA YA ZANZIBAR YA SASA NA HIVYO UNAPASWA KUFANYIKA UPYA SIO MAREJEO TENA. - SHENI NI MKOSI !
Kufuatia matokeo rasmi yaliotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kutokidhi matakwa ya kikatiba uchaguzi wa Zanzibar unapaswa kuitishwa upya na sio marejeo tena.
CCM wanapenda namba lakini hawajui kukukota, walipaswa kujua athari za matokeo rasmi waliyotangaza, inashangaza Tume ya Uchaguzi Zanzibar mkurugenzi wake ni mtu wa mahesabu na makamishna wawili ni watu wa mahesabu lakini bado wamefanya makosa yatakayoligharimu taifa fedha nyingi.
Kwa kukidhi matakwa ya katika ya sasa uchaguzi unapaswa huitishwa upya, yaani uandikishaji wapiga kura upya, uteuzi wa wagombea upya, kampeni nyengine na upigaji kura upya (fresh election).
Na hii inatokana na CCM kuwa "rigid" kupanga matokeo ya wao kusomba viti vyote, kwa mujibu wa masharti ya katiba raisi mteule baada ya kuapishwa atatakiwa kuteuwa makamu wawili wa raisi ndani ya siku saba, na mmoja katika makamu wa raisi ni makamu wa kwanza wa raisi ambaye atatokana na na chama kilichopata nafasi ya pili katika idadi ya kura kwa angalau 10% na hakuna chama kilichoshiriki uchaguzi wa marejeo kilichofika 10%.
Na kama hakuna chama kilichofika 10% katiba inataka nafasi hiyo kupewa chama kilichopata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi endapo ingekuwa mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani, lakini katika uchaguzi wa marejeo CCM ilikuwa na wapinzani 12 katika nafasi ya uraisi.
Ili kukidhi matakwa ya katiba inabidi aidha katiba kubadilishwa na hilo lina ghamara kubwa kwa sababu kubadilisha kifungu chochote cha katiba ni lazima marekebisho hayo yapelekwe katika baraza la wawakilishi na hoja kupita kwa theluthi mbili na kisha yapigiwe kura ya maoni na wanzanzibari wote kwa wingi wa theluthi mbili kuondoa vifungu vya katiba vinavyoweka masharti hayo ya kikatiba.
Vinginevyo uchaguzi unapaswa kuitishwa upya (fresh election) kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura ili kukidhi matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Vinginevyo Zanzibar itaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba tangu katiba ya Zanzibar ilipoasisiwa mwaka 1984.
Chanzo : Mwandishi Wetu Zanzibar Post