Linapokuja suala la filamu, nauheshimu sana Mkoa wa Tanga

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,140
14,678
Tanga ndiko kwa “magwiji wa filamu nchini”. Kwa nini nawaita hivyo? Ndio watu pekee waliothubutu kuandaa filamu za kibiashara katika miaka ya 1990 japo mazingira yalikuwa magumu sana; wakati huo hakukuwa na mahala pa kuuzia filamu, hata uoneshaji sinema kwenye majumba ya sinema ulikuwa ukisuasua kutokana na kuingia kwa vituo vya televisheni, na sinema zilizotawala nchini zilikuwa za Kihindi.

Pia katika miaka hiyo teknolojia ilikuwa bado ndogo na vituo vya televisheni ndo kwanza vilikuwa vimeanza. Wakati huo kulikuwa na vituo vya CTN, DTV na ITV tu ambavyo hata hivyo vilikuwa vikirusha matangazo yake hapahapa jijini Dar es Salaam.

Ni filamu ya “Shamba Kubwa” (1995) iliyotungwa na kuongozwa na Mwl. Kassim El-Siagi wa Tanga ndiyo iliyofungua milango ya filamu za kibiashara nchini. Kwa walio wengi pengine watanishangaa kwa kuwa hawajahi kuiona filamu hii kwa kuwa wakati ule ilioneshwa kwenye majumba ya sinema; Majestic Cinema – Tanga, Emipre Cinema – Dar es Saalaam, Metropole Cinema – Arusha, na kadhalika.

‘Shamba Kubwa’ ndiyo filamu iliyowaibua wasanii ambao baadaye wamekuwa mahiri katika ulimwengu wa filamu, kama Hassan Master, Jimmy Master, Kaini na wengineo, ni filamu hii iliyoteka wengi kwa wakati ule japo teknolojia ilikuwa bado ndogo sana ukilinganisha na hivi sasa.

Filamu hii na nyingine zilizofuata kama ‘Love Story Tanganyika na Unguja (1998)' ya Amri Bawji, ‘Kifo Haramu’ ya Jimmy Master, ‘Dunia Hadaa (2000)' ya Mwl. Kassim El-Siagi, na ‘Augua (2002)' ya Amri Bawji, zote zikitengenezwa na magwiji kutoka Tanga zilitengenezwa katika mfumo wa VHS (analogy), na hata uhariri wake ulitumia akili zaidi kutokana na teknolojia ya wakati huo kuwa ya kiwango kidogo, lakini zilivutia sana kutokana na maudhui na msuko mzuri wa hadithi.

Utengenezaji wa filamu enzi zile kwa kweli ulikuwa ukitufanya tushindwe hata kuwa na zaidi ya sinema mbili za Kitanzania katika soko letu kutokana na ukweli kwamba teknolojia ilikuwa ndogo, hakukuwa na msisimko wala hakukuwa na soko la kuuzia kazi zetu. Sinema zetu zilikuwa zikihifadhiwa kwenye mikanda mikubwa. Lakini pole pole, tukahama na kuyaacha masanduku yale makubwa ya mikanda maarufu kwa jina la VHS na kuhamia kwenye CD maarufu kwa jina la VCD na baadaye DVD.

Hata hivyo, kwa wafuatiliaji wengi wa seekta hii ya filamu nchini, sinema hizi zinaweza kuwa ngeni kwao kwa kuwa wakati huo hatukuwa na mfumo mzuri wa usambazaji na hivyo zilikuwa zikioneshwa kwenye majumba ya sinema, na kuuzwa kwa kiwango kidogo mno.

Ni filamu ya Girlfriend iliyotengenezwa na George Otieno Okumu (maarufu kama Tyson) ndiyo iliyotingisha sekta ya filamu na kuwafanya watazamaji wa filamu nchini kuanza kutamani kuwa na sinema zao. Wengi wanadhani kuwa sinema hii ndiyo sinema ya kwanza ya kibiashara hapa nchini.

Baadaye zilifuatia sinema nyingine nyingi kama Sabrina, Masaa 24, Fungu la Kukosa, Nsyuka, Bifu na nyingine nyingi zilizowaburudisha watazamaji japo zilikuwa na makosa ya hapa na pale ya kiufundi, msuko wa hadithi na maudhui.

Tanga pia ndiyo mkoa wa kwanza kuanzisha chama cha kitasnia ili kukabiliana na changamoto za tasnia ya filamu. Walianzisha Chama cha Watengeneza Filamu wa Tanga (Tanga Film-Makers Association “TAFMA”) kabla hata filamu ya Girlfriend inayojulikana kwa wengi haijatungwa.
 
