Msimu wa Pili wa Filamu ya Serengeti kutoka kesho

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya kupata umaarufu mkubwa kutokana na upekee wa mtindo wake masimulizi, Msimu wa Pili wa Filamu Serengeti (Serengeti II) unarejea kuanzia kesho.

Filamu hiyo inayosimulia maisha ya kila siku ya wanyama katika mbuga ya Serengeti nchini Tanzania inajitofautisha na filamu nyingi zinazoonesha wanyama wa Serengeti kutokana na kuwapa wanyama hao uhalisia wa maisha kwa kuonesha jitihada zao za mapambano, hisia za upendo, furaha, maumivu, kukata tamaa nk., pamoja na kuwapa majina kutokana na mwenendo wa matukio.

Katika msimu wa pili, tujiandae kuziona “sura” pendwa za wanyama kama Kali, Sefu, Nalla, Tembo, Bakari na Shani pamoja na ongezeko la watoto wao kama vile Aiysha, mtoto wa KiKay kutoka Msimu wa Kwanza na watoto wake, akiwamo pia Punda, mtoto wa Shani.

Tofauti na sauti nzito ya msimulizi John Boyega kutoka Msimu wa Kwanza, Msimu wa Pili unakuja na sauti nyororo ya mwigizaji kutoka nchini Kenya na mshindi wa tuzo ya Academy, Lupita Nyongo ambaye anatuongoza kuyaelewa maisha ya wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa ustadi mkubwa.

Msimu wa Pili wa Filamu ya Serengeti una sehemu sita, na utaanza kuonekana rasmi katika Chaneli ya Discovery+ kuanzia kesho, Julai 19, saa 9 alfajiri kwa majira ya Afrika Mashariki.

 
Back
Top Bottom