UZUSHI Msimbo (Code) wa rangi kwenye kasha la dawa za Meno huonesha aina za kemikali zilizotumika kutengeneza dawa hiyo

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
1702564182_new-project-2023-12-14t195829-005.jpg


Kumekuwepo na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa makasha ya dawa za meno huwa na rangi (code) za aina mbalimbali zinazofafanua aina ya kemikali zilizotumika kutengenezea dawa hiyo.

Aidha, madai hayo yanafafanua zaidi kuwa kemikali husika ni hatari kwa afya na husababisha saratani, na kwamba makampuni yanayozalisha dawa hizi hayawezi kukupa siri hii.

Ukweli wake upoje?
 
Tunachokijua
Dawa ya meno ni bidhaa ya kisayansi inayotumiwa pamoja na mswaki kusafisha na kudumisha uzuri na afya ya kinywa na meno.

Pamoja na uwepo wa kampuni tofauti zinazotengeneza dawa ya meno, muundo wa kikemikali unaotumika kwenye utengenezwaji wake hufanana kwa kiasi kikubwa.

Kwa ujumla wake, pamoja na uwepo wa viambato vingine, dawa za meno hutengenezwa kwa kutumia maji, kemikali mbalimbali, sabuni, madini ya fluoride na rangi.

Madai ya uwepo wa kemikali sumu zinazosababisha saratani
Kwa muda mrefu sasa yamekuwepo madai yanayotoa taarifa kwamba miraba midogo unayoona chini (Sehemu ya mwisho) ya kasha la dawa ya meno ni aina fulani ya msimbo (Code) wa rangi ya dawa ya meno, inayoonesha asili ya kemikali zilizopo ndani ya dawa hizo.

Chapisho hilo linadai kuwa alama ya kijani inamaanisha kuwa dawa ya meno yote ni ya asili, alama ya bluu inamaanisha kuwa ina mchanganyiko wa viambato asilia na dawa, alama nyekundu inamaanisha ina viambato asilia na viambato vya kemikali, na alama nyeusi ina viambato vyote vya kemikali.

screenshot-2023-09-07-115755-png.2741849

Mojawapo ya picha ya madai hayo
Chapisho hilo linaonya watu dhidi ya kutumia dawa za meno zenye alama nyeusi au nyekundu na kuwahimiza watu kuchagua dawa za meno zenye kijani kibichi au bluu.

Ukweli wa madai haya upoje?
JamiiCheck imefuatilia suala hili na kubaini kuwa halina ukweli.

Watoa madai haya wameshindwa kutofautisha kati ya viambato vya asili na kemikali. Kitaalamu, sio kila kemikali ni mbaya. Hata hivyo, biadhaa za asili pamoja na viambato vyake navyo pia kimsingi huwa ni kemikali.

Pia, madai haya yamebeba maelezo ya jumla pasipo kuweka wazi aina ya kemikali zinazohusishwa na kusababisha saratani.

Makampuni hayaweki alama kwenye sehemu ya mwisho ya kasha la dawa ya meno kwa miraba yenye rangi kama sehemu ya kuhada watumiaji.

Alama zenye rangi hizo huwekwa ili kurahisisha zoezi la utengenzaji wa dawa husika kiwandani. Alama hizo husaidia vitambuzi vya mwanga kutambua mwisho wa makasha hayo, ili mashine zinazotumiwa kutayarisha makasha zijue mahali pa kukata na kufunga dawa hiyo.

Kwa lugha za viwandani zinazotumika kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, alama hizi hufahamika kama Eye Marks au Colour Marks, sehemu zinazotoa utambuzi kwa mashine ili bidhaa husika iweze kukatwa na kufungwa inapokuwa inatembea kwenye mashine. Alama hizi huhusisha bidhaa zilizoungana, ambazo huhitaji kukatwa ili kuzitenganisha.

Madai haya yaliwahi pia kukanushwa na Snopes, taasisi inayojihusisha na uhakiki wa taarifa pamoja na kampuni ya Colgate inayozalisha mojawapo ya bidhaa hizo.

Ufafanuzi mwingine wa madai haya uliwahi pia kutolewa kwenye mtandao wa Facebook, Julai 19, 2019 na Dr. Sohail Khan na Februari 17, 2020 kwenye Mtandao wa Linkedin.

Unawezaje kufahamu viambato vya dawa ya meno?
Kama ilivyo kwa vyakula na dawa, maelezo ya viambato vya biadhaa hizi hupatikana kwenye sehemu ya maelezo ya "Ingredients", ambapo kampuni na wazalishaji huwajibika kisheria kuwajulisha watumiaji viambato vilivyotumika katika kutengeneza bidhaa husika.

image.cfm

Mfano wa Maelezo ya Viambato (Ingredients) vya dawa ya meno ya Colgate.
Pamoja na uwepo wa viambato vingi vinavyotumika kwenye utengenezwaji wa dawa ya meno, wataalamu wa afya hushauri matumizi ya dawa za meno zenye kiambato cha Fluoride ili kuongeza uimara wa meno.
nyingi sana madukani ni black hili naona limewekwa kuchafua biashara za watu,nafikiri viambata vimeandikwa katika kila kifungashio hili la rangi ni uzushi
 
Black= all chemicals
Red=
Blue= chemical & medicine
Green= all medicine
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
 
Kawaida wale viumbe wenye elimu ndogo duniani hujiangaisha kuanzisha uzushi usiokuwa na mashiko ili mradi waonekana wanajua kitu fulani
 
Huu ni uzushi tu, watu wasiotumia vizuri akili hudhani kila kitu ni uchawi au muujiza. Hapo watakuambia pia inahusika na namba 666
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
Sio kweli mkuu, hizi ni nadharia tu. Tuliosoma pharmacy tunaelewe hakuna mpangilio wa kutoa label ya dawa kwa mtindo huo.
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
Mtalaam wa kilimo alituingiza chaka!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom