UJAMAA wa Tanzania (Tanzanian Socialism) vs UBEPARI (Capitalism).

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,105
3,619
Je, ni mfumo gani ni bora, unaoweza kuharakisha maendeleo katika nchi za Kiafrika, kati ya ujamaa na ubebari?

Zifuatazo ni baadhi ya sifa za mifumo hii miwili;

Zingatia;
Sifa za Ujamaa zimeegemea katika Ujamaa wa Tanzania-mfumo ambao ulitumika miaka ya 1967 mpaka miaka 1980.

Tahadhari;
Naandika mada hii kutoka katika vyanzo vya masimulizi na maandiko.

Nimezaliwa enzi za Mwinyi, kwa hiyo walioishi katika Ujamaa au wenye mawazo mapana wanaweza kukosoa.

SIFA ZA UJAMAA;

•Vyanzo vyote vya uzalishaji mali kumilikiwa na serikali. Kwa mfano, shirika la ndege, reli, mabasi, viwanda mbalimbali nk. Kwa maneno mengine tunaweza kusema, sekta binafsi haina nafasi katika Ujamaa. Ni sekta ya serikali tu ndiyo inayofanya kazi ndani ya nchi.

• Mfumo wa chama kimoja. Vyama vingi vya siasa haviruhusiwi. Hii ina maana kuwa, uchaguzi uhusisha mgombea mmoja tu kutoka chama kimoja, ambaye atapigiwa kura ya ndiyo au hapana. Na ikitokea kura za "hapana" zimeshinda, basi ataletwa tena mgombea mwingine, japo ni ngumu sana mgombea kushindwa ukizingatia, wanaohesabu kura wapo chini ya mtawala.

• Watu wachache sana, ndiyo hufanya maamuzi kwa niaba ya wengi. Kwa mfano, nchi ina wananchi milioni 40, basi viongozi hata 5 wanaweza kukaa, kupanga na kuamua kwa ajili ya Taifa zima, na hakuna kupingwa.

• Hairuhusiwi kumiliki mali zaidi ya kipato chako. Wanaomiliki mali nyingi huchunguzwa sana, na mali inaweza kutaifishwa au hata mtu kufungwa ikibainika ameipata mali kinyume cha sheria za Ujamaa. Kwa mfano, mtumishi unalipwa mshahara wa laki mbili, halafu umejenga nyumba ya milioni 20 ndani ya mwaka mmoja, basi utachunguzwa tu hata kama uliipata kihali kama vile kulima. Katika Ujama, kumiliki mali zaidi ya wengine ni dhambi.

• Kuhimiza haki na usawa. Katika Ujamaa, watu wote ni sawa, hivyo matabaka hayaruhusiwi. Kwa mfano, usawa katika kupata elimu, huduma za afya nk.

• Ujamaa unahubiri umoja na mshikamano. Yaani changu ni chako, chako ni changu.

• Pia, watu kuishi pamoja katika vijiji vya ujamaa, huku wakizalisha pamoja. Kwa mfano, linakuwepo shamba la kijiji ambalo wanakijiji wote wataenda kulima na mazao yatagawanywa kwa wote.

SIFA ZA UBEPARI;

• Katika ubepari, sekta binafsi inaruhusiwa na kuheshimika sana sana, huku serikali ikibaki kama msimamizi. Watu wenye mitaji wanaruhusiwa kumiliki uchumi wa nchi, kwa mfano kuanzisha viwanda. Sekta binafsi inaruhusiwa ili kuzalisha ajira, kuongeza pato la serikali kupitia kodi, kuboresha huduma ndani ya jamii. Chukulia mfano mdogo tu, kuna kampuni zaidi ya 30 zinatoa huduma inayofanana, je, unahisi huduma itakuwa nzuri au mbaya?

• Ushindani huru katika biashara ni sifa mojawapo katika ubepari. Kwa mfano, serikali haiwezi kuzibana sekta binafsi huku na yenyewe ikifanya biashara. Kufikiri kidogo tu, mtu amekopa benki afanye biashara lakini anashindana na serikali ambayo ina mtaji wa kutosha kutoka vyanzo mbalimbali kama vile kodi.

• Mfumo wa vyama vingi unaruhusiwa katika ubebari, ambapo chama tawala kinaweza kukosolewa na vyama vya upinzanu bila shida. Hapa, ndipo kanuni za demokrasia zinafanya kazi, kama vile; Uhuru wa kutoa maoni kwa raia, uhuru wa kugombea au kupiga kura bila kuamrishwa, uchaguzi huru na haki, nk.

• Katika ubepari mtu anao uhuru wa kumiliki mali ambayo ameipata kihalali. Kwa hiyo, ni juhudi za mtu mwenyewe kufanya kazi kwa bidii, na kutumia ujira alioupata kumiliki anachokitaka kwa mujibu wa sheria, mfano kununua bunduki, kuanzisha viwanda, kujenga majumba nk.

• Pia, kiwango cha ubinafsi, ni kikubwa sana katika ubepari. Yaani, changu ni changu, chako ni chako.

• Unyonyaji ni sifa mojawapo ya ubepari ambapo matajiri huwanyonya maskini.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu, naona mfumo mzuri ni wa kibepari wenye chembe ndogo sanaa za Ujamaa.

Mfumo wa kibebari huharakisha maendeleo kupitia mambo mbalimbali; Kwa mfano, sekta binafsi huzalisha ajira, na kuboresha huduma mbalimbali kwa sababu kunakuwa na ushindani.

Pia, ubebari huziamsha akili za mwanadamu. Hakuna mchezo katika maisha ya kibepari. Mtu mwenyewe unapambana ili upate ridhiki. Hakuna kitu cha bure. Ujamaa unadumaza akili tena sana. Chukulua mfano, mtu anavuta kwa raha zake halafu anakuomba hela ya kununulua sigara!

Tulifundishwa kuwa, ubepari ni unyonyaji! Je, hakuna unyonyaji katika Ujamaa? Vipi mnazalisha halafu watu wachache ndiyo wanapanga matumizi ya mlichozalisha, huo siyo unyonyaji?

Mwenye uzoefu na hizi nchi ambazo bado zinasemekana zina Ujamaa lakini zina maendeleo kama vile China, angetueleza wao wanaendesha vipi huo Ujamaa?

Je, serikali ya China hufanya biashara?

Je, hakuna kampuni binafsi nchini China? Kama zipo, zinajiendesha vipi katika Ujamaa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom