Msimamo wa Rais Dkt Magufuli dhidi ya ugonjwa wa Corona ndio ulikuwa mpango wa Mungu kwa Afrika

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MSIMAMO WA RAIS DKT MAGUFULI DHIDI YA UGONJWA WA CORONA NDIO ULIKUWA MPANGO WA MUNGU KWA AFRIKA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo nitazungumza mambo makubwa ambayo yatapambwa na ushahidi wa kiimani. Hivyo kwa wasomaji wangu ili uweze kunielewa juu ya makala hii utahitaji utulivu mkubwa wa akili.

Ieleweke kuwa kwa sasa Dunia nzima wimbo ni CORONA. Toka mwaka jana ugonjwa huu uliporiootiwa Rais wa Tanzania Dkt Magufuli ndiye Rais pekee aliyekuwa na msimamo tofauti juu ya kupambana na vita hii. Alikataa kabisa kuwafungia Watanzania ndani. Maana alijua hatari ya kuwafungia ingeleta vifo vingi kuliko kutokuwafungia. Mtanzania huyu mwenye familia ya watoto kumi unamfungia ndani mwezi unategemea atakula nini? Rais Magufuli alikata unyonge huu kwa kuwa alikuwa anajua Mpango wa Mungu kwa Afrika tangu kuumbwa kwa Dunia hii. Alisema unyonge basi!

Hali ya unyonge kwenye mkutadha wa makala yangu hii ni kitendo cha kuto kujiamini na kukubali kuburuzwa. Ni ukweli kuwa Afrika tumekubali kuwa Wanyonge pamoja na historia kubwa tuliyonayo katika Dunia hii. Kwa sababu tumeamua kufuta historia yetu na maagizo ya Mungu ndio maana bado watu wanaamini sisi hatuwezi kuuitibu Corona ila Wazungu tu. Ninaomba niwakumbushe mambo machache. Lakini kabla ya hapo tukubaliane kuwa maendeleo ni population. Huwezi kuwa na maendeleo makubwa kama una idadi ndogo ya Watu.

Divine promise inaeleza kuwa Yesu alishasema Afrika ndiyo itakuwa Madhabahu yake na nguzo Mpakani mwake. Kitendo cha JPM kusisitiza kuomba juu ya Corona ni juu ya ukamilifu na utimilifu wa maagizo ya Kiroho ambayo Mungu aliyaacha kwa Afrika. Mh Rais alijua ugonjwa huu ni mkubwa na wakati huo Tanzania hatuna Madaktari wa kutosha, hatuna hospitali za kutosha wala teknolojia ya kuweza kupambana na dubwana hili. Lakini akavuviwa kuwa tunahitaji kuomba kwa kuwa neno la Mungu ni upanga ukatao kote kote. Na neno lake linanguvu ya kuweza kuvunja mawe na miamba. Hivyo kwenda mbele za Mungu kumuomba kutuepusha na gonjwa hili ni sahihi kwa kuwa Mungu ni zaidi ya Madaktari na teknolojia zote.

Nimesema leo ninatumia hoja ya Kiblia kuungana na Mh Rais juu ya msimamo wake katika kupambana na Corona. Mungu hakuandika kuwa mkijenga mahospitali ndipo mtakuwa mumepona pamoja na kwamba Hospitali ni mhimu ila Mungu aliagiza kuwa Mkiomba nitajibu na moto wa Madhabahu hautazimika. Kwa tafsiri halisi kwa Magonjwa haya ambayo hayana chanjo wala tiba, yaani maradhi ambayo hadi sasa Mungu hajatuonyesha tiba yake kisayansi basi hatuna Budi kupiga magoti na kusali sana huku tukiendelea kuchukua tahadhari zingine zote. Kwani pamoja na Mungu kutupa uwezo huo ametupa maarifa mengine.

Dunia hii tangu kuumbwa Mungu alitupatia Afrika neema kubwa.Inawezekana kuna mahali tulifanya makosa, sasa ni muda wa kujisahihisha. Mapambano ya vita vya Corona na msimamo wa JPM ni maagizo ya Mungu aliyotuandikia Afrika. Ukisoma Biblia agano la kale Isaya 19:19-25 tunamuona Mungu akiitaja nchi ya Misri kuwa wa watamlilia Bwana juu ya watu wanaowaonea, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea naye atawaokoa. Anasema wakirudi kwa bwana atakubali maombi yao na kuwaponya. Anasisitiza kuwa itakuwepo njia kuu itokayo Misri na kufika Ashura hadi Israel.

Ukiutafakari hili neno utaona kuwa baada ya vita ya Corona Mh Rais alisema pamoja na tahadhari zingine zote Watanzania tuingie kwenye maombi. Rais alishaona kuwa hakuna silaha zaidi ya maombi kwani kitabu hiki cha Isaya kinaonyesha namna Mungu alivyoiandikia Afrika iwapo itajinyenyekesha kwake. Wazungu wao walikata kuomba wakasema tunafinga makanisa, sasa inapofunga makanisa na kufungua hospitali, Je hospitali zina nguvu ya kuponya kuliko roho mtakatifu? Huu ni wakati wa Afrika kusimama na JPM na kwenda kulikomboa bara hii ktk minyororo ya fikira na mawazo mgando juu ya kuwaamini Wazungu kwenye kila kitu. Afrika tumekuwa waoga kuamini mawazo yetu, lakini wakati huo Mungu alishasema utafika wakati Afrika itakuwa na uchumi imara kuliko mabara yote. Na ili kuwa na uchumi mzuri ataleta mtikisiko kwanza according to biblical perspective ( Isaya 19:24).

Lakini hata tusipoamini katika maandiko, basi tunaweza kuamini ktk ushahidi wa kihistoria na kisayansi.Kwanza tukubaliane kuwa Dunia nzima binadamu wa kwanza kuishi Duniani, Kisayansi na kihistoria inatuthibitishia kuwa aliishi Afrika. Bonde la Olduvai George Tanzania ndiko inasemekana binadamu wa kwanza Duniani aliishi. Hii ni hoja ya kwanza kuwa tunapaswa kujiamini na tunaweza kushughulikia mambo yetu. Kama binadamu aliishi Afrika kwani ni dhambi Afrika kugundua tiba ya Corona? MUNGU alishaanza kutupendelea na kutupa ufunuo huu toka zamani kwa Binadamu wa kwanza kuishi Duniani. Ni mzazi gani mwanae akimuomba Mkate atampa Nyoka? Sisi ni watoto wa kwanza wa Mungu hivyo tukimuomba ktk roho na kweli atatupa tunachostahili. Mwaka jana tuliomba ktk roho na kweli Mungu akatunusuru na Maiti tulizoambiwa zitazagaa mabarabarani.

Hoja ya Pili ambayo bado inatubeba Afrika ni kuwa wasomi wa kwanza Duniani walianza Afrika. Haya yote yanaonye mapenzi ya Mungu kwa Afrika. Afrika ndilo bara la kwanza kuwa na wasomi na ndio Bara la kwanza waliogundua maandishi. Ushahidi wa kisayansi na kihistoria unatuthibitishia kuwa Misri ambayo ipo bara la Afrika ndiko yalikogundulika maandishi. Hivyo ufahamu wetu ni mkubwa kuliko mtu mwingine. Mungu alishasema utafika wakati Afrika itaiongoza Dunia na haitakuwa mara ya kwanza kuongoza kwani Afrika ilishawahi kuongoza Dunia kwa miaka saba. Nitawapa andiko lake wapi imeandikwa hivyo. Tusiwe wanyonge, ni wakati wa Afrika kwenda kuipindua Dunia. Ni wakati wa Afrika kuungana, ni wakati wa Afrika kumuelewa JPM na ni wakati wa Watumishi wa Mungu kuwaambia ukweli huu Waafrika.


Kwa sisi ambao tunaamini katika ukristo tunaambiwa Afrika ndilo bara la kwanza kuwa tajiri Duniani kabla ya kupinduliwa. Afrika imeshawahi kuilisha Dunia kwa miaka saba. Neno la Mungu linatueleza kuwa Yusufu akiwa Waziri Mkuu hapa Afrika (Misri) chakula cha kulisha Dunia kilitoka Afrika. Afrika ndilo bara ambalo linatajwa kumpokea Yesu. Hivi hamkumbuki kama Yesu baada ya kufukuzwa na Herode alikuja Afrika? Lakini baadaye kadiri dunia ilivyokuwa ikiendelea tulisauhau agano la Mungu la kuomba na kusali basi tukavurugwa tukakubali kuvurugwa na leo tunatawaliwa watu ambao tuliwalusha kwa miaka saba. Lakini ukisoma kitabu cha Isaya 19 basi hizi ni dalili tosha kuwa tena Afrika inaenda kuikalia Dunia.