Inasikitisha kuona movie za wenzetu za miaka ya 70 huko tunazipata mpaka sasa,ila shamba kubwa ya mwaka 95 hatuna nakala yake mitandaoni mpaka leo.kizazi cha elfu 2000 hawawezi elewa mapinduzi ya filamu zetu,mpaka tulipofikia sasa
Umeona eh! Ukweli bado tuna safari ndefu sana...
 
Hivi yule msanii aliyecheza character ya nsyuka jina lake halisi ni nani?.
 
Yule ras, jina limenitoka kidogo...
Nakumbuka siku moja tukiwa na Mrisho Mpoto (back in 2005, wakati huo hajawa maarufu), tulikuwa Kibaha basi ikawa tafrani, watu walijaa kumwona Nsyuka (kwa sababu ya rasta zake)...
 
Tanga ndiko kwa “magwiji wa filamu nchini”. Kwa nini nawaita hivyo? Ndio watu pekee waliothubutu kuandaa filamu za kibiashara katika miaka ya 1990 japo mazingira yalikuwa magumu sana; wakati huo hakukuwa na mahala pa kuuzia filamu, hata uoneshaji sinema kwenye majumba ya sinema ulikuwa ukisuasua kutokana na kuingia kwa vituo vya televisheni, na sinema zilizotawala nchini zilikuwa za Kihindi.

Pia katika miaka hiyo teknolojia ilikuwa bado ndogo na vituo vya televisheni ndo kwanza vilikuwa vimeanza. Wakati huo kulikuwa na vituo vya CTN, DTV na ITV tu ambavyo hata hivyo vilikuwa vikirusha matangazo yake hapahapa jijini Dar es Salaam.

Ni filamu ya “Shamba Kubwa” (1995) iliyotungwa na kuongozwa na Mwl. Kassim El-Siagi wa Tanga ndiyo iliyofungua milango ya filamu za kibiashara nchini. Kwa walio wengi pengine watanishangaa kwa kuwa hawajahi kuiona filamu hii kwa kuwa wakati ule ilioneshwa kwenye majumba ya sinema; Majestic Cinema – Tanga, Emipre Cinema – Dar es Saalaam, Metropole Cinema – Arusha, na kadhalika.

‘Shamba Kubwa’ ndiyo filamu iliyowaibua wasanii ambao baadaye wamekuwa mahiri katika ulimwengu wa filamu, kama Hassan Master, Jimmy Master, Kaini na wengineo, ni filamu hii iliyoteka wengi kwa wakati ule japo teknolojia ilikuwa bado ndogo sana ukilinganisha na hivi sasa.

Filamu hii na nyingine zilizofuata kama ‘Love Story Tanganyika na Unguja (1998)' ya Amri Bawji, ‘Kifo Haramu’ ya Jimmy Master, ‘Dunia Hadaa (2000)' ya Mwl. Kassim El-Siagi, na ‘Augua (2002)' ya Amri Bawji, zote zikitengenezwa na magwiji kutoka Tanga zilitengenezwa katika mfumo wa VHS (analogy), na hata uhariri wake ulitumia akili zaidi kutokana na teknolojia ya wakati huo kuwa ya kiwango kidogo, lakini zilivutia sana kutokana na maudhui na msuko mzuri wa hadithi.

Utengenezaji wa filamu enzi zile kwa kweli ulikuwa ukitufanya tushindwe hata kuwa na zaidi ya sinema mbili za Kitanzania katika soko letu kutokana na ukweli kwamba teknolojia ilikuwa ndogo, hakukuwa na msisimko wala hakukuwa na soko la kuuzia kazi zetu. Sinema zetu zilikuwa zikihifadhiwa kwenye mikanda mikubwa. Lakini pole pole, tukahama na kuyaacha masanduku yale makubwa ya mikanda maarufu kwa jina la VHS na kuhamia kwenye CD maarufu kwa jina la VCD na baadaye DVD.

Hata hivyo, kwa wafuatiliaji wengi wa seekta hii ya filamu nchini, sinema hizi zinaweza kuwa ngeni kwao kwa kuwa wakati huo hatukuwa na mfumo mzuri wa usambazaji na hivyo zilikuwa zikioneshwa kwenye majumba ya sinema, na kuuzwa kwa kiwango kidogo mno.

Ni filamu ya Girlfriend iliyotengenezwa na George Otieno Okumu (maarufu kama Tyson) ndiyo iliyotingisha sekta ya filamu na kuwafanya watazamaji wa filamu nchini kuanza kutamani kuwa na sinema zao. Wengi wanadhani kuwa sinema hii ndiyo sinema ya kwanza ya kibiashara hapa nchini.

