Msimlaumu Sana Magufuli - Ubepari Ni Unyama Msisahau

Let me put it bluntly, Mwananikiji is simply an hypocrite. Anaushangilia ujamaa wakati yeye na familia yake wananufaika na ubepari. Ni kweli kuwa hakuna mfumo ulio perfect hapa duniani ila ubepari una unafuu mara mia dhidi ya ujamaa.

Mfumo wa ubepari umejikita kwenye uhalisia wakati ujamaa uko zaidi kwenye hisia. Na mbaya zaidi sehemu zote ambapo ujamaa umejaribiwa 100% nchi hizo zimejikuta kwenye matatizo makubwa. Angalia taifa la Venezuela kabla na baada ya Chavez ku-embrace ujamaa. Sababu kubwa ni kuwa serikali nyingi hapa duniani haziko effective kutokana na kukosekana kwa ushindani wa biashara (monopoly). Kitu hiki kinapelelekea huduma nyingi zinazoletewa na serikali kuwa chini ya kiwango ukifananisha kama za sekta binafsi. Ndio maana Rais Regan aliwahi kuwaasa Wamarekani kuwa "serikali sio suluhu ya matatizo yao kwani serikali yenyewe ni tatizo."
 
Hawa watu wa ajabu sana. Wanaonea fahari uchumi uliokuwa mahututi, uchumi uliokuwa umejaa pesa nyingi unaccounted for; pesa za rushwa, magendo, wizi, ukwepaji kodi, mauzo ya unga, utakatishaji, nk, eti ndo wanaona kilikuwa kitu cha kujinia.
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hawa watu wengine ni wasomi kabisa! It sucks when educated people act the same way as uneducated.
How come sasa uncounted economy ulikuwa unasoma average economic growth rate ni between 6.7%-7% na hiyo counted economy bado inacheza hapo hapo?!

How come uncounted economy iliacha deni la taifa ambalo ni very manageable na hii counted economy ikiendelea kuongeza deni la taifa kwa kasi ya ajabu?

Hii shilingi ambayo bado inaendelea kuporomoka ni matokeo ya uncounted au counted economy?!

Mnahitaji miaka mingapi kuonesha positive impact ya hiyo accounted economy yenu baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa 3+ years?!

Hivi kabisa mtu unaweza kutoka mbele na kusifia uchumi usiozalisha ajra lakini badala yake unapukutisha ajira??

Hivi unaweza kusifia uchumi unaoshindwa hata kuajiri walimu na madaktari wakati walimu na madaktari wamejaa mitaani kibao huku mashule yakikosa walimu na mahospitali kukosa madaktari wa kutosha?

Hivi mnapata wapi ujasiri wa kusifia uchumi unaotumia mabilioni ya pesa za serikali kwenda kujenga international airport kijijini ambako hakuna any airline commercial and/or economic viability tena tenda ikiwa imetolewa kiushikaji?!

Uchumi uliokuwa umejaa rushwa huku ukiendeshwa na dawa za kulevya ulikuwa ume-highlight tatizo la msingi la ukosefu mkubwa wa walimu wa sayansi kwenye shule za msingi na sekondari. Kwa kuona hilo, ikaanzishwa 3 years special diploma program... science na mathematics!

Now tell me, baada ya uchumi wenu unaotakiwa kushangiliwa kwa nyimbo na mapambio kuona special diploma ile ni upumbavu mtupu; je, hadi sasa kimefanyika nini kuongeza walimu wa sayansi? Mmepandisha mishahara ya walimu wa sayansi ili kuwa-encourage watu wakasomee ualimu wa sayansi au mmefanya nini hasa?

Aidha, ni juzi tu hapa Mzee Mwanakijiji ameshindwa kabisa kunisaidia kwenye ujuha wangu wa kutofahamu how competent this government is! Hebu nielimishe wewe sasa kwa sababu inaonekana wewe na MJJ mnafanana kimtazamo!!

Hapo kabla nilipata kusikia kwamba, popote ambapo grand corruption ilikuwa transacted, two forces must keep the system in equilibrium for such transaction kuwa effected na moja ya hizo forces, ni ama top government executives or high profile politicians au both!

