Msokotano mpya wazuka Zanzibar

Msokotano mpya wazuka Zanzibar

Hivi hii issue ya Zbar haiwezi pelekwa mahakama zingine ikapatiwa uvumbuzi?
 
Mfalme Suleimani alipoambiwa na Mwenyezi Mungu aombe atakacho atapewa, yeye aliomba Hekima na Busara,hili kwa viongozi wetu wa sasa ni ngumu sana wao wanafikiria madaraka tu ile dhana ya utawala bora ishawekwa pembeni.
 
Kama katiba imevunjwa,hapo kuna doa kwa nchi
katiba waliitunga wenyewe,na kwa mahesabu ya karibu
ililenga endapo chama chochote kibwa kitakosa urais
basi kihusishwe kwenye utawala,sasa ona madhara yake
sheria imekuwa tanzi,basi wapika matokeo
walitakiwa kuhakikisha aMadi RasHin anapata hiyo 10%
angalau apachikwe huo umakamu rais
sasa mahesabu ziro amezaa ziro.

Lakini msemo unasema "Mbwa kala mbwa"
Ccm ni bingwa wa namba lakini hawajui MAGAZIJUTO imewapiga chenga() ÷ × + -
 
Ccm wakiamua jambo lao hata iweje watalitimiza tuuu.kwa ccm katiba na sheria ni upuuzi usio takiwa fuatwa.

Wanatamani hata kusingekua na katiba na sheria,lau wangelikua wanatambua uwepo wa katiba na sheria kuna upuuzi mwingi unaofanyika kinyume cha katiba na sheria.

Muda wowote,mahali popote,namna yeyote,kwa yeyote ccm wakiamua jambo lao wanafanya.labda wasitake tu.mark my word.
Hizo ndio dalili zote za utawala unaofika ukingoni. CCM hawawezi kuwa maharamia zaidi ya serikali ya kijeshi ya Myanmar fka Burma. CCM haiwezi kuwa na power kuliko aliyikuwa nayo Husni Mubarak. CCM haiwezi kuwa na ushawishi kwa wananchi wake zaidi ya Muammar Gaddafi. CCM haiwezi kuwa na watekelezaji majasusi zaidi ya aliokuwa nao Saddam Husein. Wote wako wapi sasa hivi? Jembe likikaribia kufa huzidi makali!
 
Mimi siamini kama kweli Ccm walishindwa kumpa HR hiyo ten percent! Mi nadhani kuna plan mahususi ambayo Ccm wameipanga baada ya kugundua upuuzi waliowafanyia Wazanzibari,
 
Wamefanikiwa kuvunja Muungano ndio washindwe kubadilisha hicho kifungu? Subiri watakuja wanasheria wao sasa hivi na watasema hakuna Katiba iliyovunjwa. Subirini muone
Wamekuja na kamsemo siku hizi " busala za raisi zitatumika"
 
Hao wahafidhina wa CCM hivi sasa hawafuati tena katiba ya nchi, wanachojua wao ni ubabe na utemi, wakiamini kuwa vyombo vya dola 'wanavyovimiliki ' ndivyo vitakavyoendelea kuwawekea kinga na kuwalinda katika utawala wao wa kidhalimu.
unakumbuka Tunisia? watakimbia wenyewe
 
Back
Top Bottom