Msimlaumu Sana Magufuli - Ubepari Ni Unyama Msisahau

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
1544130434309.png

Wanataka Bei ya vitu iwe ile ile miaka nenda rudi - sukari, chumvi, mafuta vyote visibadilike bei hata kidogo (iwe kuakisi hali ya uchumi au vinginevyo)..
Wanataka kampuni zisife
Wanataka watu wasipoteze ajira
Wanataka benki zisifungwe kea kukosa mitaji
Wanataka Kila mtu awe nacho asiwepo aliyepungukiwa
Wanataka benki zifanye kazi tu; zikitakatisha fedha zisiulizwe

Ubepari ni Unyama! Maisha ya Ubepari ni magumu.. tumeona juzi Ufaransa na yameshaonekana Uingereza, Ujerumani na hapa Marekani... kweli kabisa katika ubepari wapo watu wanaotanua na kufanikiwa. Jambo moja ambalo watu wengi wamesahau kuwa msingi hasa wa ubepari ni unyonyaji wa mfanyakazi! Leo watu wanalalamikia mafao, wengine wanalalamikia hali ngumu ya kazi, wakati huo huo wanaambiwa "uchumi unakua" na hawaelewi inawezekanaje? Well.. katika ubepari uchumi na unakua kwa kupunguza maslahi ya mfanyakazi! Ndio asili hasa ya ubepari. Wale ambao walipitia somo la Political Economy pale Sangu kwa ndugu yangu Mwl. Mwambene watakumbuka vizuri sana hili..

Njia pekee ya kuondokana na unyonyaji ilipendekezwa na kina Max, Lenin, na ikaja kuwa modified na kuelezewa vizuri zaidi na Mwalimu Nyerere... ukikubali ubepari na maua yake ya mafanikio, ubunifu, utajiri n.k ni lazima ukubali pia na miiba yake...
 
Ni kweli maana ubepari ni uchumi wa nchi na mfumo wa siasa ambapo katika nchi biashara na viwanda vinahodhiwa na watu binafsi au wafanyabiashara na faida zinakuwa ni zao badala ya nchi hiyo.

Kuna aina nyingi za uchumi ukiwemo ule wa uchumi wa masoko huru au free market economy.

Suali la kujiuliza ni kwamba Tanzania mpaka sasa inafuata uchumi upi?
 
Ni kweli maana ubepari ni uchumi wa nchi na mfumo wa siasa ambapo katika nchi biashara na viwanda vinahodhiwa na watu binafsi au wafanyabiashara na faida zinakuwa ni zao badala ya nchi hiyo.

Kuna aina nyingi za uchumi ukiwemo ule wa uchumi wa masoko huru au free market economy.

Suali la kujiuliza nikwamba Tanzania mpaka sasa inafuata uchumi upi?

Kinachoitwa "free market economy" ndio ubepari wenyewe huo
 
SERIKALI YA CHINA INASAIDIA WAWEKEZAJI WAKE WAKIJA HUKU KWETU LAKINI SERIKALI YETU HAISAIDII WAWEKEZAJI WAZALENDO WANAOSHINDANA NA WAWEKEZAJI TOKA NCHI ZA NJE!!! MABENKI KWA MFANO YANAYOKUJA KUWEKEZA HAPA YANASAIDIWA MITAJI TOKA HUKO KWAO NA SISI HAPA UNATEGEMEA KUTOKAN NA HALI YA NCHI YEYU SERIKALI INGEKUWA INATOA AFUENI KIDOGO KWA BENKI ZETU WENYEWE ZIWEZE KUIMARIKA; BADALA YA KUZIWEKEA MASHARTI MAGUMU NA HATA KUZIFUNGA!!
 
Ubepari ndo unamfanya atunze hela ya nchi kama ya familia yake?

Ubepari ndo unamfanya apigane vita ya uchumi kwa kutumia jeshi nalala ya principles?

Ubepari ndo unasababisha asisikilize washauri?

Naamini hili ni kosa kubwa; Magufuli anachofanya ni kuulazimisha uchumi umtumikie Mtanzania.. ni kama mtu anaamua kusukuma gari lililokwama kwenye matope.. wakati mwingine anatumia nguvu kubwa sana ya misuli hadi pale litakapokwamuka ndio ashughulikie injini.. na matatizo ya gari lile..
 