Now tell me: Unaweza kunitajia ONLY 3 top government officials and/or high profile politicians waliofikishwa mahakamani hadi sasa kwa tuhuma za ufisadi kiasi cha kufanya uchumi wetu wa miaka iliyopita kuwa ni uchumi uliotokana na vitendo vya rushwa, magendo n.k?

Btw... who's the economy for?!

Kama huo uchumi wenu usio wa dawa za kulevya wala rushwa unashindwa kutoa ajira hata kwenye sekta nyeti kama afya na elimu; kuna maana gani basi ya kuwa na uchumi wa aina hiyo?! Who's it for?!

Acheni kutetea upumbavu wakati kila mwenye akili timamu anafahamu kuna matatizo makubwa sana ya kiuchumi!! Akina nyie hamna hoja yoyote ya maana zaidi kama alivyosema JokaKuu kwamba, badala ya kutuambia what you have achieved so far, bado mnaendelea kupiga simulizi za kale za kwamba, kila aliyepiga hatua basi alipiga hatua hiyo ama kwa kula rushwa au kuuza dawa za kulevya!

You don't believe in personal hustle, na matokeo yake mnaona kila aliyefanikiwa ni mwizi, mla rushwa, muuza dawa za kulevya, Freemason n.k… mawazo ya kimaskini kabisa! Lakini wakati mtu anaweza kudhani ni wapinga ufisadi kweli kweli, utashangaa wale walio deep inside the circle wanafanya mambo ya hovyo kabisa kiasi cha kutia shaka mzito juu ya uadilifu wao!

Btw, kati ya hayo mabilioni ya rushwa na dawa za kulevya, wewe binafsi uliweka kibindoni bilioni ngapi?! Binafsi,hata senti 5... what about you na wenzako ambao hata baada ya miaka mitatu kupita, bado mnaendelea kujificha kwenye simulizi zile zile miaka nenda rudi!!
 
How come sasa uncounted economy ulikuwa unasoma average economic growth rate ni between 6.7%-7% na hiyo counted economy bado inacheza hapo hapo?!

How come uncounted economy iliacha deni la taifa ambalo ni very manageable na hii counted economy ikiendelea kuongeza deni la taifa kwa kasi ya ajabu?

Hii shilingi ambayo bado inaendelea kuporomoka ni matokeo ya uncounted au counted economy?!

Mnahitaji miaka mingapi kuonesha positive impact ya hiyo accounted economy yenu baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa 3+ years?!

Hivi kabisa mtu unaweza kutoka mbele na kusifia uchumi usiozalisha ajra lakini badala yake unapukutisha ajira??

Hivi unaweza kusifia uchumi unaoshindwa hata kuajiri walimu na madaktari wakati walimu na madaktari wamejaa mitaani kibao huku mashule yakikosa walimu na mahospitali kukosa madaktari wa kutosha?

Hivi mnapata wapi ujasiri wa kusifia uchumi unaotumia mabilioni ya pesa za serikali kwenda kujenga international airport kijijini ambako hakuna any airline commercial and/or economic viability tena tenda ikiwa imetolewa kiushikaji?!

Uchumi uliokuwa umejaa rushwa huku ukiendeshwa za kulevya kama unavyodai, ulikuwa ume-highlight tatizo la msingi la ukosefu mkubwa wa walimu wa sayansi kwenye shule za msingi na serikali. Kwa kuona hilo, ikaanzishwa 3 years special diploma course science na mathematics!

Now tell me, baada ya uchumi wenu unaotakiwa kushangiliwa kwa nyimbo na mapambio kuona special diploma ile ni upumbavu mtupu; je, hadi sasa kimefanyika nini kuongeza walimu wa sayansi? Mmepandishwa mishahara ya walimu wa sayansi ili kuwa-encourage watu wakasomee ualimu wa sayansi au mmefanya nini hasa?

Aidha, ni juzi tu hapa Mzee Mwanakijiji ameshindwa kabisa kunisaidia kwenye ujuha wangu wa kutofahamu how competent this government is! Hebu nielimishe wewe sasa kwa sababu inaonekana wewe na MJJ mnafanana kimtazamo!!

