Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wanataka Bei ya vitu iwe ile ile miaka nenda rudi - sukari, chumvi, mafuta vyote visibadilike bei hata kidogo (iwe kuakisi hali ya uchumi au vinginevyo)..
Wanataka kampuni zisife
Wanataka watu wasipoteze ajira
Wanataka benki zisifungwe kea kukosa mitaji
Wanataka Kila mtu awe nacho asiwepo aliyepungukiwa
Wanataka benki zifanye kazi tu; zikitakatisha fedha zisiulizwe
Ubepari ni Unyama! Maisha ya Ubepari ni magumu.. tumeona juzi Ufaransa na yameshaonekana Uingereza, Ujerumani na hapa Marekani... kweli kabisa katika ubepari wapo watu wanaotanua na kufanikiwa. Jambo moja ambalo watu wengi wamesahau kuwa msingi hasa wa ubepari ni unyonyaji wa mfanyakazi! Leo watu wanalalamikia mafao, wengine wanalalamikia hali ngumu ya kazi, wakati huo huo wanaambiwa "uchumi unakua" na hawaelewi inawezekanaje? Well.. katika ubepari uchumi na unakua kwa kupunguza maslahi ya mfanyakazi! Ndio asili hasa ya ubepari. Wale ambao walipitia somo la Political Economy pale Sangu kwa ndugu yangu Mwl. Mwambene watakumbuka vizuri sana hili..
Njia pekee ya kuondokana na unyonyaji ilipendekezwa na kina Max, Lenin, na ikaja kuwa modified na kuelezewa vizuri zaidi na Mwalimu Nyerere... ukikubali ubepari na maua yake ya mafanikio, ubunifu, utajiri n.k ni lazima ukubali pia na miiba yake...