Msimlaumu Sana Magufuli - Ubepari Ni Unyama Msisahau

Hujui lolote wewe , hakuna unyama mbaya kama ujamaa sasa kama ujui , fuatilia nchi za kijamaa uone raia wake wanavyosuffer na viongozi wanaishi kwa raha
 
Kwanza punguza hasira na uwe una Edit kabla ya kupost

Huyu bwana mabadiliko kama ulivyomuita. Ni kweli awamu ya nne ilikuwa na mapungufu yake, lakini angalau watu waliwekewa mazingira bora kidogo ya kufanya kazi. Angalau masikini nao walikuwa wanapata harufu ya michuzi. Siyo hii hali iliyowakumba wafugaji, wavuvi , wafanyakazi etc maeneo mbalimbali. Hebu tembelea kada hizo tatu nilizokutajia, uone kama kuna mtu ana hamu na awamu ya tano. Wamefilisiwa kwa kunadiwa vitu vyao bila kuhukumiwa kisheria bali kwa matamko.
Sasa kama unajenga nchi kwa kuvuruga uchumi wa wananchi wenyewe si ni kupiga marktime hapo ?!.

Pili 2015 watu hawakuwahi kupendekeza u dictator, Bali walitaka katiba mpya, democracy zaidi, na Tanzania bora kwa watu wote.
 
Unafikiria China hawafungi benki zinazojiendesha kwa hasara au kwa matatizo? China ina jaribu kutengeneza ubepari kwenye ujamaa.. na inaonekana kushindwa.. Bila nguvu za jeshi na polisi China isingekuwa China..
Sidhani kama china wameiba fedha za mafao za wafanyakazi wao
 
Mzee Mwanakijiji..

Ni kosa kupora mafao

FAO LA kujitoa

Mafao ya Wazee

Wabunge na Vigogo wanapewa 100% ..

Ujamaa gani huu? Shame to them

Hata mabepari hayawezi kufanya wizi huu mchana kweupe

Wafanyakazi watakosa morali...watakata tamaa..

Kodi atapata wapi, kama uzalishaji ukipungua...
 
Uchumi ulishaharibika ila ulikuwa unakwenda tu..utakaposahihishwa vizuri na kuanza kujiendesha mtasahau yote haya na tumshukuru Mungu
Kama unachosema ni kweli au ni sanaa za kisiasa tutafahamu huko mbeleni inshaaallah.
 
WACHINA HUZISAIDIA BENKI ZAO KUIMARIKA NI ZILE AMBAZO HAZIWEZI KUJIIMARISHA NDIO ZINAFUNGWA!!! SISI HAPA HATUZIPI NAFASI BENKI ZETU HASA ZA WAZAWA NAFASI YA KUWEZA KUJIIMARISHA HATA PALE WANATOA MPANGO WAO WA KUWEZA KUJIIMARISHA!!
Hizi fikra za utegemezi pamoja na kupata elimu ili tujikwamue naona zimekataa kabisa kutuondoka sisi watanzania, yaani kila kitu tunailaumu serikali na kutegemea itufanyie kila jambo.
 
Kuna neno Petty capitalism. Hao ndiyo wale wanatumia mabenki kutakatisha pesa na wahongaji kupata tenda na wakwepa kodi na wanaopewa dili kindugu nk. Watu wanafikiri huu ndiyo ubepari. Na mtoa mada anafikiri huo ndiyo ubepari.

Kiufupi ujamaa ni mfumo nyonyaji kuliko ubepari.
 
Mzee Mwanakijiji ni kweli kabisa,upepari ni unyama.Watu wakisikia Marekani na Ulaya wanadhani all is well.Kwenye ubepari uliokolea kama Marekani na Uingereza picha iko wazi.Check the following clip,you cannot believe this is happening in a country which boasts itself of being the most developed.


 
Unaonesha gross misunderstanding of my points..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…