SERIKALI YA CHINA INASAIDIA WAWEKEZAJI WAKE WAKIJA HUKU KWETU LAKINI SERIKALI YETU HAISAIDII WAWEKEZAJI WAZALENDO WANAOSHINDANA NA WAWEKEZAJI TOKA NCHI ZA NJE!!! MABENKI KWA MFANO YANAYOKUJA KUWEKEZA HAPA YANASAIDIWA MITAJI TOKA HUKO KWAO NA SISI HAPA UNATEGEMEA KUTOKAN NA HALI YA NCHI YEYU SERIKALI INGEKUWA INATOA AFUENI KIDOGO KWA BENKI ZETU WENYEWE ZIWEZE KUIMARIKA; BADALA YA KUZIWEKEA MASHARTI MAGUMU NA HATA KUZIFUNGA!!

Unafikiria China hawafungi benki zinazojiendesha kwa hasara au kwa matatizo? China ina jaribu kutengeneza ubepari kwenye ujamaa.. na inaonekana kushindwa.. Bila nguvu za jeshi na polisi China isingekuwa China..
 
View attachment 958583

Wanataka Bei ya vitu iwe ile ile miaka nenda rudi - sukari, chumvi, mafuta vyote visibadilike bei hata kidogo (iwe kuakisi hali ya uchumi au vinginevyo)..
Wanataka kampuni zisife
Wanataka watu wasipoteze ajira
Wanataka benki zisifungwe kea kukosa mitaji
Wanataka Kila mtu awe nacho asiwepo aliyepungukiwa
Wanataka benki zifanye kazi tu; zikitakatisha fedha zisiulizwe

Ubepari ni Unyama! Maisha ya Ubepari ni magumu.. tumeona juzi Ufaransa na yameshaonekana Uingereza, Ujerumani na hapa Marekani... kweli kabisa katika ubepari wapo watu wanaotanua na kufanikiwa. Jambo moja ambalo watu wengi wamesahau kuwa msingi hasa wa ubepari ni unyonyaji wa mfanyakazi! Leo watu wanalalamikia mafao, wengine wanalalamikia hali ngumu ya kazi, wakati huo huo wanaambiwa "uchumi unakua" na hawaelewi inawezekanaje? Well.. katika ubepari uchumi na unakua kwa kupunguza maslahi ya mfanyakazi! Ndio asili hasa ya ubepari. Wale ambao walipitia somo la Political Economy pale Sangu kwa ndugu yangu Mwl. Mwambene watakumbuka vizuri sana hili..

Njia pekee ya kuondokana na unyonyaji ilipendekezwa na kina Max, Lenin, na ikaja kuwa modified na kuelezewa vizuri zaidi na Mwalimu Nyerere... ukikubali ubepari na maua yake ya mafanikio, ubunifu, utajiri n.k ni lazima ukubali pia na miiba yake...
Huyo jamaa yako lazima alaumiwe kwa kuharibu uchumi wetu.
 
Watetezi wa jiwe mnateseka mno hadi huruma ! huyu mtu hateteeki , halafu mnamlisha maneno tu , hivyo vitabu vyenu wala hata hasomi yeye analowaza ndio anasonga nalo , jenga ukuta , bangua korosho kwa meno , kamata Mbowe , kamata Mello , Tandika Lissu , Teka wahindi etc
 
Ubepari ndo unamfanya atunze hela ya nchi kama ya familia yake?

Ubepari ndo unamfanya apigane vita ya uchumi kwa kutumia jeshi badala ya principles?

Ubepari ndo unasababisha asisikilize washauri?
Hahaha asee siku hizi nafarijika sana kuona wewe uliekuwa mtetezi namba moja wa mauzauza ya mkulu na Lumumba ukiwa unatoa majibu yanayoonyesha ukomavu wa akili na uhalisia wa mambo.

I hope utakuwa role model kwa vijana wengine mliokuwa nao hapo kwa slow slow mo.
 
Wanaotaka ubepari na kulaani ujamaa ndio wanao ongoza kulalamikia kupuuzwa maslahi ya wafanyakazi!!!!
 
Back
Top Bottom