Hapo kabla nilipata kusikia kwamba, popote ambapo grand corruption ilikuwa transacted, two forces must keep the system in equilibrium for such transaction kuwa effected na moja ya hizo forces, ni ama top government executives or high profile politicians au both!

Now tell me: Unaweza kunitajia ONLY 3 top government officials and/or high profile politicians waliofikishwa mahakamani hadi sasa kwa tuhuma za ufisadi kiasi cha kufanya uchumi wetu wa miaka iliyopita kuwa ni uchumi uliotokana na vitendo vya rushwa, magendo n.k?

Btw... who's the economy for?!

Kama huo uchumi wenu usio wa dawa za kulevya wala rushwa unashindwa kutoa ajira hata kwenye sekta nyeti kama afya na elimu; kuna maana gani basi ya kuwa na uchumi wa aina hiyo?! Who's it for?!

Acheni kutetea upumbavu wakati kila mwenye akili timamu anafahamu kuna matatizo makubwa sana ya kiuchumi!! Akina nyie hamna hoja yoyote ya maana zaidi kama alivyosema JokaKuu kwamba, badala ya kutuambia what you have achieved so far, bado mnaendelea kupiga simulizi za kale za kwamba, kila aliyepiga hatua basi alipiga hatua hiyo ama kwa kula rushwa au kuuza dawa za kulevya!

You don't believe in personal hustle n matokeo yake mnaona kila aliyefanikiwa ni mwizi, mla rushwa, muuza dawa za kulevya, Freemason n.k… mawazo ya kimaskini kabisa!

Btw, kati ya hayo mabilioni ya rushwa na dawa za kulevya, wewe binafsi uliweka kibindoni bilioni ngapi?! Binafsi,hata senti 5... what about you na wenzako ambao hata baada ya miaka mitatu kupita, bado mnaendelea kujificha kwenye simulizi zile zile miaka nenda rudi!!
Well argued.

Kama kuna ambaye hajaweza kujifikirisha kwa hoja hizi, siyo tu ni mjinga bali ameamua kufunga ndoa ya kudumu na upumbavu.

Mambo mengi yanayosifiwa katika awamu yamekaa kuhadaa, kudanganya na
Kupumbaza wananchi. Kiuhalisia, jakuna tulicho-achive zaidi ya kupoteza.
 
..nakushauri uelimishe wasomaji wako kuhusu uzuri wa mfumo wa uchumi wa Kijamaa.
Kupitia elimu hiyo wasomaji wataweza kuiona mifumo yote miwili na kuipima. Nadhani MM ataitikia wito

Kwa uelewa wangu wa kibubusa busa mfumo wa ''ujamaa'' uliokuwepo nchini ni wa Nyerere
Waliofuata walikuwa na mchanganyiko sijui niite 'amalgam, fusion au blending'

Mwinyi aliupa kisogo ujamaa bila kutuachia mfumo, ni kama alifungua geti la uwanja watu waingie tu
Mkapa akahitimisha ujamaa kwa kukaribisha ubepari.Kikwete akaendeleza ya Mwinyi na Mkapa akinyunyuzia ufisadi

Swali lisilo na jibu, kwanini Nyerere aliatuachia misingi ya ujamaa tukafeli hata kwa kidogo alichoacha, mfano wa viwanda na mashirika ya umma?
Na kwanini tunadhani bila majibu ya swali hilo tunaweza kurudi kule kule kwa mafanikio?

Na ni nani anaweza kutueleza tuna mfumo gani kwa serikali iliyopo madarakani!
 
How come sasa uncounted economy ulikuwa unasoma average economic growth rate ni between 6.7%-7% na hiyo counted economy bado inacheza hapo hapo?!