Neno linasema Afrika itakuwa ya Kwanza na kufuatiwa Ashura na ya Tatu itakuwa Imara. Ashura Kiblia ni Bara la Asia.

Ninaamini makala hii itaendelea kuwapa imani Watanzania wenzangu juu ya vita hii ya gonjwa la Corona. Lakini makala hii ituongezee ali kuwa vita hii si yetu pekee yetu, bali ni vita inayomhitaji Mungu.

Lakini hata hivyo tunapaswa kuwa na tahadhari na hizi chanjo za kuletewa. Hakuna adui ambaye ameshawahi kumpenda adui yake. Tukubali au tukatae hatujawahi kuwa rafiki wa hawa watu. Hawa ni marafiki zetu si kwa hasara, wao wanafaidika kuliko sisi. Nchi zao ili ziweze kwenda mbele wanahitaji zaidi malighafi zetu. Ili waweze kuchukua kirahisi ndio maana wamekuwa wanatengeneza conflict ili wapate mianya ya kuingia.

Nitoe tu mfano mdogo. Hivi ni nani aliyetuletea dawa za uzazi/ Majira ya uzazi? Siyo hawa? Leo ni akina Mama wangapi wanaumwa uzazi? Utafiti unaonyesha wanawake wengi waliowahi kutumia au wanaotumia dawa za uzazi wanapata magonjwa ya uzazi. Lengo lao lao lilikuwa kupunguza population ya Afrika, maana wanajua tukiwa na Idadi sawa na wao tutawakuta kimaendeleo na kuwaacha. Huwezi kuendesha nchi bila nguvu kazi ndio maana kwao walishajaa.

Maana yangu ni kuwa hata Corona wanaweza kuwa ni wao walitengeneza kwa njia ya kutupunguza, lakini Mungu akawageuzia kibao. Hivyo wanaweza kuleta chanjo ambazo ndizo zikasaidia kusambaza gonjwa hili na nia yao ikatimia.

Tunahitaji kuwa makini na kumuelewa sana Mh Rais ambaye ameonyesha msimamo wake wa Kimungu. Tusilazimishwe kufuata ushauri wao. Hawajawahi kutupenda, ila wanapenda rasilmali zetu.

Huu ni ukamilifu wa unabii ambao kama Africa tutaenda kusimama kwa sauti moja, basi Afrika inaenda kushika hatamu ya Dunia.
 
Dini zenyewe ni mapokeo ya haohao waliotengeneza chanjo! Ila mnajikuta wajuaji sana!

Haya yote ni serikali inakwepa majukumu yake ya msingi kulinda Afya za wananchi wake😢

Leo hii, hata ARVs zikiacha kupokelewa kwa msaada (likawa jukumu la serikali kununua) nakuhakikishia nyie wapuuzi mtakuja na ngojera nyingi za kumkingia kifua huyo jamaa wenu ambaye haya yote mnafanya kumridhisha.
 
Wewe ni mpuuzi sana kwani ni lini Mungu na huyo Magufuli walikaa na kupanga mipango? acha kumuingiza Mungu kwenye mambo ya hovyo na mbona usiseme walipanga kudhulumu korosho na mazao mengine.eti mpango wa Mungu shame on u
 
Mungu amekataza kumwabudu mwanadamu. Ninyi na viimani vidini na vyenu vya kuokoteza mmemgeuza huyu jamaa yenu Mungu wenu. Kwanza kama ungekuwa msomaji wa maandiko matakatifu ungetambua kuwa haya mahangaiko na matatizo yote ya dunia hii ikiwemo CORONA mwanadamu ukiwemo wewe, jamaa yako na mimi tulijitakia wenyewe kwa kukiuka maagizo na kutomtii Mungu.

Baada ya ukaidi ule tuliadhibiwa kwamba tangu wakati huo tutakula kwa jasho, yaani tutahenyeka hapa duniani na miiba na michongoma itatuchoma. Korona inatuchoma kweli kweli na ni haki na halali yetu kupatwa na yote hayo. Kwa hiyo tukipewa chanjo feki, tukifungiwa ndani au tukiachwa kuendelee na maisha kama kawaida na kukipata cha mtema kuni hata kufa kwa janga hili ni halali yetu.

