Msimamo: Napinga TBC kurusha Live Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,667
218,171
Kwa miaka mingi sana tangu kuondolewa kwa Tido Mhando kwenye uongozi wa TBC , Channel hii imejipambanua bila kificho wala uoga wowote kama channel ya ccm , kwa kuonyesha kila kinachofanywa na ccm hata mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa Taifa hili , imewapuuza wapinzani katika kipindi chote hicho huku ikiwanyima hata nafasi ya kukohoa tu kwenye mic zao , Watangazaji wake wamekuwa makada halisi wa ccm wenye kusifia hata ukandamizaji , hoja zote zenye tija hazijawahi kupewa nafasi kwenye TV hii .

Kwa tabia hii TBC imepoteza kabisa watazamaji katika nchi hii baada ya wananchi kwa umoja wao kuidharau moja kwa moja , nini kimetokea leo kwa TBC kutangaza mkutano wa Chadema , Je TBC inatafuta umaarufu kupitia mgongo wa Chadema baada ya wananchi kuipuuza ?

Napinga jambo hili na sitakubali Chadema itumike kama ngazi , waendelee kuifagilia ccm sisi tutapita nyumba kwa nyumba .

Naomba kuwasilisha .

UPDATES :
Mwenyekiti wa Chadema Mh Mbowe amewatimua TBC kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Urais Mbagala Zhakhiem kwa tuhuma za hujuma
 
Tbc siyo kwa ajili ya wanasiasa tu, hata wasio wanasiasa wanalipa kodi na wana haki ya kuwasikiliza wagombea wote ili wafanye maamuzi sahihi.

Cha kufanya wewe pinga nyumbani kwako kutazama TBC, usiwaze kichadema chadema muda wote.

Hata mimi binafsi nasubili kwa hamu nifuatilie mkutano huo kupitia TBC.

Wenzenu ccm wana Channel ten nyinyi sijui mtaamka lini kujuwa umuhimu wa kumiliki tv station yenu, yani mnazidiwa maarifa hatanna wahuni tu kama kina Majizo?
 
😀😀😀😀
Ni wewe au!! Viongozi wako wapo upande wako!!! 😀😀😀
Mliwasema sana.. sasa wamewasikia.. si mufurahie mnasaidiwa kupata wapiga kura au!!.. TCRA nayo inawasaidia kwa wale wanyonge.. wasio weza kusikiliza tena vipindi vyao kwenye radio yao pendwa.. wamekasirika.. na wanafikiria wali wa Rungwe na wengine.. wawape kura.. kisa TCRA kuruka wengine na kuadhibu Clouds Media.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom