chipolopolo 2
JF-Expert Member
- Nov 10, 2014
- 3,292
- 1,841
Mh mbona makubwa .Watu walikua wanaenda kupiga kura ukifika kituoni unaambiwa wewe tia wino tu kidole kura tayari tulishapiga.
Mh mbona makubwa .Watu walikua wanaenda kupiga kura ukifika kituoni unaambiwa wewe tia wino tu kidole kura tayari tulishapiga.
KAMA WALIWEZA KULAZIMISHA UCHAGUZI WA MARUDI KINYUME CHA SHERIA WATASHINDWA KUBADILISHA HIYO KATIBA YENU? HIVI MNAWAJUA CCM AU MNAWASIKIA? WATABADILISHA LABDA MUNGU AINGILIE KATI LA SIVYO MTAJUA KIBURI CHA CCM NA JINSI WANAVYO JIVUNIA DOLA KUVUNJA KATIBA![]()
Zanzibar Post
BAADA YA CCM KUKOSEA KUKOKOTA TARAKIMU NA KUTOA TAARIFA RASMI YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MAJEREO MATOKEO RASMI HAYAKIDHI MATAKWA YA KATIBA YA ZANZIBAR YA SASA NA HIVYO UNAPASWA KUFANYIKA UPYA SIO MAREJEO TENA. - SHENI NI MKOSI !
Kufuatia matokeo rasmi yaliotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kutokidhi matakwa ya kikatiba uchaguzi wa Zanzibar unapaswa kuitishwa upya na sio marejeo tena.
CCM wanapenda namba lakini hawajui kukukota, walipaswa kujua athari za matokeo rasmi waliyotangaza, inashangaza Tume ya Uchaguzi Zanzibar mkurugenzi wake ni mtu wa mahesabu na makamishna wawili ni watu wa mahesabu lakini bado wamefanya makosa yatakayoligharimu taifa fedha nyingi.
Kwa kukidhi matakwa ya katika ya sasa uchaguzi unapaswa huitishwa upya, yaani uandikishaji wapiga kura upya, uteuzi wa wagombea upya, kampeni nyengine na upigaji kura upya (fresh election).
Na hii inatokana na CCM kuwa "rigid" kupanga matokeo ya wao kusomba viti vyote, kwa mujibu wa masharti ya katiba raisi mteule baada ya kuapishwa atatakiwa kuteuwa makamu wawili wa raisi ndani ya siku saba, na mmoja katika makamu wa raisi ni makamu wa kwanza wa raisi ambaye atatokana na na chama kilichopata nafasi ya pili katika idadi ya kura kwa angalau 10% na hakuna chama kilichoshiriki uchaguzi wa marejeo kilichofika 10%.
Na kama hakuna chama kilichofika 10% katiba inataka nafasi hiyo kupewa chama kilichopata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi endapo ingekuwa mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani, lakini katika uchaguzi wa marejeo CCM ilikuwa na wapinzani 12 katika nafasi ya uraisi.
Ili kukidhi matakwa ya katiba inabidi aidha katiba kubadilishwa na hilo lina ghamara kubwa kwa sababu kubadilisha kifungu chochote cha katiba ni lazima marekebisho hayo yapelekwe katika baraza la wawakilishi na hoja kupita kwa theluthi mbili na kisha yapigiwe kura ya maoni na wanzanzibari wote kwa wingi wa theluthi mbili kuondoa vifungu vya katiba vinavyoweka masharti hayo ya kikatiba.
Vinginevyo uchaguzi unapaswa kuitishwa upya (fresh election) kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura ili kukidhi matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Vinginevyo Zanzibar itaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba tangu katiba ya Zanzibar ilipoasisiwa mwaka 1984.
Chanzo : Mwandishi Wetu Zanzibar Post
Ni kweli unavyosema, lakini kubadilisha katiba ni lazima ipigwe kura ya maoni Zanzibar, na kwa maana hiyo, uchaguzi mwengine ni lazima, kubadilisha katiba ama kuendelea na katiba! Kuendelea kutawala bila ya SUK ni kinyume cha sheria na kumchaguwa Makamo kutoka kwa wagombea ambao hawajatimiza ikadi nayo ni kuvunja sheria. Uchaguzi mpya unahitajika mpaka ikadi ipatikane. Venginevyo, CCM wanakula kiti moto mwezi wa Ramadhani mchana na hio wameona haitoshi, wameagiza kreti za bia. Haramu juu ya haramu. They put too much attention on cents while loosing shillings at the other end!KAMA WALIWEZA KULAZIMISHA UCHAGUZI WA MARUDI KINYUME CHA SHERIA WATASHINDWA KUBADILISHA HIYO KATIBA YENU? HIVI MNAWAJUA CCM AU MNAWASIKIA? WATABADILISHA LABDA MUNGU AINGILIE KATI LA SIVYO MTAJUA KIBURI CHA CCM NA JINSI WANAVYO JIVUNIA DOLA KUVUNJA KATIBA
Kwa jinsi walivyo walafi wa madaraka watapiga kimya wao bora watu wafe lakin sio upinzan uongoze nchi!! Yanamwisho lakin..CUF waliposusia halafu ccm ikasomba mpaka watoto wakapige kura ili wapate ushindi wa kishindo, waliwaona CUF hamnazo sana
Aamin...Hiyo concept ya wahafidhina wa CCM ya kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia, wakati in reality Mwenyezi Mungu ametoa hati miliki kwa kila mtanzania kuweza kuongoza nchi hii baada ya kupata ridhaa kutoka kwa wananchi walio wengi, na hiyo dhambi kubwa ndiyo itakayowatafuna Dr Shein na company yake ya jecha na wahafidhina wenziwe hadi siku ya mwisho ya maisha yao hapa diniani.
Laana hiyo itakayowakumba wahafidhina wa CCM, watanzania hatuna sababu ya kuwaonea huruma hata kidogo kwa kuwa hiyo ni laana ya kujitakia kutokana na kupuuza matakwa ya wazanzibari waliyoyafanya kwenye sanduku la kura hapo tarehe 25/10/2015.
Ee Mungu iokoe Zanzibar na kwa ukuu wako ambao hauwezi kufananishwa na kitu chochote, tumia uwezo wako kuwapa wazanzibari wengi wanachokitaka.
Umevurugwa wewe sio bure toka post ya kwanza mpaka ya kabla ya post hayo unayoongelea hayajaandikwa wewe umeyatoa wapi?udini na ukamilifu kwenye maisha manao nyinyi tuu ndio wasemaji na waonaji kwenye maisha ya siasa ya nchii hii? mshayasema mangapi na kulaani mangapi yamefanikiwa na yaloendelea!
kazi mlobaki kuendekea na fitina za kisiasa na kujifanya nyinyi ni wakamilifu hivi huo wema wenu na ubora wenu mnatusaidia nn ss wanyonge sii kutia fitina za kidini na kuapizaa tuu na kuwaona watu wote hawako sawa ila nyinyi na wazungu.
haya nasubiri uwo ukamilifu wenu wa kususa na kuanza kuapiza nione kama utapangua mchezo wa kihindi kuendeleaa