How come uncounted economy iliacha deni la taifa ambalo ni very manageable na hii counted economy ikiendelea kuongeza deni la taifa kwa kasi ya ajabu?
..Huu ni mwaka wa 3 kuelekea wa 4 tangu JPM achaguliwe, hivyo basi ni vizuri mkaanza kueleza mafanikio ya utawala wake.
Hoja mujarabu. Jokakuu anasema ni yapi mafanikio ya miaka 3 kuelekea 4 kama ambavyo chige ameonyesha growth rate ikiwa katika kiwango kile kile cha 6.7-7%

Hoja hiyo inashadidiwa na ukweli mwingine, kwamba, serikali inajivunia kuwa na inflation rate katika 5%
Kwanini haielezwi ni vipi growth rate imebaki pale pale
Kwanini hazielezwi stats za Unemployment , ajira ngapi zimetengenezwa na ngapi zimepotea
 
..Haileti picha nzuri kwamba umebaki mwaka mmoja tuingie ktk uchaguzi mkuu halafu bado tunazungumzia mapungufu ya awamu ya 4 badala ya mafanikio ya awamu ya 5.
Hatukuwa na chama tofauti kabla, tulikuwa na sera zile zile za CCM na watu wale wale. Mwaka 1 ulitosha kusafisha mapungufu ambayo si mageni kwa wahusika, waliyajua

Kwasasa tulipaswa kuongelea mafanikio ya miaka 2 iliyopita. Arguably kuna miradi inayoendelea
Je deni la taifa ni sustainable? Tutalilipaje, kwa muda gani na return ipi!
Je mafanikio ya uchumi yamewafikia walengwa na ni yapi!
 
Naendelea kujifunza juu ya Ubepari...
Mkuu MM,

Ni vyema watu waaelewa kuwa Siasa ni Uchumi...

Ombi, tuache ku-generalise hii mifumo ya kiuchumi na kisiasa:

Mosi:
Ujamaa (wa Mwalimu) sio sawa na socialism (Venezuela) wala sio sawa na communism (eg USSR, China ya zamani, DPRK, Cuba).
Pili:
Ubepari pure wa Marekani, Uingereza, Canada etal. sio sawa na Ubepari wa Ujerumani au Nchi za Nordic.

Tatu:
Kuna kitu kinachoitwa 'state capitalism' au compossianate capitlism' huu ndio mfumo wa kisiasa na kiuchumi unaotumika huko Nordic, (Norway, Sweden, Denmark, etal)

Baadhi ya Tafauti Kubwa :
Umiliki wa Nyenzo Kuu za Uchumi - Benki Kuu ktk pure capitalist economies zinamilikiwa na watu binafsi!. While in socialist au state capitalist economies ni Serikali kuu ndio inamiliki hivyo vyombo.

Asilimia Kubwa ya kampuni ktk soko la hisa ktk pure capitalist countries zinamilikiwa na watu binafsi.
Matatizo ya kiuchumi aka mdororo yakitokea ktk pure capitalist economies Serikali husaidia/bailout kampuni binafsi na sio wananchi waathirika (USA, bailout ya banks etc). While tatizo kama hilo ktk socialist au state capitalist economies, Serikali itaanza kusaidia wananchi wake then mengine baadaye.

Most socialist na state capitalist economies zinaweka kitu inaitwa 'fungu la utajiri wa taifa' kimombo National sovereignty wealth fund' (eg Norway) hilo ni kwa niaba ya wananchi wote. Wakati pure capitalist economies hakuna kitu kama hicho.

Vyama vya wafanyakazi - huvikuti hivi ktk most pure capitalist economies lkn utavikuta kkt socialist au state capitalist economies...

Vyama vya siasa na demokrasia - ktk most pure capitalist economies utakuta vyama vikuu vya sisa vichache sana mara nyingi 2 au 3 (Uingereza, USA). While ktk socialist au state capitalist economies huwa kuna uwanda mpana zaidi wa demokrasia kwani huwa kuna vyama vya siasa vingi vilivyo na nguvu zinazoshabibiana.

Je ni Lazima Nchi Zote Zifuate Hio Mifumo?
La hasha, kuna nchi nyingi haifuati hio mifumo na zinafanya vizuri tu. Mfano nchi nyingi za Uarabuni na Uajemi, South Korea, China ya leo etc.
Kwa mfano South Korea wao wana mix mazuri toka ktk mifumo yote na kupata flavor yao ya mafanikio kuwa one of the best and vibrant economy in the world.

Je Tanzania Tunafuata Aina Gani ya Mfumo?