Tunavuna tulichopanda. Kwa hiyo kumsikia mtu anasema hataki barakoa, hataki chanjo, n.k ni ujinga tu. Kuvaa barakoa hata kama unaona ni bughudha ndio kula kwa jasho huko. Maana yake tukichagua maisha ya mateso, maisha ya mahangaiko, maisha ya vipigo vya kila namna. hapa hakuna wa kumlaumu. Eti mnayalaumu mataifa ya nje kwamba yanawaletea barakoa! Ama tuletewe au tutengeneze barakoa wenyewe yote ni mateso tuliyojitakia.

Tutulie tunyolewe vizuri kabisa. Maandiko matakatifu yanasema mshahara wa dhambi ni mauti. haya ndiyo mauti yenyewe tuliyoyachagua wenyewe. hakuna wa kumlaumu. Ni kuomba tu msamaha kwa Mungu lakini siyo kujitutumua kama kwamba tuna haki fulani au tunaonewa na mtu fulani.
 
Acha kumshirikisha Mungu kwenye mambo ya ajabu! Watu wanazikwa mtaani kila uchao ww unajua?
 
Ninyi ndio huwaaminisha watu wale vinyesi, majani na kukanyaga mafuta ili wapone. Matokeo yake wanakufa. mna la kujibu mbele za Mungu hata kwa kumwabudu na kumsujudia huyu jamaa yenu muuaji mkubwa.

kuna damu za watu wengi zinamlilia. na ninyi mtaibeba laana hiyo. Haiwezekani kila wanayetofautiana naye ama apotee au apigwa risasi na ninyi mnaona sawa tu.
 
Viimani na vidini vyenu vya kuokoteza hivi vitawawafanya misukule ya kumsujudia na kumwabudu huyu jamaa yenu katili asiye na chembe ya roho ya utu.
 
Lockdown:
Kama tulitakiwa kuweka lockdown iliipasa serikali kuingia mfukoni na kufidia hasara mbalimbali za shughuli za watu za kujiongezea kopato.
Pia iliipasa serikali kuhakikisha wanannchi wake wanapata yale mahitaji muhimu wakati wote wa lockdown.
Ikienda sambamba na kupunguza gharama za huduma mbalimnali kwa jamii.


Sababu kubwa iliyotufanya tukakataa kuweka lockdown ni swala la UCHUMI wetu mdogo. Hatuna uwezo wa kutekeleza hayo hapo juu.

Kinachoendelea sasa ni UBISHI.
 
Unachekesha
Huku unaamini biblia (kuhusu binadamu wa kwanza) kisha unadai kisayansi binadamu wa kwanza katokea Olduvai Gorge
Kama una watoto usipeleke watoto kupata chanjo bali wapeleke wakakanyage mafuta kwa Mwamposya
 
Watu na bahati zao, so mtoa mada unataka niambia kwamba Mheshimiwa anakaa na sir God kiti kimoja wananza kutetea juu ya afrika!?.. mkisifia kitu msifie kwa kipimo. Ngoja uteuzi ushasikika
 
Hivi watu wengine kwenda chooni kunya mnangoja nini kuliko kuja kuharisha humu?
 
Ingawa nimesoma heading tu, huyo Mungu wako mliwasiliana wapi mkaongea haya ?, Next time umwambie kuna njia nyingi na rahisi za kuwakilisha mipango yake and not this barbaric ways, by the way umeongelea Afrika kwa imani yako wale wengine sio watu wake ?

NB: Mkumbushe pia magonjwa mengine kama malaria ukimwi n.k. yanatuangamiza sana sisi anaotupenda kushinda hata Corona inayvowaangamiza wale ambao unasema labda hawapendi ebu nikumbushe pia hizi ramani kwamba afrika inaishia pale inapoishia ni yeye pia alichora?
 
Acha kumshirikisha Mungu kwenye mambo ya ajabu! Watu wanazikwa mtaani kila uchao ww unajua?
Mwanzoni kabisa wa uzi, mtoa mada aliwaambia mtulize kichwa halafu msome kwa umakini. Inaonekana hata paragraph mbili hujamaliza, unapayuka tu. Hamna kitu binadamu anachofanya ambacho Mungu hana uwezo juu yake
 
Back
Top Bottom