Baadaye zilifuatia sinema nyingine nyingi kama Sabrina, Masaa 24, Fungu la Kukosa, Nsyuka, Bifu na nyingine nyingi zilizowaburudisha watazamaji japo zilikuwa na makosa ya hapa na pale ya kiufundi, msuko wa hadithi na maudhui.

Tanga pia ndiyo mkoa wa kwanza kuanzisha chama cha kitasnia ili kukabiliana na changamoto za tasnia ya filamu. Walianzisha Chama cha Watengeneza Filamu wa Tanga (Tanga Film-Makers Association “TAFMA”) kabla hata filamu ya Girlfriend inayojulikana kwa wengi haijatungwa.
Natafuta filamu ya kibongo ikiitwa "Auguwa" ilitayarishwa na S M Bawji aliyekuwa muasisi wa gazeti la SANI
 
Astakafirullah. Kwa hiyo ile mihela yote ile aliyopata alit....mbea?
Pesa ipi unayoizungumzia?

Jamaa aliigiza filamu zisizozidi 5 na filamu iliyompa umaarufu ni hiyo Insyuka na pesa aliyolipwa haiizidi milioni 1 kutokana na bei za kipindi hicho.

Mpaka sasa pia sidhani kama kuna muigizaji analipwa zaidi ya milioni 5 kwa filamu moja.

Waigizaji wakubwa wengi wanaishia 5 mpaka milioni 2. Kama wapo wanaolipwa zaidi ya milioni 5 kwa sasa hawazidi 10.
 
Ila mbona miaka ya 2000s kulikuwa na michezo ya kidedea na Maisha?

Nsyuka ilikuwa mbele sana miaka ya 2003 hivi.

Sio mtaalamu kwenye maswala ya filamu. Napata wakati mgumu kuamini kuwa filamu zilianza Tanga 1995.

Nieleweshwe.

Pia nimepitia website ya bodi ya filamu Tanzania. Inaonyesha filamu zimeanza toka kipindi cha ukoloni

Natafuta filamu ya kibongo ikiitwa "Auguwa" ilitayarishwa na S M Bawji aliyekuwa muasisi wa gazeti la SANI
Inaitwa AUGUA, filamu ya kwanza nchini iliyopata udhamini wa Mfuko wa Utamaduni, mtayarishaji si Said Bawji (mwasisi wa Sani) bali kaka yake, Amri Bawji, ambaye alikuja kuwa mhariri wa Sani baada ya kifo cha Said. Pia alianzisha jarida la AMBHA...

Mimi nina nakala ya filamu hii...
 
Ila mbona miaka ya 2000s kulikuwa na michezo ya kidedea na Maisha?

Nsyuka ilikuwa mbele sana miaka ya 2003 hivi.

Sio mtaalamu kwenye maswala ya filamu. Napata wakati mgumu kuamini kuwa filamu zilianza Tanga 1995.

Nieleweshwe.

Pia nimepitia website ya bodi ya filamu Tanzania. Inaonyesha filamu zimeanza toka kipindi cha ukoloni

Ni kweli filamu zilianza tangu kipindi cha ukoloni (enzi za kina Kawawa) ila zilikuwa za miradi na ziliegemea kwenye mafunzo, hapa tunaongelea commercial films (filamu za kibiashara)...
 
Ila mbona miaka ya 2000s kulikuwa na michezo ya kidedea na Maisha?

Nsyuka ilikuwa mbele sana miaka ya 2003 hivi.

Sio mtaalamu kwenye maswala ya filamu. Napata wakati mgumu kuamini kuwa filamu zilianza Tanga 1995.

Nieleweshwe.

Pia nimepitia website ya bodi ya filamu Tanzania. Inaonyesha filamu zimeanza toka kipindi cha ukoloni

Kidedea ni tamthiliya ilivyokuwa ikirushwa ITV na kundi la Mambo hayo au kama sikosei Kaole Sanaa group .

Nsyuka ni filamu ya kwanza ya kutisha iliyopata mapokezi makubwa ila kabla yake kulikuwa na filamu ya kibuyu ambayo haikutamba sana.

Shamba kubwa nayo ni ya zamani sana.
 
Kidedea (chini ya mwanadada Peace), Mambo Hayo (Nyota Ensemble chini ya Bishanga na wenzake) na Kaole yalikuwa makundi matatu tofauti yaliyorusha michezo ITV. Kidedea ndo iliyowaibua akina Jengua, Tabia n.k...
 
Back
Top Bottom