Dalili zote zinaonyesha kuwa tunaelekea ktk mix economy scenario tukichanganya Ubepari, socialism, na state capitalism. Ndio maana bado tuna Benki kuu na mashirika makubwa Chini ya state wakati huo huo tuna vibrant private sector (Akina mzee Mengi etal.) na pia utitiri wa vyama vya Siasa, uchaguzi pamoja na mapungufu yake.

Angalizo, hata kama Nchi ikichagua aina gani ya mfumo haimaanishi Kuwa mafanikio yatakuja magically, inahitaji watu kuwa wabunifu na wa hapa kazi.

My 2 cents.
 
Miaka ya nyuma tulikuwa tumesimama mguu upande sasa tunazoeshwa kusimama mguu sawa ili tuweze kupambana katika ulimwengu halisi wa kibepari.

Wafaransa na jeuri yao ya kuwa karibu na waliowatawala bado wanapambana na waandamanaji wenye hoja za msingi. Tunao manabii wa majanga, ambao wanashindwa kuitazama dunia halisi jinsi ilivyo.

Mambo yalikuwa hovyo huku bwana mkubwa akibembea kule Jamaica sura ikiwa na tabasamu bashasha. Maendeleo ni safari isiyohitaji kukata tamaa.
 
..Magufuli anastahili PONGEZI kwa kuziba mianya ya rushwa na fedha haramu.

..Vilevile anastahili LAWAMA kwa kushindwa kufungua milango ya fedha halali na uchumi shirikishi.

..kwa maoni yangu miaka 3 is enough time to TURN THE ECONOMY AROUND.

..pamoja na kushindwa ku-fix the economy Magufuli amekuja na mambo yake mapya kama CHUKI,UBAGUZI, na UKATILI kwa wapinzani.

..Kwa maoni yangu Uraisi umemshinda Magufuli. This is not what Tanzanians thought they will be getting into when they voted for him.

Cc chige, Malcom Lumumba
 
Mkuu JokaKuu ngoja nikae vizuri ntarudi kuchangia.
 
Wakati mwingine na mimi huwa natamani kumpongeza kwa kuziba mianya ya rushwa lakini wakati mwingine huwa najiuliza ni kweli ameziba mianya ya rushwa au watu hatuna access to what's going on behind the closed door!!!

Hofu yangu inatokana na imani yangu kwamba, ufisadi mwingi ambao ulifahamika wakati wa JK ni kwa sababu kulikuwa na access to information! Huwa najiuliza, hivi lile varangati la Richmond lingetokea zama hizi, hivi wabunge wa CCM wangejimwaya mwaya namna ile bungeni?!

Huwa najiuliza hivi balaa kama lile angefanya mtu kama Paul Makonda, hivi kweli sakata lingepelekwa bungeni na kujadiliwa kwa uwazi!!!

Huwa najiuliza balaa lile la Escrow lingetokea zama hizi, hivi kweli watu wangetamba bungeni hadi kufikia kuitana tumbili!!

Hofu yangu nyingine ni kwamba bado nina kumbukumbu za utawala wa Benjamin Mkapa! Hivi Malcom Lumumba unakumbuka kidogo ya Mkapa?!

Nakumbuka bwana yule alikuwa anajiita Mr. Clean... na kweli, jina la Mr. Clean lilinoga kweli kweli! Huku akijiita Mr. Clean, upande mwingine alikuwa anajigamba serikali yake ni ya ukweli na uwazi! Hili la Mr. Clean na Ukweli na Uwazi yalinoga kweli kweli!!

Pamoja na yote hayo, serikali ya Mkapa haikuwa wazi kiasi hicho! Isitoshe Mkapa alikuwa mkali kweli kweli!

Ingawaje linapokuja suala la uwazi serikalini Mkapa was far better compared to Magufuli, lakini sikumbuki kama serikali yake iliwahi kukumbwa na kashfa kubwa ya ufisadi...! Alipotoka sasa... bomu moja baada ya lingine likaanza kuripuka na kuonesha uozo uliokuwa umefichika wakati wa serikali ya Mkapa! Hilo ndilo ninalohufu kuja kutokea baada ya Magu kutoka madarakani!

