Msimamo wangu mwaka ujao!

Msimamo wangu mwaka ujao!

KARIA

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
717
Reaction score
473
Habari wana CC?
Nimeona niungane nanyi kuwaeleza mpango wangu wa mwaka 2013! Kuna kero moja kubwa inanisumbua sana nilijitahidi kiuvumilia naona nimeshindwa mimi! Hili suala la michango ya harusi kuna jamaa kumbe alishafunga harusi kijijini kwao, maisha yakamgomba si akatangaza nia kuwa anataka kufunga ndoa, kumbe ilikuwa janja yake apate hela afanye mambo yake!

Kuanzia January 01 Sitamchangia yeyote mchango wa harusi!
Michango nitakayo changa
1. Ujenzi wa nyumba ya IBADA.
2. Mchango wa ELIMU
3. UGONJWA
4. MSIBA.
 
Naunga mkono hoja mia kwa mia, nasimama then nagonga meza kuonesha msisitizo kama magambazz! Hujambo KARIA?
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru Maulana kanijaalia afya njema ijumaa ya leo Arushaone!

Hizo mambo kwa watu wa kanda ya north sidhani kama wanaweza kuacha kwani ishakuwa jadi. michango ikipita usipotoa unatengwa!
 
Last edited by a moderator:
Hizo mambo kwa watu wa kanda ya north sidhani kama wanaweza kuacha kwani ishakuwa jadi. michango ikipita usipotoa unatengwa!
Nikitoa ujue huyo mke ni wetu wote na ukinikuta nae uwe mpole maana na mimi nimechangia!
 
I've got an idea KARIA, naomba unichangie kwa kuwa nategemea kufunga ndoa na Mamzalendo mwishoni mwa January 2013 please cooporate.
 
Last edited by a moderator:
michango ya harusi mimi nilitangaza kuacha tangu mwanzoni mwa 2012
ingawa ni tabu kuacha ghafla lkn nashukuru hadi mwaka unakaribia kuisha
nimefanikiwa kutochangia nyingi tu. sasa 2013 ndio naacha kabisa.
 
Habari wana CC?
Nimeona niungane nanyi kuwaeleza mpango wangu wa mwaka 2013! Kuna kero moja kubwa inanisumbua sana nilijitahidi kiuvumilia naona nimeshindwa mimi! Hili suala la michango ya harusi kuna jamaa kumbe alishafunga harusi kijijini kwao, maisha yakamgomba si akatangaza nia kuwa anataka kufunga ndoa, kumbe ilikuwa janja yake apate hela afanye mambo yake!

Kuanzia January 01 Sitamchangia yeyote mchango wa harusi!
Michango nitakayo changa
1. Ujenzi wa nyumba ya IBADA.
2. Mchango wa ELIMU
3. UGONJWA
4. MSIBA.

Mimi hiyo Resolution nilijiwekea tangu Tarehe 01 July 2012. Na imenisaidia kweli kweli kujiimarisha kiuchumi...
 
Pacha TANMO mekumisije arifu.

Yaani Pacha, Pacha yaani, acha tu!! i cant explain nilikumisije.
Hasa katika kipindi hiki kigumu.
A%20S%20cry.gif
.............. Hujambo Pacha?
 
Back
Top Bottom