Lakini hata kama kweli Magufuli amedhibiti suala la ufisadi; mimi bado nina tatizo nae moja ambalo nimeshawahi kuhoji hapa jamvini kwamba, hivi huyu Magufuli ni kweli analenga kuisaidia Tanzania au analenga kujenga legacy yake yeye binafsi!!!

Huwezi kupambana na ufisadi wewe kama wewe... ufisadi unapigwa na mifumo thabiti itakayodumu kwa miongo kadhaa! Kinyume chake, Magufuli anapambana na ufisadi yeye kama yeye na sio kwa kutumia mifumo! Matokeo yake, hata kama atafuta ufisadi kwa 100%, a moment anatoka Ikulu ufisadi utarudi kwa kasi ile ile... itakuwa kama fungulia mbwa!

Mwalimu Nyerere alipambana na ufisadi yeye kama yeye! Hapakuwa na mifumo imara ya kupambana na ufisadi! Matokeo yake, wakati wa Nyerere wale ambao hawakufanya ufisadi si kwa sababu waliuchukia ufisadi au waliogopa mifumo ya kupambana na ufisadi bali walifanya hivyo kwa kumhofia Baba wa Taifa kama ambavyo leo hii watu wasivyofanya ufisadi (kama kweli) si kwa sababu wanauchukia ufisadi bali kwa sababu wanamuogopa Magufuli!

Matokeo yake, kama nilivyosema hapo juu, akitoka tu madarakani ufisadi unarudi kwa kasi ya kutisha unless aje mtu mwenye haiba yake!! Ni kutokana na hayo, ndo maana siachi kujiuliza ikiwa lengo lake ni kuisaidia Tanzania au kujenga legacy yale ili hapo baadae aendelee kukumbukwa kwa hoja kwamba serikali yake haikuwa ya wala rushwa kama ambavyo tunaweza kuumbuka utawala wa Mwalimu!!!

Lakini jambo lingine, hivi unapambana vipi na ufisadi wakati mizizi mikuu ya ufisadi imebaki tu mtaani... kwa sasa imepukutisha tu majani ikisubiri japo mvua za rasharasha zianze tena kunawiri!! Mimi sitaki kuamini kwamba serikali ya JK na ya Mkapa haikuwa na viongozi mafisadi! Unawaacha vipi watu kama hawa halafu unatamba kwamba unapambana na ufisadi?! Unapambana vipi na ufisadi wakati miongoni mwa hawa mafisadi wengine bado wapo serikalini?! Na excuse kwamba haina haja ya kufukua makaburi kwangu ni excuse isiyo na maana yoyote! Mbona akina Rugemalila wapo selo kwa tuhuma za makaburi yaliyopita?! Wako wapi waliowasaidia akina Rugemalila kuchota pesa za Escrow?!

Ukweli ni kwamba, Magufuli ameonesha wazi kwamba hana gut ya kupambana na high profile politicians as well as watendaji wakuu wa serikali! Au bado miaka 3 ni michache sana kuiwezesha serikali yake kuwafahamu wanasiasa na watendaji wakuu wa serikali ambao waliibia sana hii nchi?!
 
JokaKuu, post: 29544170, member: 221"]..Magufuli anastahili PONGEZI kwa kuziba mianya ya rushwa na fedha haramu.
Mambo hayo yamejenga nidhamu, kupunguza pesa nje ya mfumo na huenda ndiyo yanayopelekea inflation kuwa chini.
..Vilevile anastahili LAWAMA kwa kushindwa kufungua milango ya fedha halali na uchumi shirikishi.
Hotuba yake kwa wafanyabiashara ilikuwa na matumaini sana. Alichokitaka ni biashara au shughuli halali na kuwajibika kulipa kodi au tozo nyingine kwa mujibu wa sheria
..kwa maoni yangu miaka 3 is enough time to TURN THE ECONOMY AROUND.
Kwa ukweli kuwa hakutoka nje ya 'system', alijua mafanikio na udhaifu kutoka kwa BWM hadi kwa JK.

Mahakama ya mafisadi ilianzishwa mara moja kwasababu ilijulikana inahitajika kukabiliana na ufisadi. Hili si wazo jipya , ni maboresho ya udhaifu aliouona na kuukuta.
Kwa mwaka 1 ulitosha kuweka mambo sawa na sasa tungeona mabadiliko ya uchumi
..pamoja na kushindwa ku-fix the economy Magufuli amekuja na mambo yake mapya kama CHUKI,UBAGUZI, na UKATILI kwa wapinzani.
Mambo hayo yanafunika 'agenda' hata zile nzuri zinazofanyika.

Ingekuwa nchi zenye uchaguzi huru na wa haki, ingelikuwa tabu sana kuchaguliwa tena.
Agenda zingefunikwa na mambo mengine ambayo wapiga kura ni rahisi kuyaona kama ulivyoyaorodhesha. Kule US, hali ya uchumi ni nzuri lakini republicans wamepoteza midterm elections ikielezwa, mazonge zonge ya Trump yamefunika agenda ya uchumi

Madhara ya mambo chuki, ubaguzi n.k. ni kukosa 'national unity' na kujenga msingi mbaya siku za usoni kama Taifa.
Tukianza misingi ya chuki, kubaguana na kutendeana ubaya inakuwa ni 'precedent'

Kwasasa hivi tunaona tofauti kwasababu tulikuwa na template kuanzia enzi za mwalimu
Moja ya mafanikio ya Mwalimu ilikuwa kujenga utaifa na misingi ya umoja kwa kupendana
Kupendana si 'mahaba' ni kiungo muhimu cha muafaka(consensus) kinachosukuama mbele agenda za kitaifa, mshikamano na kuimarisha utaifa na uzalendo
This is not what Tanzanians thought they will be getting into when they voted for him.
Wengi walimuelewa kama kiongozi atakayesimamia sheria kwa rekodi yake.
Kiongozi atakayekuwa na maamuzi magumu na asiyeyumbishwa, anayesimamia sheria kama zilivyo na kuzingatia haki.Hivyo walitoa benefit of doubt kwa kudharau kauli ya Rais Lincoln wa Marekani 'If you want to test man's character give him power''
 
Hoja mujarabu. Jokakuu anasema ni yapi mafanikio ya miaka 3 kuelekea 4 kama ambavyo chige ameonyesha growth rate ikiwa katika kiwango kile kile cha 6.7-7%

Hoja hiyo inashadidiwa na ukweli mwingine, kwamba, serikali inajivunia kuwa na inflation rate katika 5%
Kwanini haielezwi ni vipi growth rate imebaki pale pale
Kwanini hazielezwi stats za Unemployment , ajira ngapi zimetengenezwa na ngapi zimepotea
Economic Indicators nyingi zinashawishi kinyume na kile kinachoimbwa kila siku! Na hata zile positive indicators zinazoonekana kwenye uchumi huu zinakuwa highly contributed na existing poor economic performance! Kwa mfano, ni kwavipi inflation isishuke wakati purchasing power imepungua kutokana na kufa kwa ajira nyingi na kutozaliwa kwa ajira mpya at the same proportionality?!
 
Ninakusoma vizuri mkuu.

Unanikumbusha tunapopewa stats za ajira zilizotengenezwa bila kuambiwa zilizopotea!

Inawezakanje kutengeneza ajira 3000 kwa kiwanda na kudhani ni mafanikiowakati kampuni zinapukutisha watu kila siku na waajiri wakubwa wanafunga biashara!

Nadhani sheria ya takwimu inalenga kutofichua mambo kama hayo ya inflation , purchasing power, unemployment n.k.
 
Ubepari sisi waafrica ndo tunautaja sababu ya kudanganyana kwenye vitabu vya historia. Sasa hivi wenzetu hawaongelei capitalism wala imperialism wao wana survival of the fittest. Ukiwa una nguvu ndo utaishi nyie ng'ang'anieni sera zenu za ujamaa usiyokuwa na kichwa wala miguu na kubaki kuwaita wenye nguvu mabepari. Upuuzi huu ndiyo tunafundisha mpaka watoto wetu wanakuwa na ujinga tukidhani tunawaelimisha kumbe tunawakaririsha zama zilizopita.

Dhana ya ubepari na ubeberu itabaki kwenye historia tu sasa hivi mambo yamebadilika mwenye nguvu ya teknolojia ndo anaikimbiza dunia. Tukicheza tutaingia karne ya 22 na mindset za kuita watu mabepari kwa gharama ya umaskini wetu mkubwa. Kinachoivuruga ufaransa si ubepari bali ni uongozi mbaya ambao wananchi wameghafilika hawaitaki serikali tena.

Tofauti na wao sisi hata uongozi ukipiga marufuku kulala na wake zetu bado tutakaa kimya kwasababu tumeelewa demokrasia lakini tumeielewa vibaya.
 
Ninakusoma vizuri mkuu.

Unanikumbusha tunapopewa stats za ajira zilizotengenezwa bila kuambiwa zilizopotea!

Inawezakanje kutengeneza ajira 3000 kwa kiwanda na kudhani ni mafanikiowakati kampuni zinapukutisha watu kila siku na waajiri wakubwa wanafunga biashara!

Nadhani sheria ya takwimu inalenga kutofichua mambo kama hayo ya inflation , urchasing power, unemployment n.k.
Hahahaaa! Wakuu Malcom Lumumba na JokaKuu vijijini kwenu kumejengwa viwanda vingapi???!!!

Mkuu Nguruvi3 ulipotaja suala la viwanda ukanikumbusha hivi majuzi nilipoamua kutafuta kufahamu hivi viwanda tunavyoambiwa vinajengwa vimejengwa wapi hasa!! Nilikuwa nimeshangazwa na idadi ya viwanda 52K vilivyotajwa na kujiuliza mbona matokeo ya hivi viwanda hayaonekani kwenye vigezo vya ukuaji wa uchumi!!

Baada ya kuhangaika sana ndipo nilipopata document kutoka National Bureau of Statistics huku ikiwa imeorodhesha viwanda vyote 52K+!! I was surprised nilipokuta eti kijijini kwetu kuna viwanda 15!!! Na kwa kasi hii, bila shaka hadi sasa vimeshafika 20... ! Bila shaka umefahamu naongea nini sasa!! Yaani ni full utani kwenye uchumi!
 
Hofu yangu nyingine ni kwamba bado nina kumbukumbu za utawala wa Benjamin Mkapa! Hivi Malcom Lumumba unakumbuka kidogo ya Mkapa?!
Wazungu walivyoamua kutengeneza taasisi miaka zaidi ya 600 iliyopita waliona mbali sana:kitu pekee kinachoweza kutunza mafanikio ya kiongozi kwa muda mrefu ni taasisi tu. Kuna ile ripoti ya Jaji Warioba mwaka 1997 ilionesha madudu mengi sana ya serikali ya Mzee Mkapa lakini aliamua kupuuza na kuiweka kapuni.

Moja ya njia ya kupambana na rushwa ni kuruhusu uwazi, ukweli na kujenga taasisi kitu ambacho Raisi Magufuli sidhani kama ana hulka nacho. Hivyo haya mambo ni suala la muda tu, yatalipuka: Hivyo kama tunashindwa kabisa kupambana na Rushwa basi tuwaige Romania ambao walisime wanataka kuhalalisha rushwa ya hadi dola 50000 za kimarekani. Teh teh teh teh

Mkuu Chige hebu cheki hapa: Romania Has Essentially Made Corruption Legal
 
Baada ya kuhangaika sana ndipo nilipopata document kutoka National Bureau of Statistics huku ikiwa imeorodhesha viwanda vyote 52K+!! I was surprised nilipokuta eti kijijini kwetu kuna viwanda 15!!! Na kwa kasi hii, bila shaka hadi sasa vimeshafika 20... ! Bila shaka umefahamu naongea nini sasa!! Yaani ni full utani kwenye uchumi!
Hahahahah yaani Mkuu ulienda kabisa kuchukua takwimu za NBS Chige au unatania ??? Mimi siku hizi nimegundua mchezo mzuri tu: Siamini chochote kile ambacho serikali inasema, ntatafuta ukweli wangu mwenyewe huko nakojua. Maana unaweza ukadanganywa halafu na wewe ukaja kutia aibu mbele za watu
 
Back
Top Bottom